Rais Samia naomba kushauri hivi kuhusu Fedha za Boost kwenye Elimu kabla ya kuanza utekelezaji

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
11,156
34,346
Sote ni mashahidi wa Juhudi Kubwa unazoendelea kuzifanya kuboresha Elimu yetu ikiwemo suala la kuboresha miundombinu ya Shule, Maabara na vitendea kazi.

Hivi karibu Serikali imetoa Fedha kwaajili ya Ujenzi wa Madarasa, Maabara za shule pamoja na madawati ili watoto wetu wawe na mazingira rafiki ya Kujisomea wakiwa shuleni.

Kiasi cha Bilioni 150 zitasambazwa kwaajili ya Ujenzi wa miundombinu hiyo kupitia BOOST program.

Hatujui Fedha hizo tumekopa au ni Fedha za makusanyo yetu lakini jambo muhimu ni Fedha zetu Watanzania, hata kama ni kulipa tutalipa wenyewe Watanzania.

Ushauri wangu, kwakuwa Fedha hizi ni nyingi na zinakwenda Shuleni. Ni muda Sasa Serikali iweze kuajiri hata Mafundi Sanifu Ujenzi (Civil Technicians) ili kusimamia Ujenzi huo ili kuja kupata value for money ya Miradi yetu.

Najua gharama za kuajiri zinaweza kuwa nyingi lakini tunaweza kuajiri hata kwa Mkataba mfupi wa miezi 3 au kulingana na kazi. Ujenzi ukikamilika na Ajira ya huyo Technician inakoma.

Sio busara unapeleka Fedha za Ujenzi wa Shule kiasi cha shilingi Bilioni 150 alafu anaekwenda kusimamia Ujenzi huo ni Mwalimu wa Chemistry/History au English.

Nadhani Fedha za Uviko -19 zilizoenda Shuleni na Afya huko Mwaka Jana zitakuwa zimetupa funzo. Unakuta Daktari anapewa Jengo la Wodi la akina Mama anasimamia Wakati hana taaluma ya Ujenzi.

Mimi naamini kama inatengwa shilingi milioni 23 kwaajili ya Ujenzi wa maybe Chumba kimoja Cha Darasa inatushinda nini kutenga walau 2,175,000/miezi 3 kugharamia huyo mtaalamu kuweza kusimamia huo Ujenzi kwa miezi mitatu (3)?

Tanzania itajengwa na Watanzania 💪.
 
Back
Top Bottom