Rais Samia: Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya Afya na Elimu baadhi zinatozwa kodi kwa sababu zinafanya biashara

BAQWATA Wana hospitali ngapi?
Post ni nzuri TU....

Post ni yenye KULIJENGA TAIFA LETU....

Ila kama ADA ya baadhi ya watu....unataka kuleta hasama za tofauti ili mjadala uharibike.....

Kwani BAKWATA wanazuiwa kuanzisha HOSPITALI ?!!

Kwani BAKWATA wanazuiwa kuingia MoU na Serikali juu ya masula ya taasisi za afya?!!!!

BAKWATA na wenzao mbona wanatoa ITHIBATI kwa wawekezaji binafsi wa afya kulitumia jina la "ARAFA DISPENSARIES&ARAFA HEALTH CENTERS"?!!!!
Ama kwa sababu hujaziona "ARAFA HOSPITALS"?!!!

Hulifahamu hilo ?!!!!
 
Kumbe Serikali nayo inapambana ili itajirike... Duh
 
Hiyo iko sawa, haiwezekani usitozwe kodi afu gharama ni kama anayetozwa.
Wanataka wafutiwe kodi,,lakini wao hawataki kupunguza gharama zao wanaziwatoza wananchi,,hiyo haiwezekani,,
Si kila mtu ataanzisha dini,hospitali na shule sasa,,
Walipe kodi ama gharama zipungue kwa asilimia 70.
 
Wanataka kutajirika kwa migongo ya masikini,,
Walipe kodi tu
 
Inapmilikiwa na nani hiyo Aghakan mkuu?
Bora aghakhan haipati ruzuku ya serikali,,hospitali kama bugando ni ya dini,inapata ruzuku na madaktari wanalipwa na serikali,,lakini gharama ziko juu mno,,kama wameshindwa zitaifishwe tu,,
Mbona Benjamin mkapa hospital ni ya serikali na inajiendesha vizuri kuliko hata hizi za dini?
 
Kweli aiseee, sasa unakwenda hospitali ya serikali unakuta huduma zenyewe mbovu, pamoja na kulipa,bado uwahonge tena ,mara uambiwe hatuna dawa fulani,kanunue pharmacy ya nje, yaani usumbufu tupu, lakini hospitali nyingi za dini, huduma zao mara nyingi ni nzuri na za haraka na uhakika bila mizunguko, kwa hiyo hata gharama ikiwa almost sawa na za serikali au watu binafsi, mie mwananchi kitu ninachotaka nimepata huduma ninayo stahiki na bila usumbufu... Hospitali za dini tena unakuta ziko hadi peripheral vijijini kwetu na kwa kweli ni stakeholders wazuri, wanaosaidiana sana na serikali kuleta maendeleo. Hivyo serikali haina budi kuwafikiria kwa jicho la tatu ktk kodi hizo ili kuona jinsi gani, wanaweza kusaidia hata angalau kuwapunguzia viwango vya kodi hizo.... kazi iendelee.
Quality ya kinachotolewa inaweza kuwa tofauti Sana. Binafsi isiyo dini quality yake huwa Ni poor na hivyo gharama kuwa chini. I stand to be corrected
 
Nailed mkuu, hivi ile hospital iliyoko jijijini kati Arusha ya cct/kkkt nayo kweli inatoa huduma au biashara?😂😂😂
Nafikiri kayombo awaite awape elimu ya mlipa kodi😅😅
 
Hizi taasisi za dini kwa mtazamo wangu zinaomba kupunguziwa kodi ili nazo zipunguze gharama za huduma zao, kama tujuavyo hospitali za serikali nyingi zina huduma mbovu, unaweza kosa hata kidonge cha Panadol, huu ndio ukweli.

Sasa hizi hospitali za dini zilikuja kuwa kama mkombozi, lakini ghafla zimegeuka na kuonekana wanyonyaji kwasababu huduma wanazotoa haziwezi kuendana na gharama wananchi wanazotaka, kwa kuthibitisha hili, watu waangalie huduma zinazotolewa Muhimbili na gharama zake pale kama huna bima utapata tabu, then waone kama zinatofauti kubwa na hizo hospitali za dini.

Ukweli ni kwamba, huwezi kutoa huduma za viwango vya kukidhi mahitaji ya wagonjwa wetu kwa gharama ndogo coz wengi wana hali mbaya kiuchumi hizo hospitali zitashindwa kujiendesha, na kama zikishindwa kujiendesha, serikali ndio italemewa na mzigo mkubwa zaidi.

Hivyo badala ya wengi kushupalia hizo taasisi za dini zitozwe kodi kwasababu wanafanya biashara akiwemo Rais, vyema wajue na upande wa pili wa shilingi, la sivyo wagonjwa ndio watakaoteseka zaidi, itakuwa huku gharama kubwa za matibabu, ila kule panaendeka lakini huduma mbovu.
 
Nakuunga mkono
 
nafikiri serikali ingeweka standard ya mishahara kwa sekta zote .lakini gharama haziwezi kuwa sawa kwa sababu ,huko public institutions serikali inapelela mishahara.Private inaetegemea hela kutoka kwa mteja tu. serikali ingesaidia kutoa ruzuku kwa private institutions gaharama zingepungua sana
 
Dah, taasisi ya kishetani iyo
Mkuu inatia hasira ,na anayewakataa ni Sister wa kitambaa ndio Incharge wa hapo,sasa jiulize hata ule uungwana wa kwaida ukowapi achilia mbali huo Udini wanajivika
 
Mimi ningeshauri serikali iwe na hospitals zake za kanda za rufaa pia kiondoa hizo DDH. Kama wameweza shule kila kata nadhani hawashindwi kujenga hizo Bugando/kcmc kila kanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…