Monica Mgeni
Member
- Oct 7, 2021
- 82
- 134
Hivi Karibuni tumeona Mhe. Rais akifanya teuzi za Viongozi Wakuu katika Vyombo vya Ulinzi, ambao ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Mkuu wa Jeshi la Polisi lengo likiwa ni kuboresha utendaji kazi wa Vyombo husika kwa maslahi ya Taifa.
Katika teuzi hizi mpya za Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa nimeona dhamira kuu ya Rais kwa kuwa aliowateua ni watu wenye sifa stahiki za uongozi na uwajibikaji, hivyo pasipo na shaka yoyote naona namna kero mbalimbali za wananchi zinazokwenda kutatuliwa kupitia wateule hao.
Katika kipindi kifupi cha uongozi wake, tumeona Rais SAMIA amejipambanua kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo katika Nyanja zote ikiwemo kuboresha miundombinu na kuwapatia wananchi huduma mbalimbali za kijamii.
Wito wangu kwa wananchi katika mikoa mbalimbali nchini, tuwaunge mkono na kushirikiana vyema na wateule hao kwa kuwa wao wanamuwakilisha Rais.
Tudumishe Amani ya Nchi yetu na kwa pamoja tujenge Umoja wa kitaifa. Aidha, tujitokeze kuhesabbiwa Agosti 23, 2022 ili tuisaidie Serikali kupata takwimu sahihi zitakazoiwezesha kutuhudumia