Rais Samia Suluhu Hassan: Hii ni Serikali ya Awamu ya 6

Ni vema tukihesabu Marais. Hivyo Samia ni Rais wa sita wa nchi hii. Hii ya kuhesabu awamu ni kujichanganya bure.

Kama tukitaka kuhesabu awamu basi tuanze na tafsiri rasmi ya awamu. Awamu ni nini?
Rais sita lakini anahudumu katika serikali ya awamu ya tano...Rais akifariki na serikali inafutika?
 
Wasomi , wanazuoni,wanasheria naomba tujadili kama ni sahihi kwa mujibu wa katiba yetu kumuita Rais Samia kama rais wa awamu ya sita badala ya kuitwa rais wa pili wa awamu ya tano?. .1..Katika Uchaguzi mkuu uliofanyika 2020 Vyama vilinadi ilani zao ili kuchaguliwa kuongoza nchi na ilani ya CCM ndiyo inayotekelezwa na ni makubaliano baina ya wananchi na serikali ya chama tawala na hiyo ilani ndiyo inatekelezwa na mama Samia.
2.je katiba inapotamka makamu wa rais kushika wadhifa wa urais inapotokea rais aliyechaguliwa kufariki haikuwa na lengo la kuhakikisha kila awamu inakamilka na ahadi za wananchi zinatekelezwa?
3.kama serikali hii ni sawa kuiita serikali ya awamu ya sita je inatekeleza ilani ipi?na hayo wanayotekeleza kama ni mapya ridhaa hiyo inatoka wapi wakati hakuna uchaguzi uliofanyika?
Kinachonisikitisha ni kwamba, waalimu wanawafundisha wanafunzi wetu huko shule za msingi kwenye SoMo la urais

Wanafunzi hawapewi misingi Bora ya uraia, bali wanakaririshwa utopolo wa wanasiasa
 
Nchi inaweza kuendeshwa bila hata ilani.
Ilani ni mbwembwe tu za vyama, kwenye hiyo ilani si ndio kuna mambo ya maji, umeme na ajira? kiko wapi?
Inatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2020 - 2025, au na Chama kimebadikika?
 
Hata Zanzibar tangu mapinduzi ni miaka hamsini na Saba, lakini kuna Rais wa awamu ya name. Rais Abeid Karume,Abdu Jumbe,Ali Hassan Mwinyi,Idriss Abdul Wakil,Salmin Amour Juma,Ali Mohamed Shein na Hussein Ally Mwinyi
 
Wasomi, wanazuoni, wanasheria naomba tujadili kama ni sahihi kwa mujibu wa katiba yetu kumuita Rais Samia kama rais wa awamu ya sita badala ya kuitwa rais wa pili wa awamu ya tano?

1. Katika Uchaguzi mkuu uliofanyika 2020 Vyama vilinadi ilani zao ili kuchaguliwa kuongoza nchi na ilani ya CCM ndiyo inayotekelezwa na ni makubaliano baina ya wananchi na serikali ya chama tawala na hiyo ilani ndiyo inatekelezwa na mama Samia.

2. Je, katiba inapotamka makamu wa rais kushika wadhifa wa urais inapotokea rais aliyechaguliwa kufariki haikuwa na lengo la kuhakikisha kila awamu inakamilka na ahadi za wananchi zinatekelezwa?

3. Kama serikali hii ni sawa kuiita serikali ya awamu ya sita je inatekeleza ilani ipi? Na hayo wanayotekeleza kama ni mapya ridhaa hiyo inatoka wapi wakati hakuna uchaguzi uliofanyika?
Hii ni awamu ya 5 iliyopata ajali.
 
Hoja zako zimeshiba!. Zimeshiba kiasi cha kuweza kufungua shauri mahakama kuu ili kupata tafsiri ya kisheria. Najiuliza tu, kile chama cha wanasheria hakilioni hili?.. Rais msomi wa wanasheria upo? 🤔
 
Ni vema tukihesabu Marais. Hivyo Samia ni Rais wa sita wa nchi hii. Hii ya kuhesabu awamu ni kujichanganya bure.

Kama tukitaka kuhesabu awamu basi tuanze na tafsiri rasmi ya awamu. Awamu ni nini?
Hii ni awamu ya tano ndiyo maana hatujafanya uchaguzi, Awamu hiyo ya sita ingekuja akiingia kwenye mchuano wa uchaguzi. Anamalizia awamu ya tano
 
Watu wanajibu sijui kwa akili gani,nilicho na uhakika ni awamu ya tano kipinsi cha pili rais wa sita.Kwa awamu ni awamu ya tano.Awamu haimaanishi lazima awe Fulani ila lazima iwe miaka kumi bila kujali nani anaongoza.
 
Mods naheshimu msimamo wenu na kazi yenu ya kuunganisha nyuzi zenye mfanano wa aina fulani. Lakini naomba kwa upole na unyenyekevu nkubwa msiunganishe huu uzi na nyingine. Nimeomba, asante sana!

Wana JF wa CCM na Upinzani na wasio na chama, Je ni kweli Rais Samia ni Rais wa awamu ya 6 ama 5?

Kumradhi:
Naomba nitangulie kusema kwamba kati ya Jambo kubwa linaloigharimu nchi yetu ni kukosekana wasomi 'very competent'; naweza kusema wasomi wetu wengi kwenye hili Taifa ni product ya 'Q & A' kwenye vitini vya hapa na pale. Taifa letu halina wasomi wenye 'natural thinking ability' badala yake tuna wasomi wengi wanao reason kwa kuambaambaa na upepo wa wakati ule. Again, kumradhi!

Nasema hivyo kwa sababu, hadi sasa hakuna msomi yeyote wa chuo chochote ama kutoka popote ambaye amewahi ku 'challenge' kisomi uwepo wa awamu ya 6 badala ya kuitwa awamu ya 5.

Awamu ya uongozi inakuwa na elements kuu tatu:
1. Uchaguzi wa urais na makamu wake
2. Uchaguzi wa wabunge kwenye majimbo pia na viti maalum
3. Uchaguzi wa Madiwani pia viti maalum.

Ilivyo ni kwamba, lazima Rais anayegombea awe na makamu wake. Logic ya kuwa na makamu ni kwamba, in case of anything unusual basi makamu wa Rais ndio anashika usukani na kuendelea. Kwa maneno mengine makamu wa Rais ni Rais.

Kuna nyakati Rais anakuwa na hali mbaya ya ki afya hivyo Makamu wake ndio anasimama kwenye nafasi yake hivyo ni Rais.

Kuna wakati mwingine Rais anakuwa yupo nje ya mipaka ya nchi yake hivyo anayesimama kwenye nafasi yake ni makamu wa Rais hivyo ni Rais.

Kipekee sana, kuna mifano mingi mno inayohalalisha kuwa makamu wa Rais ni Rais kwa maneno mengine kiasi kwamba hawezi kujitenga na awamu alioombea kura.


Kama hivyo, ni lini Rais Samia aliomba kura ya kuwa Rais wa nchi hii? Hajawahi, bali aliomba ya kuwa makamu wa Rais wa awamu ya 5.

Ni lini Rais Samia aliomba kura ya wabunge wake? Ameomba akiwa awamu ya 5.

Na Madiwani je? Pia akiwa awamu ya 5.

Kuna mambo mengi yanayoelezea kiwaziwazi kuwa Rais Samia ni Rais wa awamu ya 5 na sio ya 6.

Awamu ya urais ni package (Kuomba kura ukiwa na makamu wako + Kuunda Bunge Jipya + Kuteua Waziri Mkuu mpya + Kuteua speaker qa Bunge mpya) na kuendelea!

Ndio maana, nasisitiza tena ndio maana Magufuli alipochaguliwa awamu yake ya Kwanza aliunda Serikali yake kuanzia Bunge, Madiwani, na kwingine kote.

Alipochaguliwa awamu yake ya pili alifanya hivyo hivyo kama alivyofanya hapo awamu ya Kwanza, yaani as if anaanza kitu kipya tena kama vile hakuwepo.

Sasa, Rais Samia yeye ameunda Serikali yake? Ndio aliunda wakisaidiana na Rais Magufuli na ndio maana hata baada ya Magufuli kufariki aliendelea na serikali ile ile iliyopo maana ndio Serikali yake.

Kwa sasa kama Rais Samia akigombea mwaka 2025 - 2030 basi anakuwa rasmi ni Rais wa awamu ya 6 (sita).

Nawaasa wasomi wa Taifa hili wa kila kada, amkeni kwa ajili ya Taifa lenu!
 
Awamu zinahesabika kwa vichwa vya marais so as to document legacy correctly! Hata akikaa mwezi, AWAMU IMEISHA NA LEGACY YAKE TAYARI, HUWEZI KUIUNGANISHA NA YA RAIS MWINGINE.
 
Awamu ya tano..awamu ya sita itatimia 2025 pale le super chief commander Hangaya atakaposhinda uchaguzi na kutangazwa na Tume wa uchaguzi.
 
Kwani katiba inasemaje ndgu kuhusu awamu za serikali, isije ikawa unawatuhumu wasomi wetu bure Tu kwenye hili
 
Back
Top Bottom