Rais Samia, nimeukubali msimamo wako. Hongera sana

..@Pascal Mayalla amekushauri usichanganye hoja za maendeleo, uwekezaji, teknolojia, na masuala au mashambulizi ya kisiasa, au dhidi ya wanasiasa na vyama.

..Ni ushauri mzuri sana na kama ungeuzingatia ungesaidia kufikisha elimu na maarifa kwa wasomaji wengi.
Sawa. lakini naomba utambue kuwa sio wote ambao watasoma mada yangu hii kuhusu Helium gas wanaweza wakaelewa nini kimemaanishwa sabau wanakosa ile imagination ya matumizi ya hiyo Helium gas.

Kila mmoja anaye soma hii mada ana pick ile theme anayo penda kuijengea hoja, mara nyingi ni part ya siasa au udaku wa Mh. Jobu Ndugai.

Ni imani yangu kuwa mhusika mkuu au wasaidizi wake wakiisoma hii mada wanaweza wakanielewa na kuifanyia kazi. Hao ndiyo muhimu kwangu na sio idadi ya wasomaji ambao kwa vyoyvote vile hawatanielewa.

Kwa wale wanao pendelea ku-comment hoja za malumbano ya kisiasa watajibiwa accordingly. Wengi wao ndiyo wanachoweza.

Mambo ya kitaalam kama ya Helium gas na mengineyo kuhusu technology ni challenge kubwa sana kwa watanzania kukuelewa kwa sababu ya ukosefu wa watu wenye maarifa mapana. Tungekuwa na watu wa aina hiyo watanzania hivi sasa tungekuwa tunazungumzia mambo mengine.

Waandishi wa habari wengi watanzania, ukimwondoa Mayalla pengine, mada zao nyingi ni za kuhusu siasa na itikadi za kivyama au udaku wa kanga na vijiweni.

Kwenye mambo ya tranformation na utilization ya rasilimali zetu za asili kuwa manufacturing products bado ni mbinde kweli kweli. Hii yote ina sababishwa na ukosefu wa elimu pana waliyo pata kutoka kwa walimu wao.

Kama mwalimu hakielewi kile anacho mfundisha mwanafunzi wake, unategemea huyo mwanafunzi naye ataelewa alicho fundishwa?

Sababu nyingine ni resources. Serikali yetu bado haijajua jinsi ya kutenga pesa kwa ajili ya resources ambazo zitawafanya vijana wa participate entirely kwenye masomo ya sayansi ya vitendo ili wajifunze mbinu mbali mbali za kuweza kutambua technologies zilizopo dunuani ili waweze kuzitumua kwenye kufanya mabadiliko ya rasilimali zetu kuwa products.

Nimesha pendekeza mara nyingi sana kuwa nchi yetu tunatakiwa tuwe na wataalam wa aina tofauti wenye uwezo wa kitaalam katika kuchakata rasilimali zetu.

Nitakuja tena kutoa mpangilio wa wa hizo professions na kutoa mapendekezo kwa serikali mambo ya kufanya ili vijana wapate picha kamili ya mambo ya kufanya.
 
Back
Top Bottom