Rais Samia Suluhu, ahsante kwa nilichokisia wakati wa uapisho wa viongozi

Mama piga kazi acha kutisha raia wako,raia huwa hawatishwi hata siku moja.ukimtisha raia wako huwezi kuongoza Hilo taifa.Raia ndiyo wamekupa hayo mamlaka hivyo hupaswi kuwatisha.Mwendazake aliwatisha na kuwaogepesha raia wake kilichompata hata kisahau katika maisha yake.

Mama tunakuombea Sana Allah akupe hekima ,busara,maarifa na fikra pevu katika kuongoza Taifa letu.kesi ya mbowe Haina msingi wowote ifutwe.
 
Hakuna kitu ni mwendelezo wa maneno maneno tu, mbona Sirro aka Zirro hajamtoa kwa hiyo kalamu yake hadi leo maana kila anachomuagiza hatekelezi, anaishia kulalama tu
 
Binafsi nimefarijika sana kumsikia Rais Samia akisema kwa kujiamini kabisa.
Kamwe asikubali kuyumbishwa na maneno ya walioshindwa kutimiza wajibu wao.
Nchi yetu inazidi ya watanzania milioni 60, tuna wataalamu kibao, wasomi wazuri na wazalendo wazuri, wakisumbua wewe tumbua tu.
tumbua sisi tupo na tuko tayari kufanya kazi hata kwa kujitolea ilimradi nchi yetu isonge mbele na wananchi wanufaike ktk utawala wako.
Mungu ambariki sana Rais
 
Leo nimesikia maneno mazuri kutoka kwako ambayo nilihitaji kutasikia kwa muda mrefu sana, nakushukuru sana sasa naona umeamua kazi kazi

Tafadhali Rais wangu usicheke na kima hapa tutavuna mabua, kwakweli kwakweli niseme wazi upole wako unawafanya watu wakuone dhaifu na kukudharau.

Lakini kimsingi wewe ndiye Amiri Jeshi Mkuu lazima tukuheshimu hiyo ni lazima sio hiyari, hatutaki matabaka sisi ndani ya serikali yetu, kuna watu wanafikra za kijinga sana wakiamini wao hawawezi kuongozwa na mwanamke hawa watu ndio wa kudili nao sasa wakiongozwa na Askofu Kibwetere anakudharau sana.

Kwakweli nilikua naumia sana kuona Rais anadharauliwa hadi na watu kama Polepole ambao hata uwepo wao bungeni ni kwa msaada wa Rais.

Mheshimiwa Rais wakati wa ustaarabu sasa umepita maana sisi unaotuongoza hatujastaarabika

Fukuza wale wote wanaokukwamisha kwa dharau zao na sio kuwafukuza tu fukuza peleka na takukuru na uhamiaji wawachunguze kidogo

Hatuwezi kuwa na Taifa lisilo na nidhamu haiwezekani, mtu kama Gwajima anamtuhumu Rais kuhongwa ili alete chanjo na Rais unakaa kimya?

Naomba Mungu anipe japo moyo kama wa Samia maana Laiti kama mimi ndiye ningekua Rais sijui mpaka sasa Gwajima angekua na hali gani

Sipendi dharau,

Samia ndiye Rais basi anapaswa kuheshimika kama Rais na ieleweke hivyo

Mheshimiwa Rais sisi tuko nyuma yako, kuwa mkali mama, wote unaoona hawaeleweki fukuzia mbali watutolee ujinga wao sisi

Kifuatachi sasa nikudili na nidhamu za watumishi nao wameshaanza dharau, kama hadi mkurugenzi anaiba mabati serikali gani hii sasa

Rais anaenda sherehe meimosi mwanza huku nyuma watu wanajilipa posho za kazi maalumu zisizo na mbele wala nyuma,

Rais Samia narudia tena sasa iwe mkali uwe mkali uwe mkali mara dufu
Rais hawezi fanikiwa kwa kumtakia mema kila siku. Anatakiwa ajitambue badala ya kuwategemea hawa akina Kiwete ambao kila mtu analaani tabia yao. Hao walifanikiwa kuwa viongozi kama laana kwa taifa.
 
Back
Top Bottom