Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Runzewe mkoa wa Geita, leo tarehe 16 Oktoba, 2022
Kwanza nawashukuru, nimeingia Geita jana asubuhi sana, tumefungua hospitali ya kanda pale chato, lakini tukafungua kiwanda cha kuchenjua dhahabu itakayouzwa duniani kote, pia kituo cha umeme.
Langu mimi ni kuwahakikishia, mimi pamoja na wasaidizi wangu wakiwemo mawaziri, wabunge tupo kuitumikia Tanzania. Tupo kumtumikia mtanzani, kuleta maendeleo na kujenga Tanzania yetu.
Ombi langu kwenu, bakini na amani. Tunzeni amani na utulivu kwenye maeneo yetu, twendeni tukachape kazi, kila mtu kwa kazi anayoifanya, kila mmoja achangie maendeleo ya nchi yetu.
Sisi ni wakusanyaji wa fedha ili tulete maendeleo kwenu, hatukusanyi tusibebe sisi, hapana. ndo pesa mnazosikia mama amemwaga, mama amemwaga, ni kwa sababu tumekusanya kutoka kwenu. Tuchape kazi ili tulete maendeleo.
Nawashukuru kwa zawadi zote mlizonimiminia, ili vijana wangu waweze kufanya kazi saa 24, na ili serikali iweze kukusanya mapato ya kutosha, naleta taa za barabarani.
Mmenipa kijana mzuri sana (Waziri Wa madini Doto Biteko) aliyenyanyua sekta ya madini kutoka kuchangia asilimia 4 ya pato la taifa, sasa inachangia karibia asilimia 8. Ndo maana mnaona nawagusa wote nawabadilisha, lakini Biteko yupo hapohapo. Kwa sababu anafanya kazi nzuri sana, anaichangia Tanzania vizuri sana, mtihani wake ni hadi 2025, asipofikia asilimia 10 (ya mapato) atakuwa amewaangusha wananchi wa Bukombe. Akifikisha asilimia 10, Biteko oyee.