Rais Samia, pamoja na sifa unazomwangia Jumaa Aweso, huyu siyo mwaminifu

robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
740
1,214
Waziri Aweso kila siku yuko kwenye kamera na waandishi na yaonekana rais anaamini ni mtendaji mzuri. Kwa tabia za Waziri huyu na watendaji wa wizara hii, tatizo la maji halitakwisha nchi hii. Ifikie hatua miradi yote inayotangazwa, kama haifanyi inavyotakiwa, wahusika wote wafukuzwe kazi.

Aweso alianzia wizara ya maji kama naibu Waziri. Mkumbo akiwa katibu mkuu wa wizara. Kipindi chote walimtumia afisa bonde la Wami-Ruvu makao makuu yakiwa pale Morogoro kama njia ya kupitishia pesa za serikali na kuziiba. Miradi mingi ilipitia huko pamoja na ujenzi kwa bonde hili ambalo ni mashuhuri.

Pesa yote iliwarudia watu hawa pamoja na waziri wao. Sasa Aweso ni waziri kamili. Amejifanya kukosana na afisa bonde la Wami-Ruvu na kumuondoa au kumuhamisha. Yuko wizarani, benchi tu! Sasa aweso ana marafiki wapya na sasa nguvu kubwa iko kwa afisa bonde la Rufiji makao makuu yakiwa Iringa.

Pesa imepelekwa mara nyingi na kurudishwa kwa maafisa wa wizarani bila manufaa kwa wakazi wa bonde hili.
 
Maji tena? Hii ni wizara mbovu, mbovu kabisa! Imejaa wezi tangu waziri hadi fundi bomba mtaani.

Ninachoelewa, hawa mawaziri wanaoitwa vijana wote ni wwarafi wa pesa. Machachari yote unayosikia kwenye TV ni matangazo. Nahisi elimu yetu ni tatizo sana. Watu hadi wanapata digrii wanakuwa bado akili na ufahamu ni mdogo.
 
Weka ushahidi wa madai yako, vinginevyo hoja yako itakuwa ni chuki na wivu vinakusumbua.

Fafanua ni namna gani wanaiba hizo pesa, ni kiasi gani kimeibiwa na ni miradi ipi imeathirika kutokana na wizi au ubadhirivu huo.

Kumchafua mtu pasipokuwa na ushahidi ni kujichumia dhambi ya kumshuhudia mtu mambo ya uongo.

Kama kweli waziri Awesso ni mwizi, weka ushahidi hadharani.
 
Maji tena? Hii ni wizara mbovu, mbovu kabisa! Imejaa wezi tangu waziri hadi fundi bomba mtaani.

Ninachoelewa, hawa mawaziri wanaoitwa vijana wote ni wwarafi wa pesa. Machachari yote unayosikia kwenye TV ni matangazo. Nahisi elimu yetu ni tatizo sana. Watu hadi wanapata digrii wanakuwa bado akili na ufahamu ni mdogo.
Huyo jamaa alitoka chuo tu kazi yake ya kwanza ikawa Ni ubunge then unaibu Waziri then uwaziri kamili hajawahi kuajiriwa hata sehemu 1.
 
Inajulikana miradi ya maji inaupigaji usiokuwa wa kawaida. Lakini mleta mada maelezo yako hayana tofauti na yale yanayoendelea mahakamani, story nyingi vielelezo sifuri.
 
Inajulikana miradi ya maji inaupigaji usiokuwa wa kawaida. Lakini mleta mada maelezo yako hayana tofauti na yale yanayoendelea mahakamani, story nyingi vielelezo sifuri.

Au atakua yule mwandishi alieporwa mke mkuu wa ulaya aliyeona mwandishi mzugaji bora awe na waziri
 
Nadhani huyo Aweso, na huyo aliyekuwa mkurugenzi wa Wami-Ruvu hapo Morogoro wanapaswa kuchunguzwa, maana jamaa ana ukwasi hatari sana! Dkt Magufuli kuna watu walimdhihaki sana tena sana, yeye anaimba uzalendo watu wana mg'onga. Nadhani kwa Mama ajitahidi kuwajengea uzalendo watumishi ili waone hata kama una hela kama Billgate yet utakufa na kuziacha
 
Back
Top Bottom