Rais Samia Suluhu, ahsante kwa nilichokisia wakati wa uapisho wa viongozi

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Leo nimesikia maneno mazuri kutoka kwako ambayo nilihitaji kutasikia kwa muda mrefu sana, nakushukuru sana sasa naona umeamua kazi kazi

Tafadhali Rais wangu usicheke na kima hapa tutavuna mabua, kwakweli kwakweli niseme wazi upole wako unawafanya watu wakuone dhaifu na kukudharau.

Lakini kimsingi wewe ndiye Amiri Jeshi Mkuu lazima tukuheshimu hiyo ni lazima sio hiyari, hatutaki matabaka sisi ndani ya serikali yetu, kuna watu wanafikra za kijinga sana wakiamini wao hawawezi kuongozwa na mwanamke hawa watu ndio wa kudili nao sasa wakiongozwa na Askofu Kibwetere anakudharau sana.

Kwakweli nilikua naumia sana kuona Rais anadharauliwa hadi na watu kama Polepole ambao hata uwepo wao bungeni ni kwa msaada wa Rais.

Mheshimiwa Rais wakati wa ustaarabu sasa umepita maana sisi unaotuongoza hatujastaarabika

Fukuza wale wote wanaokukwamisha kwa dharau zao na sio kuwafukuza tu fukuza peleka na takukuru na uhamiaji wawachunguze kidogo

Hatuwezi kuwa na Taifa lisilo na nidhamu haiwezekani, mtu kama Gwajima anamtuhumu Rais kuhongwa ili alete chanjo na Rais unakaa kimya?

Naomba Mungu anipe japo moyo kama wa Samia maana Laiti kama mimi ndiye ningekua Rais sijui mpaka sasa Gwajima angekua na hali gani

Sipendi dharau,

Samia ndiye Rais basi anapaswa kuheshimika kama Rais na ieleweke hivyo

Mheshimiwa Rais sisi tuko nyuma yako, kuwa mkali mama, wote unaoona hawaeleweki fukuzia mbali watutolee ujinga wao sisi

Kifuatachi sasa nikudili na nidhamu za watumishi nao wameshaanza dharau, kama hadi mkurugenzi anaiba mabati serikali gani hii sasa

Rais anaenda sherehe meimosi mwanza huku nyuma watu wanajilipa posho za kazi maalumu zisizo na mbele wala nyuma,

Rais Samia narudia tena sasa iwe mkali uwe mkali uwe mkali mara dufu
 
leo kweli amewakumbusha mawaziri
Leo nimesikia maneno mazuri kutoka kwako ambayo nilihitaji kutasikia kwa muda mrefu sana, nakushukuru sana sasa naona umeamua kazi kazi

Tafadhali Rais wangu usicheke na Kima hapa tutavuna mabua, kwakweli kwakweli niseme wazi upole wako unawafanya watu wakuone dhaifu na kukudharau...
Kinachonishangaza ni ushujaa wenu kumsikiliza. Binafsi nilishakata tamaa kusikia anasema nini. Ninachofahamu kila kitu anauliza aambiwe nini kifanyike. Huyo anayeulizwa ndo wale walioangusha nchi hii hadi wajinga wakawa maarufu. yaani JK!
 
Leo nimesikia maneno mazuri kutoka kwako ambayo nilihitaji kutasikia kwa muda mrefu sana, nakushukuru sana sasa naona umeamua kazi kazi

Tafadhali Rais wangu usicheke na kima hapa tutavuna mabua, kwakweli kwakweli niseme wazi upole wako unawafanya watu wakuone dhaifu na kukudharau...
Kurejea matapishi ni hatari mkuu.

Usije kurejea dem mkiachana.. Atakufa mtu. Makamba sasa laziima awaonyeshe.
Ona Mwigulu anachowatenda?
 
Wa latin wanasema Castigat Redondo Morales yaani Laughing correct morals..there were so much laughing on Madam, so I think her excellency have decided to correct morals
 
Uzi wote huu unazungukazunguka tu,wewe nenda tu kwenye pendekezo lako kuwa awafukuze Gwajiboy na Polepole hapo ndo mtajua kwanini JK aliimbiwa mbele yake tunaimani na Lowassa.
 
Yakiambatana na vitendo ni sawa lakini maneno tu doh! Halaf ona wakat anaanza ilikua hamna kitu inavyuja..sasa tetesi za mawaziri zilishavuja kitambo na watz kibao kutabir makamba atakua wazir japo mwigulu pia alitajwa .lakini nimesikia mwigulu anaitwa hasan na ni mtoto wa...hawez kutumbuliwa utawala huu..
 
Mkuu we upo Kama mimi nimefurahia Sana kauli yake . Watu hawafanyikazi sikuhizi maofisini mpaka nawaulizaga mbona jamani watu hamfanyikazi au kisa mnamuona raisi dhaifu?

Maana Kama wengine madaraja wamepandishwa mpaka malimbikizo wamelipwa lakini bado unamkuta mtu hatakifanya kazi anakalia tu majungu kwa raisi. Kanikoshasana leo kwa kauli yake ya kimamlaka.

Nami nasema nipo nae na ntampigania mpaka mwisho.
 
Back
Top Bottom