Rais Samia kupokea ndege mpya ya ATCL Julai 30, 2021

Between 1962-1985 nyerere had bought 14 aircrafts.

Sasa kama role model wenu/wetu (politically)
aliona umuhimu wa kununua ndege ktk nyakati zile leo mnatwambia nini.

Ni Watz wangapi kwa nyakati zile waliweza kuziona zile ndege licha ya kuzipanda kabisa?
 
Hizi zilishawekewa order kwenye awamu ya JPM kwahiyo hatuna ujanja lazima zije tu zote.
Twendeni sawa na huyu kiti moto
๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท๐Ÿท
๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น๐Ÿ‘น
 
Na utaona msafara wa viongozi kwenda kushabikia!

Matatizo yaliyopo ni mengi kupita na viongozi wapo! Mshahara wanapokea kila mwezi! Kutembelea magazine bei mbaya! Walipe kodi basi!

Huku wanafunzi wanakufa kufukiwa kifusi! Kisa choo hakuna shjleni kinajengwa kwa nguvu za wanafunzi kubeba changa!
Maji hakuna kila kona Zima moto wanashindwa kuzima moto!!

WaTanzania tuamke kukemea haya yanayoenda sio kushabikia! Siasa zimetawala uwajibikaji..
 



Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Julai 30, 2021 anatarajiwa kupokea ndege mpya aina ya Bombardier Dash 8-Q400, hafla itakayofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Kupokelewa kwa ndege hiyo kutafanya idadi ya ndege ambazo tayari zimefika nchini kuwa tisa, kati ya ndege 11 ambazo serikali imenunua.

Ndege nane ambazo tayari zimepokelewa nchini ni ndege nne aina ya Bombardier Dash 8 Q-400 (zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja), Ndege mbili aina ya Boeing 787 โ€“ 800 Dreamliner (zenye uwezo wa kubeba watu 262 kila moja) na ndege mbili aina ya Airbus A220-300 (zenye uwezo wa kubeba abiria 160 kila moja).

Sababu kuu zilizochochea serikali kufufua Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ni kujenga heshima na kulinda hadhi ya Taifa, kwani Tanzania imejijengea sifa kemukemu duniani hivyo ilikuwa aibu kutokuwa na ndege.

Pili, ni kuimarisha na kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini ili kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kuyafikia masoko ya kimataifa kwa urahisi.

Sababu ya tatu ni kukuza sekta ya utalii ambapo licha ya Tanzania kuwa ya pili kwa vivutio vingi vya utalii duniani, bado idadi ya watalii wanaoitembelea sio wengi kutokana na uwezo mdogo wa kusafirisha watalii.
 
Imagine mtu ameshakufa lakini bado anaendelea kulitia hasara hili taifa. Mungu turehemu
 
Itakuwa vyema lau wata ondoa ule usumbufu wa kuahirisha safari kila wakati
 
Sababu zote zilizopelekea kununuliwa hiyo midege zilizotajwa hapo juu ni sababu mfu.
Watanzania bado wana changamoto katika sekta ya afya, elimu pamoja na makazi.
Kwamba viongozi wetu wameshindwa kutumia akili kupanga jinsi ya kuyatumia hayo mabilioni kutatua changamoto muhimu mpaka wananuua vitu vya maonyesho?
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Julai 30, 2021 anatarajiwa kupokea ndege mpya aina ya Bombardier Dash 8-Q400, hafla itakayofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam...
Sawa
 
Wiki iliyopita kulikuwa taarifa ya Management ya Atcl kutafuna minoti,naona kimyaa iliishia wapi?.
 
Back
Top Bottom