Rais Samia, pamoja na sifa unazomwangia Jumaa Aweso, huyu siyo mwaminifu

Una shida gani dada angu?
19059991_1386835601392897_3757162351071440092_n.jpg
 
Huyo jamaa alitoka chuo tu kazi yake ya kwanza ikawa Ni ubunge then unaibu Waziri then uwaziri kamili hajawahi kuajiriwa hata sehemu 1.

Je hilo ndilo linamfanya umwite mwizi? Umewataja mawaziri wawili hapo; Aweso na Kitilla mkumbo, weka vielelezo kuthibitisha wizi wao.
 
Hii wizara inapewa hela nyingi ila utendaji na utekelezaji ni sifuri na Kuna upigaji plus ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi huku hela za miradi zikiwa zinachezewa kwa kucheleweshwa kwa kuanzia kwa Waziri na katibu wote hao wanajuana.
Hii wizara inahitaji reformation bila hivo shida za maji kuisha itakuwa ngumu mno
 
Hii Wizara ina matatizo sana.
Moja ya sehemu ambazo zina uwizi Mkubwa ni kwenye mabonde maana kuna pesa za wahisani huwa zinakuja ili kufanya miradi kadha wa kadha kwa upande wa Wami Ruvu kuna mradi wa (WSDP II ) Kuna Mambo ya ajabu yamefanyika pesa zimeliwa kama karanga.

Nashauri serikali kupitia Ofisi ya CAG ifanye ukaguzi wa miradi hii.

Na hizi Ofisi za Mabonde ziangaliwe upya Majukumu yake maana kazi kubwa ni kutunza vyanzo vya Maji lakini ni sehemu ya kula pesa ivyo vyanzo vya Maji kweli vinatunzwa?, ndio maana Maafisa wa Maji ni matajiri sana, hapa serikali angalieni katika hilo na chunguzeni katika hilo.

na kingine hizi Kodi za visima bado zinaendelea, bado umuhimu wake hauonekani kwamba Kijiji hakina Maji wananchi wananchingishana wanachimba kisima hapo Bonde halijatoa msaada wowote lakini Maji yakishaanza kutumika tu wanaanza kuwatoza kodi, ukiuliza return ya hiyo Kodi ni Nini hamna jibu la maana maana kama kisima kitakua na matengenezo ni juu ya wanakijiji sasa kazi ya Bonde ni nin?

Naishauri serikali wayatazame upya haya mabonde kwa jicho la 3 maana ni sehemu za vichaka za watu kula pesa.

Nayajua mengi sana maana nimefanya kazi karibu na mabonde yote Tanzania.
 
Au atakua yule mwandishi alieporwa mke mkuu wa ulaya aliyeona mwandishi mzugaji bora awe na waziri
Yule mwandishi mbona ana cheo kikubwa huko Zanzibar.
Hyo wizara ina upigaji mwingi na Waziri hawachukulii hao ma manager wa mikoa maana Wana lion share
 
Hapana kwa kweli mh aweso sio mtu wa hivyo acheni kuchafua watu
 
Nakubaliana na mleta mada. Huyu kijana anachofanya ni kumghilibu huyu maza kwa vijimatangazo visivyo na faida then maza anaona mchapa kazi. Lakini kiukweli ni MPIGAJI wa hatari. Hafai hata kuwa diwani
 
Hilo kupitisha pesa huko bonde ruvu linasemwa sanaaa sijui wale tiss wapo humu kina ........wayafikishe au ndio zama zao sasa hawagusiki?
 
Weka ushahidi wa madai yako, vinginevyo hoja yako itakuwa ni chuki na wivu vinakusumbua.

Fafanua ni namna gani wanaiba hizo pesa, ni kiasi gani kimeibiwa na ni miradi ipi imeathirika kutokana na wizi au ubadhirivu huo.

Kumchafua mtu pasipokuwa na ushahidi ni kujichumia dhambi ya kumshuhudia mtu mambo ya uongo.

Kama kweli waziri Awesso ni mwizi, weka ushahidi hadharani.
Watu wajinga wote ukiwaambia matatizo yao hukimbilia kuomba ushahidi. Ukiambiwa fulani mwizi, mpuuzi, bwege, n.k. chunguza mwenyewe kwa manufaa yako. Sasa tena unamuuliza aliyekupa taarifa za ujinga wa nduguyo? Kama Aweso ndo anauliza sawa, lakini wewe Samia unatonywa juu ya upuuzi wa mteule wako halafu unaomba tena ushahidi!! Nani akupe? Umemwajili kwa kazi hiyo? Huna uliowaajili kukutafutia ushahidi? FOOOOOL!
 
Aweso ana zurura mikoani kila leo wakati hana habari sasa hivi kuna mgao mbaya sana wa maji jijini Dar es Salam
 
Ulikua wapi siku zote? Tena kipindi cha JPM? Sababu kapata kongole kwa Rais? Tutajuaje kama huna chuki nae? Weka ushahidi wa tuhuma hizi.

Simjui kiundani, lakini nafikri ni Waziri kijana aliyeweza kupunguza kero za maji kwa wengi kwa kipindi kifupi.

Wizara ya maji kwa nchi hii ni tatizo kubwa tangu Uhuru, kijana anapambana apewe support.
 
Watu wajinga wote ukiwaambia matatizo yao hukimbilia kuomba ushahidi. Ukiambiwa fulani mwizi, mpuuzi, bwege, n.k. chunguza mwenyewe kwa manufaa yako. Sasa tena unamuuliza aliyekupa taarifa za ujinga wa nduguyo? Kama Aweso ndo anauliza sawa, lakini wewe Samia unatonywa juu ya upuuzi wa mteule wako halafu unaomba tena ushahidi!! Nani akupe? Umemwajili kwa kazi hiyo? Huna uliowaajili kukutafutia ushahidi? FOOOOOL!
Kwahiyo kama ni majungu unataka Serikali ipoteze muda na raslimali kuchunguza majungu?

Tumia akili za kuzaliwa wewe. Kuna wamejaa fitina, chuki, wivu na uzandiki. Watu hawa wapo tayari kutoa habari au taarifa za uongo ili tu kuwachafua wengine.

Kwa kulitambua hilo ndiyo maana nikasema, kama mleta mada anao ushahidi wa madai yake basi ayaweke hadharani. Lakini kama hana ushahidi basi akae kimya.

Huu ni utaratibu unaotumika kote duniani. Hata ukiwa USA wanakojinasibu kuwa vinara wa freedom of speech, bado ukimtuhumu mtu watakwambia tupe ushahidi wa tuhuma zako.

Mfano mimi nikija nyumbani kwako na kumwambia Mume wako kuwa wewe unagegedwa nje ya ndoa kitu cha kwanza ataniambia nimpe ushahidi wa hizo tuhuma.

Tuache tabia za kuwachafua watu, kuna gharama zake. Mfano ni Musiba, alimchafua sana Membe matokeo yake ni kumlipa mabilioni ya pesa.
 
Tunazidiana ujinga.
 
Maji ni shida kubwa nchi hii kwa takribani miaka 60 ya Uhuru bado shida ya maji iko pale pale

Ndio maana werevu huwakumbuka Wakoloni
 
Back
Top Bottom