HAKI KWA WOTE
JF-Expert Member
- Nov 30, 2022
- 607
- 553
Habari Rais Samia,
Nianze kwa kukupongeza kwa uamuzi wako wa kuwalioa waliofukuzwa kazi kwa kughushi vyeti, ila napenda utambue kuna wengine hawaghushi vyeti bali waliachichwa kazi kwa sababu tofauti kabisa na hiyo.
Mimi nitazungumzia wale walioachishwa kazi kwakuwa tu walibadili kada zao baada ya kujiendeleza kisha wakafanya mchakato huo na kukubaliwa kubadili kada zao hasa baada ya kujiendeleza ila wanavyeti halali na wamesomea nafasi au ujuzi huo.
Mfano, ni walimu wa Voda Faster ambao kiuhalisia wao walimaliza kidato cha 6 na kupewa mafunzo ya muda mfupi ya ualimu kwa makubaliano ya kujiendeleza katika fani ya ualimu lakini kutoka na sababu na changamoto au nafasi mbalimbali zilizokuwepo walijiendeleza kwenye kada nyingine na kufanikiwa kubadilisha kada zao.
Ni wazi walimu hawa wengi wao hawakuwa na mapenzi na huo ualimu wa Voda Faster bali walitafuta njia ya kuingilia serikalini na ndicho kilichotokea.
Sasa kumekuwa na sintofahamu juu ya watumishi kama hawa nao kulipwa stahiki zao ambapo wanaambiwa kuwa hawawezi kulipwa kwani wao siyo wahanga wa vyeti feki.
Nikuombe kwa busara zako uwaangalie hawa watumishi pia kwa kuweka utaratibu wa wao pia kulipwa haki zao au kurejeshwa kazini kwenye kada walizojiendeleza na kubadilishwa.
Ni matumaini yangu kuwa utalifanyia kazi.
Nakala:
- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
- Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu.