Kiturilo
JF-Expert Member
- Sep 27, 2021
- 709
- 2,858
Waziri wa uwekezaji mh Mwambe amenukuliwa akisema kuwa hakuna mkataba wowote wa bandari ya Bagamoyo uliowahi kusainiwa huku akisahau kuwa mwaka 2015 rais wa awamu ya nne Mh Jakaya Kikwete alizindua ujenzi wa bandari hiyo.
Je, Kikwete alizindua ujenzi bila mkataba wowote?
Waziri Mwambe unamdanganya nani?
Jionee mwenyewe kwenye video hii.
Je, Kikwete alizindua ujenzi bila mkataba wowote?
Waziri Mwambe unamdanganya nani?
Jionee mwenyewe kwenye video hii.
Watanzania wote tumemsikia akisema uongo hadharani kweupe kwamba mkataba haukuwahi kusainiwa, kweli? Amekudhalilisha sana wewe Rais Samia, kwani huyu kala kiapo cha uaminifu.
Kuhusu bandari ya Bagamoyo mkataba ulisainiwa kitambo sana na serikali ya awamu ya nne na jiwe la msingi kuwekwa na Rais Jakaya Kikwete.ushahidi upo .
Uliwahi kuona wapi jiwe la msingi kuwekwa kabla ya mkataba kusainiwa? Mawaziri mfano wa Mwambe ni kirusi kibaya sana kwenye baraza la mawaziri.
Tunabaki pale pale kwa kuamini alichokisema hayati Magufuli kwamba mkataba ule ulikuwa wa hovyo sana ndio maana mazungumzo yanaanza kurekebisha unyonyaji uliopachikwa taifa letu.
Mwisho,
Mwambe anataka Magufuli aendelee kudhalilishwa kwa kumsemea uongo, kesho na wewe ukimaliza muda wako atakusemea kama alivyofanya kwa Magufuli.