Rais Samia kusomesha vijana 20 wasiojiweza

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,122
676
Rais Samia Suluhu katika ufunguzi wa chuo cha ufundi mkoani Kagera leo ameongelea mambo mengi sana lakini lililonikosha ni hili la kusomesha vijana wanaotoka katika familia duni hii inaonyesha kua Rais Samia Suluhu anampango wa kuwainua vijana na kuondokana na Tatizo la ajira Tanzania kupitia elimu ya ufundi.

Amesema "Nimemsikia Waziri anasema kwenye Chuo hiki cha Veta hapa Kagera vijana 400 watakuwa wa mafunzo ya muda mrefu, kati ya vijana hao vijana 20 wanawake 10 na wavulana 10 wale ambao wanyonge hawana uwezo wa kujilipia nitawalipia mimi." Rais Samia Suluhu

Pia ameongeza kua vijana watakaomaliza chuo hicho cha ufundi waandaliwe mazingira mazuri ya kujiajiri na kuajiriwa lakini pia ameongeza kua Mafundi stadi wengi wanahitajika katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati nchini kuna bomba la mafuta linalotoka Uganda kuja Tanzania kuna bwawa kubwa la Nyerere na kuna utekelezaji wa ujenzi wa barabara.

Rais Samia Suluhu anastahili pongezi.
 
Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,122
676
Serikali anayoindesha imeshindwa kuwalipia ila yeye binafsi atawalipia!!

Kwa nini kusiwe na sera ya kuwasaidia watu kama hao badala ya kutegemea hisani ya viongozi??
Watu wasiojiweza wanasaidiwa na mfuko wa TASAF na hivi vyuo vya afya vinajengwa kwaajili ya wananchi wasio na uwezo wa kuafford gharama za vyuo vya private
 
Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,122
676
Duh.yaani watu 20 tu hadi wanatutangazia.kwa kodi zote wanazowakamua wtz halafu wanasomesha wtz 20.
Sasa wewe unataka asomeshe Tanzania nzima jamani hata hao wanaojilipia serikali itakua inawalipia maana ada haizidi laki 2 mkuu Rais Samia Suluhu anafanya kazi kubwa tumpe sifa zake
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
18,573
51,315
Bora angerudisha ada kwenye elimu ya sekondari, halafu elimu ya VETA ikawa bure ili kuhamasisha vijana kujiajiri. Maana elimu ya sekondari kwa mtazamo ni useless tu.
 
mapesa yamejaa

JF-Expert Member
Dec 29, 2021
740
1,679
Sasa wewe unataka asomeshe Tanzania nzima jamani hata hao wanaojilipia serikali itakua inawalipia maana ada haizidi laki 2 mkuu Rais Samia Suluhu anafanya kazi kubwa tumpe sifa zake
Inatakiwa kuwepo sera ya kuwapa mikopo wote waliopo veta na wakishaajiriwa watalejesha kidogokidogo.Tozo tunazolipa wtz ni nyingi sana tukizitumia vuzuri
 
Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,122
676
Bora angerudisha ada kwenye elimu ya sekondari, halafu elimu ya VETA ikawa bure ili kuhamasisha vijana kujiajiri. Maana elimu ya sekondari kwa mtazamo ni useless tu.
Ni kama bure tu mkuu maana haitazidi laki mbili na ukimaliza hapo kazi uhakika
 
Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
14,992
27,071
Anawasaidia vijana wa kitanzania kupata elimu ya ufundi ili waweze kujiajiri na kuajiriwa hili ni jambo kunwa sana
Yeye kama Rais anawezaje kusemwa kuwa "anasaidia" kwani kuwasomesha hao vijana ni kazi ya nani mpaka isemwe yeye anasaidia??
 
Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,122
676
Inatakiwa kuwepo sera ya kuwapa mikopo wote waliopo veta na wakishaajiriwa watalejesha kidogokidogo.Tozo tunazolipa wtz ni nyingi sana tukizitumia vuzuri
Ndio maana ata gharama yake ni ndogo mkuu kwaiyo na wakimaliza watapewa pesa kutoka kwenye 10% ya mapato ya halmashauri ili waweze kujiajiri hili ni bonge la fursa mzee Rais Samia Suluhu anaupiga mwingi sana
 
Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,122
676
Yeye kama Rais anawezaje kusemwa kuwa "anasaidia" kwani kuwasomesha hao vijana ni kazi ya nani mpaka isemwe yeye anasaidia??
Hapo anawasomesha kwa pesa ya mfukoni kwake na sio ya serikali mzee Rais Samia Suluhu anaipenda sana nchi yake Mungu amuweke
 
Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
14,992
27,071
Hapo anawasomesha kwa pesa ya mfukoni kwake na sio ya serikali mzee Rais Samia Suluhu anaipenda sana nchi yake Mungu amuweke
Kwa nini atoe pesa ya mfukoni mwake??

Yaani serikali inayokusanya kodi inashindwa yeye kwa fedha za mfukoni mwake atawezaje??
 
Per Diem

JF-Expert Member
Mar 28, 2018
783
1,242
Kwa nini atoe pesa ya mfukoni mwake??

Yaani serikali inayokusanya kodi inashindwa yeye kwa fedha za mfukoni mwake atawezaje??
Nimeziona hoja zako zina ukweli. Samia ni binadamu, akifa leo? Maana yake hao vijana watashindwa kulipa ada na watashindwa kuendelea na masomo. Ila mfumo mzuri ukiweka wa kusaidia watu wa hivyo hata Leo akifa hao vijana wataendelea kulipiwa ada
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom