Rais Samia, mwagize RC. Amos Makalla amsaidie mjane huyu, ni aibu kwa Serikali Yako!

Desprospero

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
887
2,201
KUNA mambo yanafanyika nchi ambayo unaweza kuyakuta katika Banana Republic tu au "nchi ya kusadikika" isiyojali wala kuzingatia haki na misingi ya kisheria.

Wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiagiza wavamizi wa ardhi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa KIA mkoani Kilimanjaro walipwe fidia Ili kupisha eneo hilo kufanyiwa upanuzi wa uwanja hali ni tofauti kabisa kwa mama mjane Bi. Habiba Nassoro Mtema (mke wa marehemu Priva aliyewahi kuwa M/Kiti wa Simba SC).

Mjane huyu anamiliki kihalali na kisheria kiwanja Na. 200 Kitalu B Part 1 kilichopo Mtaa wa Liwiti eneo la Segerea-Wilayani Ilala mkoa wa Dar es salaam toka mwaka tarehe 7/11/1985 kupitia kampuni yake ya Jacqualine Enterprices Limited.

Pamoja na kwamba mjane huyu amekuwa akilipia kodi ya ardhi bila kuchelewa toka mwaka huo lakini mamlaka ya Serikali yako (SSH) kupitia ofisi za Ardhi Manispaa ya Ilala imemzuia mama huyo asiweze kupaendeleza na hata pale alipojaribu kufika maeneo hayo Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa pamoja na Diwani walimletea "wananzengo/vijana) ili wamshambulie mama huyo na familia yake jambo ambalo bila Jeshi la Polisi kuingilia kati pengine angedhulumiwa uhai wake.

Kinachomsononesha mama huyu ni kwamba mnamo tarehe 4/9/2012 Mkurugenzi wa Halmashauri kupitia barua yenye Kumb. Na. IMC/NT/04 ilimwandikia mama huyu kumjulisha kuwa hilo eneo ni mali yake halali na kama Serikali itapahitaji kubadili matumizi basi ni lazima afidiwe kisheria.

Lakini wakati huo huo ndani ya kipindi kifupi ofisi hiyo hiyo na mtu yule yule kupitia barua Kumb. Na. DSM/ILA/D7/4/273/VOL.IV/45 ikamwandikia mama huyo kupitia kwa mawakili wake kumjulisha kuwa kiwanja hicho kilielekezwa kwa matumizi ya umma.

Mwenyewe mama akibubujikwa machozi anasema, "ninachosema ni kwamba kwa mujibu wa sheria za Tanzania ardhi ni mali ya Serikali na ikitaka kubadili matumizi inafanya hivyo lakini mmiliki anafidiwa". Mjane huyu anaongeza akijifuta machozi, "hivi hata wewe imagine waliovamia ardhi huko Arusha sijui Kilimanjaro wanafidiwa kwa nini mimi ambaye na mume wangu hatukuvamia tusifidiwe kama Serikali inapataka?"

SIASA ZATAWALA KUPORA
Taarifa zilizopo ni kwamba Ili kupata kura za wamachinga, Mbunge wa Segerea Bonna Karua (sasa Bonna Kamole) akisapotiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda waliwaahidi wafanyabiashara ndogo-ndogo wa eneo hilo kuwa wakimchagua atawapa eneo la kufanyia biashara. Hapo ndipo mama huyu alipoporwa Ardhi yake kibabe na wababe na kupageuza kuwa gulio.

Akihojiwa na moja ya chombo cha habari kama anajua sakata hili, Bonna anasema, "siijui hiyo issue, simjui huyo mama na wala sihusiki na masuala ya ardhi. Muulize Diwani ila Liwiti napajua ni kata yangu". Anajua Liwiti lakini hajui gulio! Kituko.

Sasa cheki hizi sarakasi. Diwani wa eneo husika huku akikataa kutaja jina anasema, "suala hilo muulizeni Mstahiki Meya wa Jiji maana Mimi niliingia ofisini 2020 lakini nilioneshwa na wakubwa kuwa hilo ni eneo la umma lakini kama kuna mtu anadai ni eneo lake basi afuate kanuni, taratibu na sheria za nchi siko tayari kumuonea mtu."

Haya Sasa waya mpaka kwa Meya Omari Kumbilamoto ambaye naye anang'aka na kusema:

"Hilo suala nalifahamu, kuna mtu alinijulisha sasa limefikaje huko? Najua linashughuliwa na Mkurugenzi.

Mkurugenzi naye kwa Ushirikiano anamwomba mjane huyu kufika ofisini kwake baaba ya kudai hana jambo hilo ofisini kwake. Mama Nassoro Mtema naye kiguu na njia hadi ofisi ya Mkurugenzi ambaye naye anagani, "ngoja niwasiliane na watu wa mipango miji na ardhi, kwahi njoo Ofisini Ijumaa ya tarehe 10/3/2023 asubuhi.

Huyu mama ameshahangaika kiasi kwamba haoni maana ya siku ya wanawake duniani Yani tarehe 8/3. Kwake ni machungu tu pamoja na kwamba mmoja wa afisa katika ofisi za Mkurugenzi kwa sharti la kuhifadhiwa jina amesema, "sakata hili nalijua na fedha zilishalipwa, hapo suala ni dili imechezwa Kuna watu wamekwapua fedha za huyo mama".

Tayari mawakili wa mama huyu (RCO Advocates) kupitia barua Yao Kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Kumb. RCO/JEL/01/2023 ya tarehe 9/January/2023 imemwandikiw Ilani (notice) kuishitaki ofisi hiyo endapo haitolipa fidia halali ya mama huyu.

Mara kadhaa imesemwa kwamba baadhi ya watendaji wa Serikali wamekuwa wakiitia hasara Serikali kwa tamaa zao zisizoisha. Hakuna namna katika hili isipokuwa ni Rais Samia kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuwawajibisha mafisadi wa ardhi wanaotaka kujinufaiaha na ardhi isiyo Yao. Huu ni uhuni na ujambazi. Samia, msaidie mjane huyu.
 
Back
Top Bottom