Rais Samia Kumbuka Fao la Kujitoa

Rais Samia Kumbuka Fao la Kujitoa

Nahisi kuna watumishi wasiowaminifu zile pesa wanajikopa. Ndio maana hawaziingizi mpaka ukapige kelele
Kama ni ivyo mbona pesa tunalipia kupitia bank,wanawezaje kuzitoa tena
 
Umechangia hoja kama wengine tunavyofanya,naomba unijibu
Swali hili, Je,sheria iliyomtaka mwajiri achangie mwajiliwa 10% kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii ilianza kufanya kazi mwaka gani?
na wakati huo fao la kujitoa lilikuwepo au ilipoanzishwa na fao hilo likafutwa?

Sheria ya Mwajiri kuchangia 10% na zilizobaki 10% za mwajiriwa ndiyo msingi wa Sheria ya kuanzisha ya NPF 1964, ambayo ilikuja kuwa NSSF 1998.

Katika sheria ya msingi na hadi zote hakuna Fao la Kujitoa. Take it from me.
 
KUONDOKEWA MAFAO YA KUJITOA NI KWA MANUFAA YA WANACHAMA

Nimesoma yote yaliyoandikwa na wadau na kugundua kwamba wote hawafahamu DHANA YA HIFADHI YA JAMII. Kwa sisi tuliopiya IFM, ninvyema tukatoa elimu kidogo kwa ndani gu zetu ambao hawaelewi vizuri jambo hili. Kwa taarifa, dhana msingi ya Hifadhi ya Jamii ni:-

“Kumfanya mtu kuweka akiba kidogokidogo wakati ana uwezo wa kutengeneza mapato ili akiba hiyo imfae wakati atakapokuwa hana uwezo wa kuzalisha mapato”.

Kwa NSSF, Sheria inamtaka Mwanachama kuchangia 10% tu ya mshahara wake; na Sheria hiyo hiyo inamlazimisha Mwajiri kuchangia 10% ya ziada kukamilisha akiba ya Mwanachama huyo. Kwa maana nyingine, Mwanachama asingepata hiyo 10% ya Mwajiri bila ya Sheria hii.

Akiba hii inapaswa kuendelea kujaziwa kwa kipindi chote cha Mwanachama akiwa na uwezo wa kufanya kazi. Wakati mtu anapochangia 10% ya mshahara wake, anabaki na 90% ya mapato yake. Kudundiliza huku kutaendelea kwa kutumia waajiri mbalimbali atakaofanya nao kazi katika maisha yake.

Kama ni mjasiriamali mzuri, atatumia kiasi kingine kidogo kutoka 90% ili kudunduliza mtaki kwa muda fulani na kuanza biashara. Kama atashindwa kufanya hivyo hadi siku anakosa ajira ndiyo aanze kupambania 10% aliyokuwa anaweka ili aanzisjie biashara, huyo siyo mjasiriamali. Na uwezekano mkubwa ni kwamba hata akizipata hazitamfikisha mbali na itambidi atafute kazi tena ya kuajiriwa.

Sasa wakati akifikia utu uzima na uwezo wa kuchakarika kufanya kazi haupo, ndiyo sasa ataanza kupata pensheni ya kila mwezi hadi mauti yatakapomchukua. Kama aliwahi kuanzisha biashara na ikafanikiwa, maisha yake ya uzeeni yatakuwa mazuri. Kama hakuwahi kuanzisha biashara, basi atakuwa na uhakika wa kupata mahitaji yake muhimu.

Fursa za kuanzisha biashara ziko nyingi tu kwa wajasiriamali waziri. Tukumbuke Bilionea Reginald Mengi alianzisha IPP wakati yeye ni mwajiriwa wa PWC mpaka pale kampuni yake ya IPP ilipokuwa kubwa sana ndipo akaacha kazi. Unaweza ukachangia SACCOS au ikaweka fedha zako Benki na baadae ukachukua mkopo kuanzisha biashara. Kama haya yote huyawezi, kuwa na uhakika hata akiba yako ya NSSF ya 10% haitakusaidia kitu.

Kila mfumo umeanzishwa kwa makusudi yake na taratibu husika lazima zifuatwe. Kama kwa bahati mbaya makusudi haya hatyajui vizuri tuepuke kufanya kosa na kuongea bila elimu na kuanza kuwatukana watu matusi wasiyostahili.
Na wewe acha mambo ya kitoto,sheria yenyewe inataka mtu achangie walau miezi 180 ndio ukidhi kuweza kuwa covered na pension baada ya kustaafu.

Sasa Kazi zetu nyingi hazifiki huko,kwa nini nisipate changu? Maana hata ukifika uzee hutolipwa kwa sababu hukukidhi matakwa ya kuchangia.

Tunataka fao la kujitoa la sivyo sheria ya kuchangia iwe miaka 5 sio 15.
 
No please, fao la kujitoa lipo kwaajili ya kumlinda mwaajiriwa pale anapo kosa ajira au pale ambapo mwajiri wake amefilisika. Fao la kujitoa ni haki ya mwajiriwa ila awe nje ya ajira. Kwa mfano Mtu amefukuzwa kazi, ameugua kwa mda mrefu au mkataba haujaongezwa kama kwenye sekta binafsi unaenda kwenye Fao la kujitoa kwaajili ya kukulinda kipindi chote ambacho utakosa ajira.

Rais alifikilie hili suala la fao la kujitoa kwa kina, waajiriwa wengi waliokoondolewa kwenye ajira hasa sekta binafsi, wanapata shida huku pesa zao zipo NSSF zinatumika kwenye Mambo ambayo si ya msingi kwa uanzishwajo wa mfuko huo.
Kwa unskilled wameliacha ila skilled wamezuia.
 
KUONDOKEWA MAFAO YA KUJITOA NI KWA MANUFAA YA WANACHAMA

Nimesoma yote yaliyoandikwa na wadau na kugundua kwamba wote hawafahamu DHANA YA HIFADHI YA JAMII. Kwa sisi tuliopiya IFM, ninvyema tukatoa elimu kidogo kwa ndani gu zetu ambao hawaelewi vizuri jambo hili. Kwa taarifa, dhana msingi ya Hifadhi ya Jamii ni:-

“Kumfanya mtu kuweka akiba kidogokidogo wakati ana uwezo wa kutengeneza mapato ili akiba hiyo imfae wakati atakapokuwa hana uwezo wa kuzalisha mapato”.

Kwa NSSF, Sheria inamtaka Mwanachama kuchangia 10% tu ya mshahara wake; na Sheria hiyo hiyo inamlazimisha Mwajiri kuchangia 10% ya ziada kukamilisha akiba ya Mwanachama huyo. Kwa maana nyingine, Mwanachama asingepata hiyo 10% ya Mwajiri bila ya Sheria hii.

Akiba hii inapaswa kuendelea kujaziwa kwa kipindi chote cha Mwanachama akiwa na uwezo wa kufanya kazi. Wakati mtu anapochangia 10% ya mshahara wake, anabaki na 90% ya mapato yake. Kudundiliza huku kutaendelea kwa kutumia waajiri mbalimbali atakaofanya nao kazi katika maisha yake.

Kama ni mjasiriamali mzuri, atatumia kiasi kingine kidogo kutoka 90% ili kudunduliza mtaki kwa muda fulani na kuanza biashara. Kama atashindwa kufanya hivyo hadi siku anakosa ajira ndiyo aanze kupambania 10% aliyokuwa anaweka ili aanzisjie biashara, huyo siyo mjasiriamali. Na uwezekano mkubwa ni kwamba hata akizipata hazitamfikisha mbali na itambidi atafute kazi tena ya kuajiriwa.

Sasa wakati akifikia utu uzima na uwezo wa kuchakarika kufanya kazi haupo, ndiyo sasa ataanza kupata pensheni ya kila mwezi hadi mauti yatakapomchukua. Kama aliwahi kuanzisha biashara na ikafanikiwa, maisha yake ya uzeeni yatakuwa mazuri. Kama hakuwahi kuanzisha biashara, basi atakuwa na uhakika wa kupata mahitaji yake muhimu.

Fursa za kuanzisha biashara ziko nyingi tu kwa wajasiriamali waziri. Tukumbuke Bilionea Reginald Mengi alianzisha IPP wakati yeye ni mwajiriwa wa PWC mpaka pale kampuni yake ya IPP ilipokuwa kubwa sana ndipo akaacha kazi. Unaweza ukachangia SACCOS au ikaweka fedha zako Benki na baadae ukachukua mkopo kuanzisha biashara. Kama haya yote huyawezi, kuwa na uhakika hata akiba yako ya NSSF ya 10% haitakusaidia kitu.

Kila mfumo umeanzishwa kwa makusudi yake na taratibu husika lazima zifuatwe. Kama kwa bahati mbaya makusudi haya hatyajui vizuri tuepuke kufanya kosa na kuongea bila elimu na kuanza kuwatukana watu matusi wasiyostahili.
Kuwa na elimu ndogo ni msiba kuliko kutokuwa na elimu kabisa. Mtu ana maneno ya kukaririshwa nae anadai ana elimu, pole!
Mifuko hii lengo mahususi ni kuwanyonya wanachama ili waendelee kuwa tegemezi. Kama ni tija, basi ingekuwa inatoa riba kwa kila fedha ya mwanachama kwani wao wanafanyia biashara hizo fedha na kuvuna faida kubwa kwa jasho kiduchu. Ukijitambua hutasema 'all over the world' kwani hakuna kitu hicho. Kwa mfano, zipo nchi hadi sasa, afya, maji na elimu ni bure kwa kila raia kwani ni mahitaji ya msingi, lakini si hapa kwetu. Tena zipo zinazotoa fedha za kujikimu kwa kila mtu mzima ambaye hana ajira, kitu ambacho hapa ni tozo tu hata kwa vikongwe. Zipo nchi hazijui kukatika kwa umeme na hivyo wanaweza kuendesha biashara ndogondogo bila kikwazo lakini hapa kukatika umeme inadaiwa ni lazima alafu unataraji tuwe sawa na hiyo ' all over the world' yako kama sote tu mazuzu.
Nimalizie kwa kusema fao la kujitoa ni sahihi tena mwanachama apewe na riba siyo hela alizoweka tu, kama si wanyonyaji. Serikali yenyewe imeshindwa hata kutoa nyongeza za kisheria za mishahara kwa miaka kadhaa, licha ya kushindwa kutoa ajira kwa maelfu ya nguvu kazi, halafu unamwambiaje mtu aajiriwe tena wakati kampuni na mashirika na viwanda vinakufa kiasi cha kukosekana majeneza ya kuvizikia? Toeni haki za watu, wapeni fao la kujitoa.
 
Vipi kuhusu wakulima ambao ni 80% ya watanzania wote
mnafanya nini kuhakikisha wana hifadhi ya uzeeni?
Watu hatulalamiki,tunanyoshea kidole mifumo kandamizi ibadilishwe.

Story za ''all over the world'',ni kodi zetu zinawapeleka huko nje ili mjifunze mambo ya maana mtuletee maendeleo
siyo kujifunza mifumo inayokandamiza peke yake,
Huko duniani,vipi miundombinu ikoje? Kuna wanaochangia visima vya maji na mifugo?
mbona hamuigi kuwapa fedha ya kupunguza ukali wa maisha wasio na ajira,tukajua mnaenda sambamba na ,mifumo ya duniani?
Au mnaona hilo la kutokuwa na fao la kujitoa peke yake ndo la kufanyia kazi?
Wakulima nao wameanza kuingizwa ktk mfumo wa hifadhi ya jamii,
Tembelea ofisini utapata maelezo zaidi
 
Mfano, mtu anafanya kazi ya Ulinzi au vibarua migodini na viwandani?

Kwahiyo, kwa AKILI zenu nzito huyo mtu atafanya kazi mpaka kufikisha miaka 60 ili muanze kumpa pension?

Kama pension Ni kitu muhimu hivyo, mbona hata hao wanaostahili tunaona wanahangaika tu kupata pesa zao?

Mbina wastafu hali zao Ni tete vile vile?
Tuwekee mstaafu mmoja hapa na namba yake tuone ukweli wenyewe
 
Na hao waliofikisha hiyo miaka 60 wakifika ndo wanakwambia jina lako la ukoo lina upungufu wa herufi fulani
unakuta mtu anatembea mpako soli ya kiatu inaisha,wakati kila mwezi mshahara unaletwa kwa majina hayo hayo na hawaulizi wanasubiri ustaafu.
Jambo jingine hasa NSSF unakuta ukiomba statement unapewa unakuta mshimo kibao kama miezi sita n.k
unapewa form umpelekee mwajiri arekebishe,ukipeleka unakuta mwajiri karipa kwa uaminifu ila wao hawajazi.
Ukienda mwaka mwingine unakuta mashimo tena,
Ni kama kuna mchezo mchafu unafanyika,kama sio ni kwa nini unakuta karibia kampuni nzima wote hamjajaziwa,wakati mwajiri anapeleka makato inavyotakiwa?
Sasa fanya uzembe usiende kabisa ukisubiria hiyo miaka sitini ifike
ndo utaelewa ni kwa nini humu wanapiga kelele kuhakikisha fao la kujitoa halirudishwi.
Swala la majina ni umbumbumbu wenu, kwanini utumie majina tofauti kila sehemu, benk magufuli,nssf makufuli,rita maghufuli sasa we unaona hayo majina ni moja
 
Nadhani NSSF ni mojawapo ya shirika la umma lilijaa viazi na VILAZA kupindukia.

Wanachomaanisha Ni kulipana tu hiyo michango ya watu.
Unataka wafanye kazi bila kulipwa,
Je wewe ni mmoja wa wanaofanyakazi bila malipo?
 
Nina jamaa yangu yuko anafia kitandani. Anaumwa sana na matibabu yake yanahitaji hela nyingi. Anapofanya kazi hakuna bima na ni miezi mitatu yuko kitandani kazini kwake wameshasitisha mshahara. Ameomba barua ya kuacha kazi amepewa. Amepeleka NSSF ili alipwe mafao yake eti wanamwambia mpaka atimize miaka sijua 55. Anawambia sina hata uhakik wa kuiona wiki ijayo naombeni mafao yangu yanifae sasa ili nipate matibabu nipone nianze upya lkn wamekataa. Niliumia sana yani jamaa anakufa na hela anayo alaf watarithi na kufaidika wengine.

Walioondoa fao la kujitoa laana hii iwafikie popote walipo
We ni muongo, amelala kitandani halafu hana cheti cha daktari au hajaenda hospital.
Kama ni kweli muelekeze aende hospital jopo la madaktari wathibitishe ugonjwa wake then aende nssf, psssf
 
Huyo anateswa na hofu. Hofu ya kuona kwamba pesa zitakuwa hazikai kwenye mifuko muda mrefu hivyo ulaji wao usio rasmi utatoweka.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
Mimi Maza nimemkubali Sana ame overhaul vitu vingi Sana.Ila kwenye Mifuko hii Kuna mchawi amemtia maza kwenye kichupa
Sector ya Utalii kwa mfano iliathirika Sana wakati Covid 19 mahoteli mengi yalifungwa na Kuna wengine walistaafishwa ki ulazima,kimbembe chake sasa Mafao yametoka robo na mengine mpaka ufikishe miaka 60.
Kwanza hao Staff wa NSSF naona wao ndo wanauwezo wa kumwagia Maza mchanga machoni na akanawa ,wako very arrogant to the extreme,na hawana utu hata robo yaani Hawa they live in separate entity within Tanzania.
Wanapoteza Documents hovyo .

Particulars za mtu na Data entry hata form IV mwenye Divishen four angejaza lakini Hawa sijui wanashahada za Wapi au sijui walifoji vyeti? Ni wa hovyo kabisa.Mama hii mifuko unaiogopa kuifanyia Review (Please amend kipenge Cha fao la kujitoa ) Kuna emergency ya Corona wengi wa Sector ya Utalii tumefukuzwa kazi na hatujalipwa Mafao yetu.
Kuna Swali alijibu Mheshimiwa Majaliwa kutoka kwa mbunge wa Bulaya kuhusu hii mifuko alijibu vizuri lakini hakumalizia kuhusu hiki kipengee Cha fao la kujitoa.
Mheshiwa Spika Tulia aliuliza huwa mnataka Tena particular za mwanachama za Nini wakati mlikuwa mnakata hamkujia Kuna profiles Zina Data Zina miss? Au na Hilo jamani mnataka wataalamu toka nje?Yaani hata Mheshimiwa Tulia angetusaidia ana uchungu na hii Hali siyo wengine hapo wapo kisiasa zaidi.

Kiukweli kikao kijacho Cha Bunge msipotengua hili fao la kujitoa mtamwangusha Mama kwa Asilimia nyingi,yaani hata mkifunga magoli ya mkono wastaafu wa fao la kujitoa Hawatawapigia kura.
Mtupe pesa zetu tulistaafishwa wakati wa Corona hasa sector ya utalii
 
Baada ya kusoma postings zote hapa, nimeona nichangie yafuatayo:

1) Wakulima hawapati Mafao ya Uzeeni kwa sababu hawachangii ktk Mfuko wowote.

Ninaamini Serikali iko katika maandalizi ya kuwafanya waanze kuchangia na hivyo kupata Mafao stahiki.

2) Hakuna aliyesema kuwa Mchango wa Mwajiri siyo stahili ya Mfanyakazi; bali hiyo sheria iliyomlazimisha Mwajiri kuchangia 10% ndiyo yenye Kanuni ya kutokuwa na Mafao ya kukitoa.

Hiwezi kuchukua bipande vya sheria fulani unavyovipenda na kuacha vingine. Kama siyo hiyo sheria mchango wa Mwajiri usingekuwepo.

3) Mchango wa Mwanachama hauwezi kukupa Mkopo kwa ajili ya kijengea nyimba, mtaji wa biashara na kusomeahea watoto au wewe mwenyewe.

Ila ikijipanga vizuri unaweza kutumia 90% unayobaki nayo, pamoja na fursa zingine za mitaji zilizopo kuanzisha biashara.

4) Kama kuna mapungufu ya kibinasamu ya mfanyakazi fulani wa Mfuko wa Hifadi ya jamii, soyo busara kurukia na kusema kuwa fedha za wanachama haziko salama. Hiyo ni generalisation isiyokuwa na busara. Wajenha wanasemanjoyo mo sweeping statement.

5) Suala la kusema “Mimi nipewe pesa zangu tu zote, kitakachotokea baadaye ni jukumu langu, siyo la Serikali” siyo la busara.

Serikali yenye kujalinwatu wake haifanyi kazi namna hiyo kama mambo ya kimtaani.

6) Hoja za watu wengi walioandoka zinaonyesha kuwa hawajui sheria ya hifadhi ya jamii. Wanatumia zaidi hisia na utashi binafsi kusema maneno mengiii ambayo hayana msingi wa sheria au kanuni. Haya siyonrahisinkuzingatiwa na Serikali.

Nashauri watu wazame zaidi katika kuelewa mantiki ya sheria zilizoanzisha mifuko ya hifadhi ya jamii.

Nahitimisha mchango wangu
Hiyo serikali iliyopitisha hii sheria na ilo bunge lililoitunga hii sheria, vipi wao inawahusu?
 
Hakuna fao la kujitoa ktk mifuko ya hifadhi ya jamii duniani kote.
Mifuko hyo ni kwa ajili ya kumlinda mfanyakazi na majanga baada ya kustaafu ndo maana wewe unachangia only 10% ili hali mwajiri nae anaweka 10%.
Kama unataka kujiajiri jiwekezee 10% kwenye kibubu tuone kama utaweza kuwekeza baada ya miaka kumi.

Fao la kujitoa liliwekwa mwaka 1998 wakati wa ushindani kwenye kusaka wanachama kwa kua kulikua na mifuko 5,
Mwaka 2012 liliondolewa kina ZZK wakatetea likabaki kiaina ila ni kinyume na maana ya kuanzishwa mifuko hyo.na mwaka 2018 IRENE ISAKA alilifuta rasmi lakini mwendazake ktk kutafuta sifa akamfukuza kazi nanyi mkachekelea kizuzu.

Hakuna fao la kujitoaaa

Over
Shinyangakwetu!

Wewe matako kweli hujui kitu chochote fao la kujitoa lipo na wafanyakazi wengi tuu walioachishwa kazi ndani ya miezi sita wanapata fao la kukosa ajira na ikifika miezi 18 mingine yaani baada ya kukamilisha jumla ya miezi 24 unapewa fao la kujitoa.

Acha kuwa mpumbafu na kupotosha watu kenge wewe@
 
Mimi Maza nimemkubali Sana ame overhaul vitu vingi Sana.Ila kwenye Mifuko hii Kuna mchawi amemtia maza kwenye kichupa
Sector ya Utalii kwa mfano iliathirika Sana wakati Covid 19 mahoteli mengi yalifungwa na Kuna wengine walistaafishwa ki ulazima,kimbembe chake sasa Mafao yametoka robo na mengine mpaka ufikishe miaka 60.
Kwanza hao Staff wa NSSF naona wao ndo wanauwezo wa kumwagia Maza mchanga machoni na akanawa ,wako very arrogant to the extreme,na hawana utu hata robo yaani Hawa they live in separate entity within Tanzania.
Wanapoteza Documents hovyo .

Particulars za mtu na Data entry hata form IV mwenye Divishen four angejaza lakini Hawa sijui wanashahada za Wapi au sijui walifoji vyeti? Ni wa hovyo kabisa.Mama hii mifuko unaiogopa kuifanyia Review (Please amend kipenge Cha fao la kujitoa ) Kuna emergency ya Corona wengi wa Sector ya Utalii tumefukuzwa kazi na hatujalipwa Mafao yetu.
Kuna Swali alijibu Mheshimiwa Majaliwa kutoka kwa mbunge wa Bulaya kuhusu hii mifuko alijibu vizuri lakini hakumalizia kuhusu hiki kipengee Cha fao la kujitoa.
Mheshiwa Spika Tulia aliuliza huwa mnataka Tena particular za mwanachama za Nini wakati mlikuwa mnakata hamkujia Kuna profiles Zina Data Zina miss? Au na Hilo jamani mnataka wataalamu toka nje?Yaani hata Mheshimiwa Tulia angetusaidia ana uchungu na hii Hali siyo wengine hapo wapo kisiasa zaidi.

Kiukweli kikao kijacho Cha Bunge msipotengua hili fao la kujitoa mtamwangusha Mama kwa Asilimia nyingi,yaani hata mkifunga magoli ya mkono wastaafu wa fao la kujitoa Hawatawapigia kura.
Mtupe pesa zetu tulistaafishwa wakati wa Corona hasa sector ya utalii
Endelea kudhani hizo documents zinapotea kweli

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Fanya kazi ndugu, tutakulipa ukifikia miaka 55 kama sheria ya nchi au hata zile za kimataifa kuhusu pensheni zinavyosema, unajitoa kwenda wapi?
 
Swala la majina ni umbumbumbu wenu, kwanini utumie majina tofauti kila sehemu, benk magufuli,nssf makufuli,rita maghufuli sasa we unaona hayo majina ni moja
Hoja yangu mnapokuwa mnapokea michango ya mhusika mbona hamuulizi usahihi wa majina? Na je ninyi hamna kitengo cha elimu kupita kwenye maofisi yanayoleta michango ili kuondoa tatizo hilo mapema?
Tunaojua,tunaelewa kwamba mnanufaika na umbumbumbu wetu ndo maana hamtoi elimu
Lakini kumbuka yana mwisho ndugu.Kabla hujaajiriwa hiyo nafasi alikalia mtu,jiulize yuko wapi hadi anakuachia unakalia wewe?
Hilo liwe funzo kwako kwamba kuna siku na wewe utaondoka watakaa wengine,na utaenda mtaani kukutana na uliowafanyia ufedhuri.

Siku ya kutoa pesa ndo umbumbu unaonekana?
Haya kuna mtu kalalamikia mnavyodai rushwa wazi wazi kwenye uzi mwingine,unamwambia aweke ushahidi hivi wewe ndo mfanyakazi pekee wa nssf kujibu hoja zate? kuanzia za malipo hadi za rushwa?
Ndugu nakushahuri badilika,unayowafanyia wenzio usipolipwa wewe uwe na uhakika yatawakuta wanao.

Unataka kuniambia na huyu aliyelalamika kuwa mnadai rushwa naye amekosea majina?
na kama amekosea majina ,akitoa rushwa,rushwa inarekebisha vipi jina ili liwe sahihi alipwe stahiki zake?

Niwashauri wafanyakazi wote wanaochangia mifuko hii,muwe na tabia ya kutembelea mifuko hii, ombeni
statement zenu,usisubiri siku ya kustaafu,fuatilia mapema ukutane na nyodo ukiwa bado una nguvu za kukimbizana nao
na kuchukua hatua mapema ili ujue na mahali pa kutoa taarifa unapofanyiwa ndivyo sivyo.
 
Back
Top Bottom