Rais Samia: Mwanamke ana haki sawa na Mwanaume. Wanawake lazima waheshimiwe na kupewa Haki zao!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,512
141,240
Rais Samia amelitaka Kanisa la Anglican kuhakikisha linawasaidia Wanawake kupata haki zao za msingi na yeye Rais atalisimamia hilo na anamuomba askofu mkuu baba Mndolwa amsaidie katika hilo.

Rais amesema Wanawake na wanaume wana haki sawa na ndio maana hata darasani wasichana na wavulana wanachuana kwa ufaulu.

Rais amesisitiza kuwa tofauti pekee iliyopo ni ya kimungu yaani uumbwaji ambapo mwanamke amepewa " Fahari" ya kubeba mimba na kuzaa mtoto kitu ambacho mwanaume hawezi

Ndio maana katika makabila mengine mtoto ni wa mama amesema

Source: Upendo tv!

===================================

“Wanawake ni zaidi ya 50% kwenye nchi hii mkituacha nyuma nchi itaendelea lini na malengo ya kimataifa yanatuambia mtu asiachwe nyuma, sasa mnapowadogosha wanawake, mkawanyima haki zao, mkawanyang'anya ardhi zao maendeleo yatakuja lini"

“Mimi nabeba mimba najifungua wewe huwezi, Mungu amenipa heshima ya kuleta viumbe wengine duniani, unachokifanya wewe (Mwanaume) ni kunichangia tu mbegu yako, mengine yote nafanya mwenyewe, ndiyo maana makabila mengine mtoto ni wa Mama"

“Mzigo alionipa Mungu ni mkubwa na ni heshima, lazima niheshimiwe, nyote nimewaleta mimi, nimewakuza, ukiumwa ni mimi, shibe yako ni mimi, raha yako ni mimi, sasa unaponiona ni mtu wa daraja la pili sikuelewi"

“Mwanamke anaweza kufanya kama anavyofanya mwanaume, tulizaliwa sawa hata darasani si tulikuwa tunawapita, matokeo tunayoyashuhudia sasa hivi ya kidato cha nne na sita wanaoongoza ni wanawake lakini inapokuja kwenye madaraka na haki za kiuchumu wanaonekana hawafai,”
 
Watafanya nini bila ya mchango wa mbegu. Wao ni ubavu tu kutoka kwa mwanamume. Mwanamume ni kichwa cha nyumba/familia kama Kristo alivyo kwa Kanisa na Taifa hujengwa kuanzia kwenye familia zetu. Ajue hapo anapo hutubia ni mkutano wa kanisa na silazima sana kutaka kujilinganisha, ajiamini mbona anasongesha taifa mbele na ni mwezi wa saba mambo yanaenda. Mambo yaleyale UNGA tujisahihishe.
 
Biblia. 1 Wakorintho 11:3
[3]Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.
But I would have you know, that the head of every man is Christ; and the head of the woman is the man; and the head of Christ is God.
 
Rais Samia amelitaka Kanisa la Anglican kuhakikisha linawasaidia Wanawake kupata haki zao za msingi na yeye Rais atalisimamia hilo na anamuomba askofu mkuu baba Mndolwa amsaidie katika hilo.

Rais amesema Wanawake na wanaume wana haki sawa na ndio maana hata darasani wasichana na wavulana wanachuana kwa ufaulu.

Rais amesisitiza kuwa tofauti pekee iliyopo ni ya kimungu yaani uumbwaji ambapo mwanamke amepewa " Fahari" ya kubeba mimba na kuzaa mtoto kitu ambacho mwanaume hawezi

Ndio maana katika makabila mengine mtoto ni wa mama amesema

Source: Upendo tv!
Ameanza "kambeni ya uchaguzi" wa mwaka 2025? Terrible!😝😝😝😝
 
Biblia. 1 Wakorintho 11:8-10
[8]Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.
For the man is not of the woman; but the woman of the man.
[9]Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.
Neither was the man created for the woman; but the woman for the man.
[10]Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.
For this cause ought the woman to have power on her head because of the angels.
 
Haki sawa kweli ni Vema na Haki....

Ila kunganganiza namba sawa hata kama kuna watu wawili unaowahitaji ila wa kiume ana uwezo kuliko wa kike ukamchukua wa kike ili tu ufikie zile idadi za pasupasu huo tena sio usawa.....

Tusinganganize sijui uongozi, siasa n.k. huenda kuna kazi wanawake haziwavutii sio kwamba hawawezi bali wengi wao hawajitokezi
 
Back
Top Bottom