voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Kwamba Tanzania Royal Tour ilikuwa ni siasa, Royal Tour ilikuzwa kuliko uhalisia wake.
Na pia Royal Tour Documentary haikuwa na maudhui yoyote makubwa yenye ushawishi kwa watalii kuweza kuijua Tanzania pamoja na vivutio vyake.
Bali Royal Tour ilitumika na kundi la wajanja ndani na nje ya nchi hii,ili kumuweka Rais Samia karibu yao zaidi.
Na hatimae kutimiza malengo yao kisiasa na kiuchumi.
Nimeweka video links hapa,za Documentary mbili tofauti,moja ni hiyo Royal Tour,na ingine ni ya mzungu binafsi aliyetumia pesa zake kiduchu,na hatimae kuitangaza Tanzania kuliko hiyo Royal Tour.
Na hapo muelewe kwamba Royal Tour ilitumia zaidi ya Bilioni 12,huku majina ya wachangiaji yakiwekwa kapuni mpaka leo hii