beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi eneo la Tegeta Mkoani Dar es Salaam amesema Tozo zitaendelea kuwepo na hataki kuficha hilo

Amesema, "Tuliweka tozo kwenye mambo ya fedha za mitandao, yamepigiwa kelele sana, nimesikia. Nimekaa na Wataalamu tumepunguza 30%. Miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya kama Bilioni 60 na zimepelekwa kujenga Vituo 220 vya Afya"

Ameongeza, "Januari tuna wimbi kubwa la Watoto wanataka kuingia Sekondari, lakini wapya wanaoingia Darasa la Kwanza. Hakuna wa kutujengea ni sisi wenyewe. Fedha zitakazokusanywa Septemba na Oktoba zitaenda kujenga madarasa zaidi ya 500"
 
 

Attachments

  • Rais samia kuhusu tozo.mp4
    2.8 MB
Namwonea huruma Rais Samia. Namwunga mkono katika mengi. Aliponikwaza ni kwenye kesi ya kumbambikia Mbowe. Lakini najua siyo maagizo yake.

Naelewa shida kubwa ya upungufu mkubwa wa fedha aliokutana nao kutokana na sera mbaya za uchumi alizokuwa amezianzisha marehemu.

Rais Samia hana namna, la sivyo mambo mengi yatasimama. Wakati tukiendelea kutozana ili kuokoa jahazi, juhudi kubwa zielekezwe kwenye kubadilisha sera na sheria ili zivutie na kuimarisha uwekezaji.
 
Kuna watu walikuwa wanasema mama anaingizwa chaka,kumbe mama ndio anaidhinisha matukio yote katika nchi hii,nasikia mtima wangu unavuja damu.
Na ndiye huyu huyu anaye mjaza upepo, dharau na kiburi yule Waziri wake wa fedha!
 
Very Magufuli-like statement.
Ukimsiliza vizuri Samia anasema: TOZO ni kwa sabu siasa za CCM zimekataa masharti ya Wafadhili/ MABEBERU.
TOZO ni UFISADI na UJAMBAZI wa matumizi mabaya ya madaraka.
CCM imepoteza uhalali Tanzania.
CCM hawataki kuheshimu maamuzi ya wanachi kwenye chaguzi.
Tunaongozwa na MAJAMBAZI Samia, Mpango, Majaliwa na Mwigulu.

CCM = Chama Cha MAGAIDI
 
Ukimsiliza vizuri anasema: TOZO ni kwa sabu siasa za CCM zimekataa masharti ya Wfadhili/ MABEBERU.
CCM hawataki kuheshimu maamuzi ya wanachi kwenye chaguzi. CCM imepoteza uhalali Tanzania. Tunaongozwa na MAJAMBAZI Samia, Mpango, Majaliwa na Mwigulu.

CCM = Chama Cha MAGAIDI
Wewe upo kisiasa mimi siko huko. Mama kasema ukweli, nchi yetu itajengwa na sisi wenyewe, watoto wetu tumewazaa wenyewe na tutawasomesha sisi wenyewe. Hiyo ya kutegemea mfadhili nao ulikuwa upumbavu tu kama upumbavu mwingine, na pia ni laana kuishi kwa kudra za watu wengine.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom