Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,136
- 884
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kinara wa Umoja wa Afrika wa Masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuwaongoza Viongozi wakuu wa nchi Barani Afrika na Wadau wa Maendeleo kujadili na kuhamasisha uwekezaji katika afya ya uzazi, mama, mtoto mchanga na mtoto, Afrika.
Kikao hicho cha ngazi ya juu kinatarajiwa kufanyika Septemba 23, 2026, Jijini New York, Marekani, pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA-81) huku Rais Samia akiwa mwenyeji wa kikao hicho katika nafasi yake ya Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Mama na Mtoto.
Miongoni mwa matokeo yanayotarajiwa ni kupitishwa kwa tamko rasmi la kuharakisha hatua za kukomesha vifo vinavyoweza kuzuilika vya mama, mtoto mchanga na mtoto, pamoja na kutangazwa kwa ahadi za uwekezaji kutoka kwa nchi na washirika wa maendeleo.
Kwa Tanzania kuongoza ajenda ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto sii jambo lililoibuka siku moja, hapana. Ni utashi wa kisasi, nia ya uwajibikaji na kuchukua hatua zenye kuleta matokeo ndio zilizochangia mafanikio makubwa ya uboreshaji wa huduma hizo.
Hatua hii inaendeleza dhamira ya dhati ya Rais Samia kwenye masuala ya afya ya uzazi, mama na mtoto yanaendelea kupewa kipaumbele, huku Tanzania ikiwa sehemu ya juhudi ndani ya Bara la Afrika katika kuharakisha upatikanaji wa huduma bora na salama kwa wanawake na watoto ifikapo mwaka 2030.