Rais Samia, usipoteze dhumuni la kuifanya Dodoma kuwa jiji la mfano kimpangilio

Mipango miji ni taaluma sio siasa. Ikiwa tumefikia mahali wakina Kunambi ndio wanaopanga mji kama Dodoma uwaje matatizo hayako mbali. Kupanga aina ya mabati ya kuezeka sio kigezo cha ubora wa mipango miji. Na umenitisha zaidi uliposhauri watumike wanafunzi kwenye suala hili nyeti. Tukifuata ushauri wako ndio utakuwa mwisho wa Jiji la Dodoma lenye staha.

Amandla...
Umemaliza kila kitu. Huyu jamaa inalekea ni wale wanaodhani wanasiasa ni wabobezi wa kila kitu. Na bila shaka kwake kiongozi mbovu kama alivyokuwa Makonda, atasema ni kiongozi mzuri. Kma ulivyosema mji unapangwa na wataalam na hupangwa kitaalam kabla. Nji kama Dodoma bila shaka kama walizangatia sheria utakuwa ulishapangwa na haiwezekani kila mkurugenzi aingie na ''ufundi'' wake.
 
Suala la Rangi za mapaa halipo practical.... kuna Rangi nyingine hazifai kuwekwa hapo Dodoma kutokana na climatic condition. Hopefully Mkurugenzi wa Jiji wa sasa ambaye ni Town Planner mzoefu analifanyia kazi hili.
Rangi za mapaa??? Kwamba hali ya hewa itaziathiri vip????
 
Kilichoniuma ni kufutwa kwa mpango wa ile barabara ya mzunguko! Nasema kufutwa kwa sababu hata watu wameruhusiwa kuendelea kujenga nyumba maeneo yao ambayo barabara ingepita na mwanzoni walizuiwa kuendeleza. Hii ina maana hakuna tena mpango wa kuijenga hiyo barabara kwa miaka ya karibuni! Very sad!! Vinginevyo basi itakuwa ni ufisadi kwa maana ya kwamba watu waruhusiwe kujenga huku wakijua ni eneo la barabara ili kesho watu wajklipe fidia ya mabilioni ya pesa! Au ina maana tunapingana na salamu yetu ya "kazi iendelee"? Sijajua kipi kimelengwa kati ya kupiga hesabu ya kufanya ufisadi kupitia fidia na kupingana na dhana ya kazi iendelee. Yote ni mabaya !
 
Umemaliza kila kitu. Huyu jamaa inalekea ni wale wanaodhani wanasiasa ni wabobezi wa kila kitu. Na bila shaka kwake kiongozi mbovu kama alivyokuwa Makonda, atasema ni kiongozi mzuri. Kma ulivyosema mji unapangwa na wataalam na hupangwa kitaalam kabla. Nji kama Dodoma bila shaka kama walizangatia sheria utakuwa ulishapangwa na haiwezekani kila mkurugenzi aingie na ''ufundi'' wake.
Mpango wa awali wa Dodoma ulitayarishwa na wa Canada lakini ukiondoa drainage system ba Area C hamna kilichofuatwa. Wana siasa wakawa wanajiamulia wanachotaka. Hata huo mpango wa sasa nina shaka nao.

Amandla...
 
hakuna mji wa hovyo kama Dodoma dunia hii, na hakuna watu wajinga kama wa Dodoma ,ndio maana ikawekwa ngome hapo
 
Back
Top Bottom