Waziri Biteko: Hakuna Mradi Utakaosimama Chini ya Rais Samia

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Doto Biteko, amewahakikishia Wananchi wa Mkoa Geita kuwa, miradi yote mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano, inaendelea kutekelezwa na hakuna mradi utakaosimama.

Biteko ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, ameyasema hayo kwenye wa mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho, na kuwakutanisha wabunge wote wa mkoa huo, na ulilenga kuelezea utekelezaji wa ilani ya CCM.

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kupitia kauli mbiu ya kazi iendelee, amehakikisha miradi yote mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano, inaenndelea kutekelezwa na hakuna mradi uliosimama wala mradi utakaosimama,” amesema Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini na kuongeza;

“Nawaomba wananchi wote na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi tuendelee kumuunga mkono Rais na Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anayoifanya ya kumwaga fedha za maendeleo kote nchini, na ana maono makubwa ya kufikisha nchi yetu mahala pazuri.”

Chanzo: Mwananchi
 
Na sie tusio na vyama tunacomment wapi?
:mad::mad::mad::mad::mad:🥸🥸🥸🥸🥸😶‍🌫️😶‍🌫️😶‍🌫️😶‍🌫️😶‍🌫️
 
Mpwa wake Magufuli huyo, ila kazi anaiweza tumpe maua yake. Hivi unadhani angeongea Jambo la kumkosoa Rais na mwenyekiti wa chama?
 
Ebu kamilisheni jengo la uwanja wa ndege Mwanza,tumia u naibu Waziri Mkuu,kushughulikia hili.
 
Back
Top Bottom