Rais Samia, mbona kila unaloagiza watendaji wakuu wanakugomea?

Kauli za viongozi kama Mwigulu, Ndugai na Mbunge Gwajima ziko wazi kabisa hawakubaliani na wewe katika yale unayo agiza.

Sio hayo ya miamala na chanjo za corona pekee, lakini kuna jingine kubwa mno ambalo Watumishi waathirika na zoezi la vyeti wanakutazama kwa mshangao.

Ulitoa agizo kuwa watumishi walio ondolewa kazini kwa matatizo ya majina na vyeti ambao walikuwa wanakatwa fedha kupelekwa kwenye mifuko ya jamii walipwe pesa zao kwani ni jasho lao na serikali sio ya kudhulumu haki za watu.

Ulisisitiza hilo ni AGIZO. Lakini watendaji kama kawaida yao Wamedharau na hawajawalipa na wakihoji wanakejeliwa.

Kwa nini wanakudharau namna hii?

Au kwa vile serikali iliyopo hukuiunda wewe bali umeipinduapindua tu?

This is 2021, na hadi 2025 ni mbali mno na utaona ugumu wa kubaki na hawa watu wa mwendazake!
SAMIA na MAGUFULI ni kitu kimoja.

Unataka nini tena?

Au uhamia Burundi basi.
 
Asipoangalia Ndugai na Mwigulu watamsumbua sana......kuelekea 2025....muda mwalimu mzuri
 
Rais,na Wizara wanasema watu wachanjwe kwa hiari,Gwajima wanasema watu wasichanjwe kabisa.
Naona kama Watu Wanamdharau Rais SAMIA.
Gwajima anaibuka na kauli hizo baada ya kuibuka kundi la mandezi wachache ambao walianza kushinikiza chanjo ziwe za lazima,tena zaianzie kwa askari kama majaribio.
 
Kauli za viongozi kama Mwigulu, Ndugai na Mbunge Gwajima ziko wazi kabisa hawakubaliani na wewe katika yale unayo agiza.

Sio hayo ya miamala na chanjo za corona pekee, lakini kuna jingine kubwa mno ambalo Watumishi waathirika na zoezi la vyeti wanakutazama kwa mshangao.

Ulitoa agizo kuwa watumishi walio ondolewa kazini kwa matatizo ya majina na vyeti ambao walikuwa wanakatwa fedha kupelekwa kwenye mifuko ya jamii walipwe pesa zao kwani ni jasho lao na serikali sio ya kudhulumu haki za watu.

Ulisisitiza hilo ni AGIZO. Lakini watendaji kama kawaida yao Wamedharau na hawajawalipa na wakihoji wanakejeliwa.

Kwa nini wanakudharau namna hii?

Au kwa vile serikali iliyopo hukuiunda wewe bali umeipinduapindua tu?

This is 2021, na hadi 2025 ni mbali mno na utaona ugumu wa kubaki na hawa watu wa mwendazake!
Yeye mwenyewe ni mtu wa mwendazake, atawaacha vipi hao wanaoonekana kuwa wasaliti?. Cha muhimu ni kuchapa kazi na kuwaamini wote wanaomzunguka.
 
Siyo hao tu Bali Kuna wastaafu kibao wamepunjwa haki zao mfano unastaafu ukiwa ngazi ya mshahara kidato 'F' unalipwa ya chini yake kidato 'E'
 
Bavicha nyie wajinga sana aisee!

Watu wa mwenda zake ni wapi? Yeye Samia pia si mtu wa mwenda zake?
 
Rais huyu ni mvivu wa kuunda serikali yake mwenyewe.

Ngoja ajivutevute, Asipouanika atautwanga mbichi.

Mwanzo alivyoingia madarakani alitangaza bei za bando zishushwe, kuna makampuni yakamgomea!
Hayo makampuni yalimgomea sababu ya selikali kuwa siyo ya samia?
 
Back
Top Bottom