Rais Samia: Msiseme Mama anazunguka tu, sitozunguka bila sababu

Naipendatz

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
5,091
Reaction score
8,243
"Safari nilizokuwa nafanya Nchi Jirani zilikuwa na lengo la kuondosha vikwazo, tumeondosha vikwazo na Kenya na biashara imekuwa mara sita zaidi ya ilivyokuwa, kwahiyo tukizunguka msiseme Mama anazunguka tu, sitozunguka bila sababu, nilishacheza vya kutosha kwenye nchi nyingi duniani, sasa hivi kazi ni moja tu kuzunguka kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania" -Rais Samia akiwa Arusha leo
 
CCM watakuwa na kazi kubwa sana kwenye kampeni aisee, Magufuri alisema hasafiri sababu nchi yetu ni tajiri wenye shida ndio wanakuja, huyu tena naona kama anageuza hiyo kauli.

sasa sielewi hawa watu huwa wanapewa Ilani au Ilani ndio inajichanganya namna hii
[emoji2][emoji2][emoji2] Maendeleo yataletwa kwa kutembea na kuomba misaada Nje...pathetic...
 
CCM watakuwa na kazi kubwa sana kwenye kampeni aisee, Magufuri alisema hasafiri sababu nchi yetu ni tajiri wenye shida ndio wanakuja, huyu tena naona kama anageuza hiyo kauli.

sasa sielewi hawa watu huwa wanapewa Ilani au Ilani ndio inajichanganya namna hii
Watanzania tunasahau mapema sana mkuu ,kwaio hakutakua na shida
 
Umesahau Kama huyo jiwe wako ndo alisababisha hata mahindi tusiuze Kenya ,mama.ameenda Leo mahindi yanaenda bila shida bado wewe unaona anaenda kuomba msaada?
Kama mahindi yananunuliwa Kenya,mbona hayapandi bei toka tumevuna mpaka Sasahivi gunia la mahindi alizidi elfu 35000/ na ilikuwa hivo hata mwaka Jana
 
CCM watakuwa na kazi kubwa sana kwenye kampeni aisee, Magufuri alisema hasafiri sababu nchi yetu ni tajiri wenye shida ndio wanakuja, huyu tena naona kama anageuza hiyo kauli.

sasa sielewi hawa watu huwa wanapewa Ilani au Ilani ndio inajichanganya namna hii
Matokeo ya Chama maiti hayo
 
Sina uhakika kamaSamia ana mkono katika kesi ya kumbambikia Mbowe, lakini mambo katika mengine mengi, I support Madam president.

Katika yote mazuri yenye dhamira njema, Mungu akubariki Samia, na akujalia hekima zaidi. Mapato yanapoongezeka kwa kiwango cha kuridhisha, punguza au ondoa baadhi ya kodi na tozo. Hiyo itapunguza ukali wa maisha, itaongeza uwekezaji na hatimaye kuongeza ajira.

Kesi ya kubambikiza kwa Mbowe, ndiyo doa pekee kubwa.
 
Huyu mama huyu aache uongo.

Kikwete alikuwa waziri wa mambo ya nje kuanzia mwaka 1995 mpaka 2010. Waziri wa mambo ya nje, hivyo kama kuna mtu alicheza huko nje alikuwa ni Mheshimiwa Kikwete.

Then alipokuwa Rais sasa ikawa ndio kama karogwa, mwaka 2015 Rafiki yangu Mheshimiwa Membe alisema kwamba kipindi cha mwaka 1995 mpaka 2010 watumishi wa serikali walikuwa wanapishana anganani kama vile huku chini kunawaka moto.

Maanake Kikwete alikuwa anasafiri asikuambie mtu, na kimsingi safari zake zote zilikuwa ni katika ufujaji tu, sababu mpaka sasa sielewi tulifaidika nazo kivipi, kuna kipindi alienda akapiga picha kibao ofisi za google, aliporudi hapa akadai google wanakuja, then google wakaja kweli KENYA.

Kuna kipindi sijui alikosana nini na akina mseveni, yaani hapo sasa ndio alikomeshea, akina mseven wakikutana Kampala yeye huyo London, akirudi akakuta bado wanaendelea na vikao vyao kampala anaingia ikulu anabadiri nguo huyo tena New York.

Sasa naanza kuamini inawezekana kweli kuna mambo kikwete anamuambia huyu mama
 
Nonsense !

Unatupigia kelele tu na maujinga yako na chuki zako binafsi kwa raisi Samia na raisi mstaafu kikwete.
 
Wamachinga wanatia huruma Sanaa.nikiwaona jinsi wanavyobomoa mabanda yao.hadi huruma.
 
"Safari nilizokuwa nafanya Nchi Jirani zilikuwa na lengo la kuondosha vikwazo, tumeondosha vikwazo na Kenya na biashara imekuwa mara sita zaidi ya ilivyokuwa, kwahiyo tukizunguka msiseme Mama anazunguka tu, sitozunguka bila sababu, nilishacheza vya kutosha kwenye nchi nyingi duniani, sasa hivi kazi ni moja tu kuzunguka kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania" -Rais Samia akiwa Arusha leo
Wamchukue tu hata miezi 6...
 
Back
Top Bottom