Rais Samia: Mimba za utotoni zimeongezeka Dar

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika Mikoa ya Dar es salaam, Njombe na Ruvuma viwango vya mimba za utotoni vimeongezeka, huku mapambano ya kupunguza idadi ya mimba hizo yakirudi nyuma ambapo amewataka Wazazi waendelee kuwalinda Watoto wetu dhidi ya mimba za utotoni.

Rais Samia amesema hayo wakati akizindua Ripoti hiyo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya Mwaka 2022 na Ugawaji wa Magari ya Kubebea Wagonjwa na Vifaa Tiba Jijini Dar es salaam.

Rais Samia amenukuliwa akisema “Mkoa wa Dar es salaam, Chalamila uko wapi?, upo?, kwa Mkoa wako wa Dar es salaam mmerudi nyuma kutoka 11.9% sasa mko 18.1% mmelegeza wapi sijui kajiangalieni”

“Njombe wametoka 19.7% wamepanda mpaka 25.5% kuna nini kajiangalieni, Ruvuma mmetoka 32% mmekwenda 37.2% kaangalieni sababu za hili mzifanyie kazi, nitoe wito kwa Wazazi tuendelee kuwalinda Watoto wetu dhidi ya mimba za utotoni”
 
Inasikitisha sana, wakati huo serikali na jamii ikipambana kutokomeza mimba za utotoni kuna mashehe wanataka mabinti wadogo waolewe punde tu wanapovunja ungo,inasikitisha sana.
 
Culture na social behaviour vinachangia. Unzinzi unatangazwa wazizi huku wazazi wakiangalia tu

This is the outcome
 
Maadili ya Kihuni huni ya Kimrisho Mpoto Mpoto ni kwanini Watoto wasipigwe Mimba?
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Analalamika nini!!?? Si ni yeye mwenyewe aliruhusu wazazi warudi shule,jambo ambalo limewafanya raia wasione kuwa nishida kwa mabinti wadogo kunasa mimba.
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika Mikoa ya Dar es salaam, Njombe na Ruvuma viwango vya mimba za utotoni vimeongezeka, huku mapambano ya kupunguza idadi ya mimba hizo yakirudi nyuma ambapo
Hali ya kiuchumi imekuwa mbaya madaraja ya kipato yamekuwa ni tofauti mno ukifanya utafiti hapo wasio kuwa na uhakika wa kula ya siku ndio wengi wao walioathirika!
 
Magufuli aliwaambia kuna shule za bure hivyo wafyatuane! Ndio shida kubwa ya nchi hii hakunaga continuation ya sera au mipango. Taifa lilipiga hatua sana jatika kudhibiti kuzaliana hovyo bila mpango na gharama kubwa zilitumika katika hilo kuingia yule pang'ang'a tukarudi nyuma watu walianza zaliana hovyo utasema watakula hizo shule.

Nilikua Ruvuma siku moja kila hatua moja unakutana na mtoto kabeba mtoto yaani ni kichefu chefu!
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Mimba za utoto Dar zapanda hadi 18.1%, Rais Samia aongea haya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom