GE2025 Rais Samia: Serikali itaajiri wahudumu wa afya 5000 ndani ya siku 100

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Dkt. Samia Suluhu Hassan mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema Serikali itaajiri wahudumu wa afya 5000 ndani ya siku 100 ili kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.

Dkt. Samia amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, unaofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.

Your browser is not able to display this video.
 
Kwanini wasifanye sasa hivi kuachia miili ya marehemu?
 
Rais Samia Suluhu ameeleza vyema kabisa kwamba, wakipata ridhaa ya Watanzania katika kuongoza tena awamu nyingine, basi watatoa ajira mpya zaidi ya 10,000 kwa watumishi wa afya na walimu.
 
Rushwa to rushwa
Kazi ni kipimo cha utu
 
Mgombea Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Samia Suluh Hassan, ameahidi kuwa atatekeleza mambo mbalimbali ambayo ameyaahidi katika kampeni zake mkoani Songwe ikiwemo sekta ya Afya,elimu na miundombinu ya barabara.

Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi hiyo wakati akizungunza na wakazi wa Mlowo Jimbo la Mbozi mkoani Songwe akiwa njiani kuelekea mkoani Mbeya.

🗣"Lakini niwaambie Songwe ninayoijua ya 2020 sio Songwe ya leo mambo ni makubwa kwa hiyo niwaahidi mtakapotupa ridhaa ya kurudi kuendesha Serikali yale niliyoyataja jana yote tunakwenda kuyatelekeza"

🗣"na kubwa zaidi nilisema wakati nafungua kampeni kwamba tunakwenda kuanza utekelezaji wa masuala ya bima ya Afya, tumejenga vituo vingi vya Afya,Zahanati,Hospitali za Wilaya na Rufaa na zote tumezijaza vifaa,watumishi niliahidi kuajiri zaidi, watumishi nadhani elfu tano zaidi wa Afya nitaajiri ndani ya siku zangu 100" Amesema Dkt Samia Suluhu Hassan.
Your browser is not able to display this video.
 
Rais Samia Suluhu ameeleza vyema kabisa kwamba, wakipata ridhaa ya Watanzania katika kuongoza tena awamu nyingine, basi watatoa ajira mpya zaidi ya 10,000 kwa watumishi wa afya na walimu.
Jinga kbs hilo, kwani nani rais kwa sasa?!?!
 
Rais Samia Suluhu ameeleza vyema kabisa kwamba, wakipata ridhaa ya Watanzania katika kuongoza tena awamu nyingine, basi watatoa ajira mpya zaidi ya 10,000 kwa watumishi wa afya na walimu.
Unatumia kichwa au kiungo kipi kufikiri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…