Rais Samia na mafanikio ya UNGA

Ngaliwe

Senior Member
Dec 30, 2015
161
364
Ilisema huko na zamani na wa wahenga na wahenguzi kwamba, “It’s not how you are, but what people thinks how you are that counts,” kwa tafsiri isiyo rasmi, hoja siyo jinsi ulivyo isipokuwa jinsi watu wanavyofikiri ulivyo ndiyo watakavyokuchukulia.

Kanuni hii inahusika na maisha yetu moja kwa moja kama mtu mmoja mmoja, familia na hata taifa. Kwamba maisha ni watu ni ukweli ambao wengi wetu tunaukubali, ukichukulia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja au familia, anayeshirikiana na wenzake katika hali zote, wanamjua na wanafahamiana, hivyo siku akihitaji washikaji zake wamashike mkono kwenye suala lolote iwe tatizo la ugonjwa au msiba, au jambo la furaha kama sherehe za harusi, amba ubatizo, kipaimara na mengine, au hata anataka mkopo wa ada na kujikwamua kwa changamoto yoyote ile, rafiki zake watakuwepo kushikamana naye, wanaweza wasiwe wote lakini maadam anao wa kutosha, wapo watakaojitokeza katika hali zote, ndiyo maana wahenga wakasisitiza, “Make friends before you need them,” kwamba tengeneza marafiki sasa ili hata ukipata shida uwe tayari na watu wa kukusaidia.

Ndivyo ilivyo katika diplomasia ya kimataifa, Rais akijuana na wakubwa wa dunia, wakawa wanapata muda wa kuzugumza na kujadiliana mambo mbali mbali ana kwa ana, inajenga ‘rapport’ (tamka ra paw) maelewano mazuri kati ya taifa na taifa, taifa na taasisi zozote muhimu ambazo kwa kweli zinahitajiana sana.

Rais Samia Suluhu Hassana, akiwa New York tayari amekutana na Rais wa Benki ya dunia, Mkuu wa World Trade Organization – WTO na UNHCR na wengine, malengo ya msingi katika mikutano ya viognozi kama hii ni kujenga kwanza maelewano na uhusiano na taasisi kubwa kubwa duniani zenye maamuzi ambayo mara nyingi huathiri namna tunavyoendesha uchumi wetu, lakini zaidi sana ni kujenga na kuimraisha ushawishi wa Tanzania katika uga wa kimataifa.

Nchini ikiwa na ushawishi mkubwa kimataifa, ziko faida nyingi ambazo taifa linapata lakini hazionekani moja kwa moja kwamba zimetokana na ushawishi huo, ingawa kutoonekana kwake moja kwa moja hakuondoi ukweli kwamba zimetokana na ushawishi wa viongozi wa nchi husika.

Viongozi wanao onana na kuzungumza ana kwa ana hujenga hali ya kuaminiana na kushawishiana, ili siku ya siku ukiwa na jambo lako unataka lifanikiwe, ni rahisi kupigia simu viongozi kadhaa duniani ambao Rais anafahamiana nao kushawishi jambo lake na hapo nchi inafaidika kutokana na mahusiano yaliyojengwa kabla.

Ni kwa muktadha huo huo, ndiyo maana viongozi wa mataifa makubwa kama Marekani na China, wanatembea duniani kote kujenga ushawishi wa kimataifa kwa manufaa ya nchi zao hata kama wana uchumi mkubwa, lakini wanajua nguvu ya mahusiano kimataifa.

Rais Samia kwa kuwa Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania, anatumia nafasi hii kuiambia dunia kwamba ustaarabu wetu umefika kiwango cha juu kiasi kwamba mwanamke leo yuko katika ofisi ya juu kabisa nchini kuliko zote kitu ambacho mataifa mengine bado wanapambana kupata rais mwanamke. Hilo tu peke yake linaweza kujenga ushawishi mkubwa hasa kwa wanaharakati wa haki za jinsia duniani kuiweka Tanznaia katika mizani tofauti na hivyo kuongza ushawishi wetu kama taifa katika masuala mbali mbali duniani.

Diplomasia wakati wote ni suala la kujenga wasifu wako (au brand) ili wakati wote watu waaamini kwamba wewe ni bora na muungwana zaidi, na kwa kufanya hivyo unaweza kupata ukitakacho bila kutoa jasho la ziada. Hiki ndicho anachokifanya Rais Samia, anajenga mahusiano, anatengeneza marafiki, anachomeka kwenye akili za wakubwa wa dunia fikra mpya kuhusu Tanzania, na wakianza kutuona kama wenzao, bila shaka itaturahisishia mambo mengi kama Taifa. Kongole Rais Samia.
 
Naunga mkono juhudi za mama ktk utendaji wake isipokuwa ili kuboresha zaidi nashauri yafuatavyo:-

1. Ajitahidi kuepuka kupokea na kufanyia uamuzi wa kurudi tulikotoka kwa kila ushauri anaoupata toka kwa wasaidizi wake kwani baadhi yao ni wapigaji tu na hawako kwenye nafasi zao kwa manufaa ya watanzania bali kwa manufaa ya wapigaji.

2. Kama taifa chini ya uongozi wake ni vema tujikite kwenye ubunifu zaidi kwenye rasilimali zetu badala ya kuendeleea na mazoea katika kutenda na kufanya maamuzi. Mambo uliyoyaeleza hapo juu kuhusu mahusiano yamelenga zaidi kwenye kukopa kwenye taasisi za kimataifa badala ya kujenga mahusiano ya uwezeshwaji wa kufanya biashara kati ya taifa na taifa na watu wa taifa moja na jingine. Japo nimeona mama anaendelea kuimairisha mahusiano hayo ya watu kwa watu na taifa kwa taifa.

3. Tuwe viongozi wa kupenda kuboresha yaliyopita badala ya kuyariudisha yaliyopita kwa sababu ya mazoea. Tuwe wabunifu tusonge mbele tusirudi nyuma.

4. TUJIFIKIRISHE ZAIDI TUACHE MAZOEA TAIFA LETU NI TAJIRI KWA RASILIMALI ZA ASILI HIVYO BASI TUZITUMIE KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA. TUSITEGEMEE WAGENI KULETA MAENDELO YETU BALI TUWASHIRIKISHE KULETA MAENDELEO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom