Rais Samia, The Royal Tour isiache maeneo haya...

Sema dunia inabadirika sasa hivi tunaingia kwenye utalii wa teknolojia inabidi taifa tulitambue ilo. Hizi mambo sijui asili asili zinaanza kukosa ushawishi. Hivi kwa nini dubai inavutia watalii wengi na ikiwa haina mbuga ata moja?
 
Lake Ngozi
Lake Ngozi! Ndiyo ziwa Mbeya?
Lake Ngozi ninaijua kwani mwaka 1968 niliitembelea na kupiga kambi hapo kwa siku tatu, ila hiyo haiko Mbeya labd ungesema barabara ya Chunya Kawetere kwenye eneo la barabara iliyo kina kirefu kutoka usawa wa bahari katika Afrika, (highest Road Point above sea level in Africa).
 
Lake Ngozi! Ndiyo ziwa Mbeya?
Lake Ngozi ninaijua kwani mwaka 1968 niliitembelea na kupiga kambi hapo kwa siku tatu, ila hiyo haiko Mbeya labd ungesema barabara ya Chunya Kawetere kwenye eneo la barabara iliyo kina kirefu kutoka usawa wa bahari katika Afrika, (highest Road Point above sea level in Africa).
Nilikosea mkuu. Kawetere papo safi. Pia hata Kiwira hadi Kyela hasa Matema Beach napo kunahitaji kutangazwa. Ni kuzuri mno.
 
Ugawaji huu wa coordinates kama njugu, unafanya wanausalama wetu kuwa na kazi ngumu
 
Hujui utalii unakua kwa sababu zipi, Kagame na Netanyahu walikuwa wanatumia Royal tour kwa ajili ya propoganda tu ili kuficha uhalifu wao dhidi ya binadamu wengine.
 
Amani iwe nawe Mama yangu!

Kwanza napenda kukupongeza kwa hii creativity kubwa uliyokuja nayo ya kushiriki na kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia kupitia program maarufu ya “The Royal Tour”

Program hii kwa ufahamu wangu imezinyanyua nchi nyingi sana katika sekta ya Utalii na Uwekezaji Mf. Ni Israël waliyofanya kupitia Waziri Mkuu Mstaafu kipindi Benjamin Netanyahu mwaka 2014, Rwanda kupitia Paul Kagame mwaka 2018 na Jordan ambao walifanya kupitia Mfalme wao.

Kwa miaka mingi sana, Tanzania tumekuwa tukilalamika kuwa tuna rasilimali nyingi, wanyama, mito na mabonde Ila Serikali yetu imekuwa ikilala katika kutumia vitu hivyo na kulinufaisha Taifa.

Kwa upande wa vivutio, Tanzania tuna vivutio vingi na vizuri kuliko nchi za Morroco,Misri, Algeria na South Africa ila hata siku moja hatujawai kufikisha hata Watalii Mil 2 kutembelea nchi yetu. Nchi hizi nilizozitaja kwa mwaka zinapokea Watalii si chini ya Milioni 5.

Swali nililokuwa ninajiuliza siku nyingi ni Je endapo sekta yetu ya utalii ingekuwa inaingiza at least watalii milioni 3 Au 4 tu kwa mwaka , Leo hii Tanzania tungekuwa wapi? Kwa maana pamoja na sekta hii kuongoza katika kuchangia pato la Taifa kwa miaka mingi kabla ya corona, Tanzania hatukuwai kufikisha watalii hata Mil 2 kwa mwaka.

Pamoja na kutoa pongezi zangu kwako Mama Samia kwa hii creativity ambayo hakika nina uhakika wa asilimia 100 itaenda kuipaisha zaidi na zaidi Tanzania , naomba katika ziara yako hii usisahau kuwapitisha watu hawa kwenye maeneo haya

1. Vitalu vya Gesi LIndi na Mtwara ili kuonesha kwa kiasi gani nchi yetu ina huu utajiri wa Gesi. Ikumbukwe, pamoja na changamoto za kiuchumi za dunia, Gesi ni bidhaa adhimu sana

2. Mashamba ya wananchi na Wawekezaji ya Parachichi katika Mikoa ya Njombe na Iringa. Hii ni Kwa sababu sasa hivi duniani Parachichi inafahamika Kama Dhahabu ya Kijani na ndo tunda lenye thamani zaidi kutokana na demand yake huko duniani. Ni wakati sasa Dunia ioneshwe bidhaa hii adhimu inapatikana kwa wingi na ubora unaotakiwa hapa Tanzania ili watu wa Dunia waje kuifuata hapa Tanzania na wananchi wetu waizalishe kwa wingi.

Kwenye hili usisahau pia kuwapitisha kwenye mashamba ya Korosho Kwa sababu korosho pia ni bidhaa iliyokuwa na demand kubwa

3. Madini ya Chuma, Nickel na Dhahabu. Mama Dunia sasa ina uhitaji sana wa haya Madini, ni vizuri kuitangazia dunia kupitia programs hii kuwa yanapatikana kwa wingi hapa Tanzania na Dunia inakaribushwa kuyanunua kupitia masoko maalum tuliyoyaanzisha. Si vibaya wapiga picha wa Royal Tour wakafika kwenye haya Masoko kwenye mikoa kama Mwanza na Geita kuchukua video za masoko husika.

4. Viwanda vya bidhaa mbalimbali za Tanzania ikiwemo maeneo huru ya uwekezaji yaliyotengwa na Tanzania. Naomba pia uwapitishe wapiga picha hawa kwenye haya maeneo, wajionee kwa Jinsi gani tunaza

Mwisho napenda kumalizia kwa kusema, una kwenda vizuri, Mwenyezi Mungu akutangulie kwenye majukumu yako na Tanzania izidi kufaidika zaidi kiuchumi na kimaendeleo
Umeelezea vizuri sana tatitizo ni kuwa Tz hakuna INFRASTRUCTURE plus hakuna ENERGY plus WATER hivi vitu ni muhimu sana hawezi kuja muekazaji wakati hakuna mambo hayo wakati Dunia haiko hivyo ,baada ya kumfanya muekezaji anakuja kujenga kiwanda inabidi aje na umeme wake na maji yake hiyo ndio shida.
 
Naomba afike na kule Mbeya, kuna ziwa linaitwa Ngosi, na kule Songwe kwenye kimondo. Ila ziwa nasikia lina masharti ya kufika huko😂
Nimefika huko mkuu. Lake NGOSI. Unasalimia tu pale ofisi ya kijiji unaanza safari ila mlima ni mkali sana. Unahitaji watu wenye pumzi za kutosha.
 
Sema dunia inabadirika sasa hivi tunaingia kwenye utalii wa teknolojia inabidi taifa tulitambue ilo. Hizi mambo sijui asili asili zinaanza kukosa ushawishi. Hivi kwa nini dubai inavutia watalii wengi na ikiwa haina mbuga ata moja?

Umeona mkuu hata mm naona hilo tujitahidi pia kuwekeza kwenye utalii wa bata eg kuboresha beach zetu, kutengeneza mahoteli na kumbi kubwa za mikutano
 
Sambamba na royal tour. Wakuu wa mikoa wangeweza kuratibu maeneo ya mikoa yao ambayo yana vivutio mbali mbali. Mzee wa toronto na kisarawe wakati wa Jokate walifanya hilo vizuri sana.
 
Umeona mkuu hata mm naona hilo tujitahidi pia kuwekeza kwenye utalii wa bata eg kuboresha beach zetu, kutengeneza mahoteli na kumbi kubwa za mikutano

Ndio ndio dunia ya sasa mtu anatafuta hela ili atumie tuwekeze huko
 
Back
Top Bottom