Rais Samia: Msiseme Mama anazunguka tu, sitozunguka bila sababu

Enhe! Ulicheza michezo kwenye nchi nyingi, tuambie michezo gani hiyo?
Hahaha, anamaanisha ameshatembea nchi nyingi hapo nyuma (Misemo ya kiunguja hii mkuu, tuizoee), kwa sasa anatembea kwa manufaa ya TZ tu
 
Sina uhakika kamaSamia ana mkono katika kesi ya kumbambikia Mbowe, lakini mambo katika mengine mengi, I support Madam president.

Katika yote mazuri yenye dhamira njema, Mungu akubariki Samia, na akujalia hekima zaidi. Mapato yanapoongezeka kwa kiwango cha kuridhisha, punguza au ondoa baadhi ya kodi na tozo. Hiyo itapunguza ukali wa maisha, itaongeza uwekezaji na hatimaye kuongeza ajira.

Kesi ya kubambikiza kwa Mbowe, ndiyo doa pekee kubwa.
Hana mkono mkuu, hiyo kesi ilifunguliwa August 2020, lakini kwa kupisha aibu ya uchaguzi ikabidi iminywe na jiwe ili kusubiri uchaguzi upite, then yakatokea yaliyotokea! Ila soon itakuwa resolved, ndani ya miezi 6 kafanya mengi, ndani ya mwaka mmoja hiyo kesi haitokuwepo tena, tutakaa chini kama wamoja, nadhani Askofu Shoo jana kamaliza kila kitu, tusubiri
 
"Safari nilizokuwa nafanya Nchi Jirani zilikuwa na lengo la kuondosha vikwazo, tumeondosha vikwazo na Kenya na biashara imekuwa mara sita zaidi ya ilivyokuwa, kwahiyo tukizunguka msiseme Mama anazunguka tu, sitozunguka bila sababu, nilishacheza vya kutosha kwenye nchi nyingi duniani, sasa hivi kazi ni moja tu kuzunguka kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania" -Rais Samia akiwa Arusha leo
Safi sana Mama
 
Hahaha, anamaanisha ameshatembea nchi nyingi hapo nyuma (Misemo ya kiunguja hii mkuu, tuizoee), kwa sasa anatembea kwa manufaa ya TZ tu
Basi kama ndio hivyo abadilishe misemo yake ya kizanzibari.
Kumbukumbu zinaonyesha Rais wa awamu ya pili Mzee Mwinyi aliwahi kusema: sisi watanzania tumekalia UCHUMI!. huku bara neno hilo la kukalia uchumi, likaleta tafsiri ya Kibarabara.
 
Au kuna ile alisema "UKIMWI umekaa PAHALA PATAMU", watu walitafsiri kibarabara pia
 
Sina uhakika kamaSamia ana mkono katika kesi ya kumbambikia Mbowe, lakini mambo katika mengine mengi, I support Madam president.

Katika yote mazuri yenye dhamira njema, Mungu akubariki Samia, na akujalia hekima zaidi. Mapato yanapoongezeka kwa kiwango cha kuridhisha, punguza au ondoa baadhi ya kodi na tozo. Hiyo itapunguza ukali wa maisha, itaongeza uwekezaji na hatimaye kuongeza ajira.

Kesi ya kubambikiza kwa Mbowe, ndiyo doa pekee kubwa.
Kabisa[emoji1320][emoji1320][emoji1320][emoji1320][emoji1320]
 
Back
Top Bottom