johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,035
- 142,150
Rais Samia amelitaka Kanisa la Anglican kuhakikisha linawasaidia Wanawake kupata haki zao za msingi na yeye Rais atalisimamia hilo na anamuomba askofu mkuu baba Mndolwa amsaidie katika hilo.
Rais amesema Wanawake na wanaume wana haki sawa na ndio maana hata darasani wasichana na wavulana wanachuana kwa ufaulu.
Rais amesisitiza kuwa tofauti pekee iliyopo ni ya kimungu yaani uumbwaji ambapo mwanamke amepewa " Fahari" ya kubeba mimba na kuzaa mtoto kitu ambacho mwanaume hawezi
Ndio maana katika makabila mengine mtoto ni wa mama amesema
Source: Upendo tv!
===================================
“Wanawake ni zaidi ya 50% kwenye nchi hii mkituacha nyuma nchi itaendelea lini na malengo ya kimataifa yanatuambia mtu asiachwe nyuma, sasa mnapowadogosha wanawake, mkawanyima haki zao, mkawanyang'anya ardhi zao maendeleo yatakuja lini"
“Mimi nabeba mimba najifungua wewe huwezi, Mungu amenipa heshima ya kuleta viumbe wengine duniani, unachokifanya wewe (Mwanaume) ni kunichangia tu mbegu yako, mengine yote nafanya mwenyewe, ndiyo maana makabila mengine mtoto ni wa Mama"
“Mzigo alionipa Mungu ni mkubwa na ni heshima, lazima niheshimiwe, nyote nimewaleta mimi, nimewakuza, ukiumwa ni mimi, shibe yako ni mimi, raha yako ni mimi, sasa unaponiona ni mtu wa daraja la pili sikuelewi"
“Mwanamke anaweza kufanya kama anavyofanya mwanaume, tulizaliwa sawa hata darasani si tulikuwa tunawapita, matokeo tunayoyashuhudia sasa hivi ya kidato cha nne na sita wanaoongoza ni wanawake lakini inapokuja kwenye madaraka na haki za kiuchumu wanaonekana hawafai,”