Ndugu Rais.
Huku mtaani wananchi wana shock kubwa, hawaamini kinachoendelea nchini.
Wanasema kwa mujibu wa mashitaka ambayo serikali yako imemfungulia Lissu, huenda akanyongwa mpaka kufa. Idea hiyo pekee inawapa wananchi ganzi, simanzi na kwa kweli inawafanya wakuchukie.
Na makada wa CHADEMA wanawaambia wananchi kwenye mikutano ya hadhara kuwa serikali yako inataka kumnyonga Lissu.
Kesi hii ndugu Rais, inawafanya watu wakuone kama huna moyo hivi. Tafadhali kabla ya haiba yako haijachafuka na watu kukuona mtawala katili, tafadhali ondoa hii kesi mahakamani.
Soma Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025
Tunapoelekea utaanza kuchukiwa na umma kama kipindi kile ulivyoendelea kumshikilia Mbowe gerezani, Kesi ile ilikuwa imekutoa ktk mioyo ya Watanzania sana na laiti ungeng'ang'ania kumshika Mbowe kwa muda mrefu zaidi, umma ungekuona kwa jicho negative sana. Sasa situation kama hiyo ninaiona sasa ambapo umma umeanza kukuangalia kwa jicho baya.
Ndugu Rais, Serikali yako inaongoza kwa kuwaweka wapinzani wa utawala wako jela. Ushanuweka Mbowe ndani kwa kesi ya Ugaidi, Ushamfungulia Dr Slaa, Mwabukusi na Mdude kesi ya Uhaini, na sasa Lissu serikali yako imemfungulia kesi ya uhaini. Wananchi wanasema unatumia mahakama kisiasa kupitiliza. Wanakuona kuwa huwezi kujibu hoja za wapinzani kwa hiyo badala yake unatumia msuli wa dola!.
Ndugu Rais ni kweli unaweza kumuweka Lissu jela na hata kumnyonga, lakini kiukweli hii dhana ya kumnyonga Lissu inaibua hisia nzito mno kwa wananchi huku mtaani na watu wanakuangalia vibaya sana.
Ujumbe nimekufikishia, utaamua mwenyewe serikali ifanye nini, Wananchi hawaamini kuwa mahakama inaweza kuwa huru kutenda haki kulingana na historia ya kesi hasa za hivi karibuni, kwa hiyo wananchi wanasema kuwa hii ngoma ni yako na si mahakama.
Kumnyonga Lissu kwa maoni yangu is not a good idea!.