Rais Samia Kumbuka Fao la Kujitoa

Rais Samia Kumbuka Fao la Kujitoa

KUONDOKEWA MAFAO YA KUJITOA NI KWA MANUFAA YA WANACHAMA

Nimesoma yote yaliyoandikwa na wadau na kugundua kwamba wote hawafahamu DHANA YA HIFADHI YA JAMII. Kwa sisi tuliopiya IFM, ninvyema tukatoa elimu kidogo kwa ndani gu zetu ambao hawaelewi vizuri jambo hili. Kwa taarifa, dhana msingi ya Hifadhi ya Jamii ni:-

“Kumfanya mtu kuweka akiba kidogokidogo wakati ana uwezo wa kutengeneza mapato ili akiba hiyo imfae wakati atakapokuwa hana uwezo wa kuzalisha mapato”.

Kwa NSSF, Sheria inamtaka Mwanachama kuchangia 10% tu ya mshahara wake; na Sheria hiyo hiyo inamlazimisha Mwajiri kuchangia 10% ya ziada kukamilisha akiba ya Mwanachama huyo. Kwa maana nyingine, Mwanachama asingepata hiyo 10% ya Mwajiri bila ya Sheria hii.

Akiba hii inapaswa kuendelea kujaziwa kwa kipindi chote cha Mwanachama akiwa na uwezo wa kufanya kazi. Wakati mtu anapochangia 10% ya mshahara wake, anabaki na 90% ya mapato yake. Kudundiliza huku kutaendelea kwa kutumia waajiri mbalimbali atakaofanya nao kazi katika maisha yake.

Kama ni mjasiriamali mzuri, atatumia kiasi kingine kidogo kutoka 90% ili kudunduliza mtaki kwa muda fulani na kuanza biashara. Kama atashindwa kufanya hivyo hadi siku anakosa ajira ndiyo aanze kupambania 10% aliyokuwa anaweka ili aanzisjie biashara, huyo siyo mjasiriamali. Na uwezekano mkubwa ni kwamba hata akizipata hazitamfikisha mbali na itambidi atafute kazi tena ya kuajiriwa.

Sasa wakati akifikia utu uzima na uwezo wa kuchakarika kufanya kazi haupo, ndiyo sasa ataanza kupata pensheni ya kila mwezi hadi mauti yatakapomchukua. Kama aliwahi kuanzisha biashara na ikafanikiwa, maisha yake ya uzeeni yatakuwa mazuri. Kama hakuwahi kuanzisha biashara, basi atakuwa na uhakika wa kupata mahitaji yake muhimu.

Fursa za kuanzisha biashara ziko nyingi tu kwa wajasiriamali waziri. Tukumbuke Bilionea Reginald Mengi alianzisha IPP wakati yeye ni mwajiriwa wa PWC mpaka pale kampuni yake ya IPP ilipokuwa kubwa sana ndipo akaacha kazi. Unaweza ukachangia SACCOS au ikaweka fedha zako Benki na baadae ukachukua mkopo kuanzisha biashara. Kama haya yote huyawezi, kuwa na uhakika hata akiba yako ya NSSF ya 10% haitakusaidia kitu.

Kila mfumo umeanzishwa kwa makusudi yake na taratibu husika lazima zifuatwe. Kama kwa bahati mbaya makusudi haya hatyajui vizuri tuepuke kufanya kosa na kuongea bila elimu na kuanza kuwatukana watu matusi wasiyostahili.

No please, fao la kujitoa lipo kwaajili ya kumlinda mwaajiriwa pale anapo kosa ajira au pale ambapo mwajiri wake amefilisika. Fao la kujitoa ni haki ya mwajiriwa ila awe nje ya ajira. Kwa mfano Mtu amefukuzwa kazi, ameugua kwa mda mrefu au mkataba haujaongezwa kama kwenye sekta binafsi unaenda kwenye Fao la kujitoa kwaajili ya kukulinda kipindi chote ambacho utakosa ajira.

Rais alifikilie hili suala la fao la kujitoa kwa kina, waajiriwa wengi waliokoondolewa kwenye ajira hasa sekta binafsi, wanapata shida huku pesa zao zipo NSSF zinatumika kwenye Mambo ambayo si ya msingi kwa uanzishwajo wa mfuko huo.
 
Lengo la mifuko ya hifadhi ya jamii ni kutatua majanga baada ya kustaafu all over the world.

Sasa kama sisi tanzania ni tofauti lalama utalipwa fao la kujitoa.

Otherwise kimbia nchi

Unafahamu maana ya fao la kujitoa. Yani haupo kwenye mfumo wa ajira lakini michango yako ipo kwenye mfuko. Unachofanya unajitoa kwenye mfuko kwenye kipindi ambacho haupo kwenye ajira kwa kuchukua michango yote. Ukipata ajira utajiunga Tena. Hivyo ndivyo watu walikuwa wanafanya. Kuliko mtu Hana ajira miaka miwili halafu akaunti Kuna milioni ishirini. Please don't impose sanctions on the customer s but provide equity to customers.
 
Miongoni mwa mambo yaliyonifanya niichukie serikali yà awamu ya tano hasa yule dada wa peramiho alivyolishupalia hilo suala.kwanza kulikuwa hakuna haja ya kuanzisha fao la kujitoa pili ulikuwa ungumbaru wa kiwango cha reli kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii leo psssf umechoka imechakaa kazi kutesa wastaafu
Awamu iliyotangulia ilifilisi hiyo mifuko mbaya zaidi iliweka mianya mingi iliyopelekea kufujwa kwa hela za wastaafu hadi kufikia hatua ya hiyo mifuko kushindwa kujiendesha(mfano ; vikao vya menejiment dubai) achana na udini na ukiritimba wa kila namna.

Suluhu pekee kuiokoa ilikuwa kuiunganisha kuepusha mvurugano uliokuwepo .. nakumbuka ilifikia wakati mifuko ilikuwa inashindana kama coka na pepsi

Hoja nyingine: japo kuwa tunaambiwa limefutwa lakini kuna wadau wasio waaminifu wanaendelea kulipa hilo fao la kujitoa huku wakiwatoza wanufaika zaidi ya 40% ya hela wanayoitarajia. Yani .. unakabidhi cash unapewa cheki yako(inaumiza sana!!)
 
Nina jamaa yangu yuko anafia kitandani. Anaumwa sana na matibabu yake yanahitaji hela nyingi. Anapofanya kazi hakuna bima na ni miezi mitatu yuko kitandani kazini kwake wameshasitisha mshahara. Ameomba barua ya kuacha kazi amepewa. Amepeleka NSSF ili alipwe mafao yake eti wanamwambia mpaka atimize miaka sijua 55. Anawambia sina hata uhakik wa kuiona wiki ijayo naombeni mafao yangu yanifae sasa ili nipate matibabu nipone nianze upya lkn wamekataa. Niliumia sana yani jamaa anakufa na hela anayo alaf watarithi na kufaidika wengine.

Walioondoa fao la kujitoa laana hii iwafikie popote walipo
Inaskitisha sana.. akifariki .. wengine ndo watafaidi
 
Waasalam!

Hili ni ombi muhimu sana kwa Rais wetu mpendwa, anairudisha nchi katika muelekeo sahihi basi na sie vijana tulio sekta binafsi ambao tunatamani kujiajiri tunatamani sana fao la kujitoa lirudi ili angalau tupate mtaji wa pa kuanzia.

Sio wote tunatamani kuajiriwa mpaka miaka 55 - 60+ huko, wengine tuna “entrepreneurial spirits” lakini mitaji ndio kikwazo na mifumo ya fedha ya nchi haiamini kuwekeza katika mawazo bunifu, ndio maana wengi tunakubali kuajiriwa kwa miaka 5 - 10 kwa ujira mdogo tuweze kuwekeza kwenye mafao yetu ili baada ya ajira tukaanzishe biashara zetu.

Lilipopitishwa suala la kuzuia fao la kujitoa “kibabe” pasipo kishirikisha wananchi, wengi tuliumia sana kwani mfumo huo unanyima vijana wenye mawazo ya kujiajiri nafasi ya kufanya hivyo na unawalizimisha kuajiriwa kwa maisha yao yote. Mfumo uliopo sasa hivi umetengeneza mwanya mkubwa sana wa rushwa ili mtu kupata hata hicho kiasi kidogo cha fao la kukosa ajira, kama hutoi rushwa utasugua sana soli NSSF na “maafisa” wanakuchora tu, mpaka unakata tamaa.

Tukilazimisha vijana wote kuajiriwa miaka 50+ pasipo kuwa na mbadala wa kufikiria kuanzisha biashara/kujiajiri ni kivipi tutaweza kuanzisha biashara mpya na kuongeza ajira zaidi nchini?

Ushauri wangu ni kurudisha uhuru wa fao la kujitoa ili kama kijana amechoka na ujira mdogo kibaruani, anaweza akajiajiri mwenyewe kwa kuwa tayari ana mtaji wa kuanzia.

Hoja ya kuwa vijana hawa wakizeeka watakua mzigo kwa serikali, inaweza kutazamwa upya kwa kuwndelea kuwawekea vijana hao waliojiri mazingira rafiki ya kuchangia mafao yao wakiwa kama wajasiriamali.

Shukrani.
Itakuw amoja ya mambo mazuri sana kufanywa na Rais. Hizo ni pesa zetu. Ili kudhibiti fujo ya kuzichukua angalau wangeweza kuweka masharti ya miaka ili mtu achukue pesa zake. Mathalani mtu akiamua kuacha kazi, akifikisha miaka 10, 15 au 20 ya utumishi, na pengine asipewe zote bali asilimia kadhaaa mathalani 30% au 50 % lakini kuzishukilia huku watu hawana mitaji ya kufanya ujasiriamali ni wizi
 
Nina jamaa yangu yuko anafia kitandani. Anaumwa sana na matibabu yake yanahitaji hela nyingi. Anapofanya kazi hakuna bima na ni miezi mitatu yuko kitandani kazini kwake wameshasitisha mshahara. Ameomba barua ya kuacha kazi amepewa. Amepeleka NSSF ili alipwe mafao yake eti wanamwambia mpaka atimize miaka sijua 55. Anawambia sina hata uhakik wa kuiona wiki ijayo naombeni mafao yangu yanifae sasa ili nipate matibabu nipone nianze upya lkn wamekataa. Niliumia sana yani jamaa anakufa na hela anayo alaf watarithi na kufaidika wengine.

Walioondoa fao la kujitoa laana hii iwafikie popote walipo
So sad. Mafao ambayo hayawezi kumfaa mtu akiwa na shida
 
Na hao waliofikisha hiyo miaka 60 wakifika ndo wanakwambia jina lako la ukoo lina upungufu wa herufi fulani
unakuta mtu anatembea mpako soli ya kiatu inaisha,wakati kila mwezi mshahara unaletwa kwa majina hayo hayo na hawaulizi wanasubiri ustaafu.
Jambo jingine hasa NSSF unakuta ukiomba statement unapewa unakuta mshimo kibao kama miezi sita n.k
unapewa form umpelekee mwajiri arekebishe,ukipeleka unakuta mwajiri karipa kwa uaminifu ila wao hawajazi.
Ukienda mwaka mwingine unakuta mashimo tena,
Ni kama kuna mchezo mchafu unafanyika,kama sio ni kwa nini unakuta karibia kampuni nzima wote hamjajaziwa,wakati mwajiri anapeleka makato inavyotakiwa?
Sasa fanya uzembe usiende kabisa ukisubiria hiyo miaka sitini ifike
ndo utaelewa ni kwa nini humu wanapiga kelele kuhakikisha fao la kujitoa halirudishwi.
Nahisi kuna watumishi wasiowaminifu zile pesa wanajikopa. Ndio maana hawaziingizi mpaka ukapige kelele
 
Leo hii nimeona clip whatsap ya mh.mbunge msukuma ikisema "Mtu mnaongea anakuambia habari za masters,n.k mwisho wa mazungumzo anakuomba buku kumi...'' mwisho wa kunukuu
hivi watu wote wanaoshtakiwa kwa kutumia ofisi zao vibaya wote hawajaenda shule?
Kama wameenda shule,imewasaidiaje,mbona niwezi kuliko wasiosoma?
Hapa namaanisha,mliosoma msifikirie wasiosoma ni mbumbumbu,kiasi
kwamba unaweza kufanya yasiyofaa kwa kuwadanganya kwamba ni usomi wakakuelewa.

Sasa nikuulize,tulionufaika na fao hilo la kujitoa miaka hiyo ya nyuma,
inamaana waliokuwa wanaendesha mifuko hiyo hawakuwa na uelewa wa kutosha
wa kuendesha mifuko hiyo? kama jibu ni ndiyo,effect yake kwa sasa ni kiasi gani?
mbona tunaona wazee na watu wa makamo wana maisha mazuri,na sheria iliwaruhusu
wakachukua fedha zao pindi walipotaka.

Nimeishasema hapo juu,na niseme tena kuwa asilimia kumi
anayokuchangia mwajiri siyo hisani,sheria inamtaka afanye hivyo kama mimi
inavyonitaka nilipe PAYE na nisipolipa ni kosa kisheria.Na mimi kama mwajiriwa nina wajibu wa kutimiza ili anichangie hiyo 10%
nisipofanyakazi kiwanda kikafungwa hawezi kunichangia kutoka kwenye akiba yake binafsi.Sasa huu ujasiri wa kusema mwajiliwa fedha ya kwake ni 10% mnaupata wapi? Ndo maana nilimpongeza Magu alipomfukuza yule mama aliyekuwa anakomaa na hoja hii
Sijui kwanini mnaoitwa wasomi hamlioni hili?
wasomi matapeli ndio aina yao.
 
Mfano, mtu anafanya kazi ya Ulinzi au vibarua migodini na viwandani?

Kwahiyo, kwa AKILI zenu nzito huyo mtu atafanya kazi mpaka kufikisha miaka 60 ili muanze kumpa pension?

Kama pension Ni kitu muhimu hivyo, mbona hata hao wanaostahili tunaona wanahangaika tu kupata pesa zao?

Mbina wastafu hali zao Ni tete vile vile?
Pesa yako ni ile uliyonayo. Tumbua pesa zako mwenyewe. Nje ya hapo ni ujanja ujanja wa serikali zetu za Afrika
 
Waasalam!

Hili ni ombi muhimu sana kwa Rais wetu mpendwa, anairudisha nchi katika muelekeo sahihi basi na sie vijana tulio sekta binafsi ambao tunatamani kujiajiri tunatamani sana fao la kujitoa lirudi ili angalau tupate mtaji wa pa kuanzia.

Sio wote tunatamani kuajiriwa mpaka miaka 55 - 60+ huko, wengine tuna “entrepreneurial spirits” lakini mitaji ndio kikwazo na mifumo ya fedha ya nchi haiamini kuwekeza katika mawazo bunifu, ndio maana wengi tunakubali kuajiriwa kwa miaka 5 - 10 kwa ujira mdogo tuweze kuwekeza kwenye mafao yetu ili baada ya ajira tukaanzishe biashara zetu.

Lilipopitishwa suala la kuzuia fao la kujitoa “kibabe” pasipo kishirikisha wananchi, wengi tuliumia sana kwani mfumo huo unanyima vijana wenye mawazo ya kujiajiri nafasi ya kufanya hivyo na unawalizimisha kuajiriwa kwa maisha yao yote. Mfumo uliopo sasa hivi umetengeneza mwanya mkubwa sana wa rushwa ili mtu kupata hata hicho kiasi kidogo cha fao la kukosa ajira, kama hutoi rushwa utasugua sana soli NSSF na “maafisa” wanakuchora tu, mpaka unakata tamaa.

Tukilazimisha vijana wote kuajiriwa miaka 50+ pasipo kuwa na mbadala wa kufikiria kuanzisha biashara/kujiajiri ni kivipi tutaweza kuanzisha biashara mpya na kuongeza ajira zaidi nchini?

Ushauri wangu ni kurudisha uhuru wa fao la kujitoa ili kama kijana amechoka na ujira mdogo kibaruani, anaweza akajiajiri mwenyewe kwa kuwa tayari ana mtaji wa kuanzia.

Hoja ya kuwa vijana hawa wakizeeka watakua mzigo kwa serikali, inaweza kutazamwa upya kwa kuwndelea kuwawekea vijana hao waliojiri mazingira rafiki ya kuchangia mafao yao wakiwa kama wajasiriamali.

Shukrani.
Pointi
 
Sitashangaa Awamu ya 5 ikihusishwa kwenye hili...
Japo walilikuta!
Awamu zaccm ndo zimetufikisha hapa. Zijaribu kututoa.
Awamu ya 5 walikuwa na fursa ya kulikataa but walilikoroga vibaya sana.
 
Hakuna fao la kujitoa ktk mifuko ya hifadhi ya jamii duniani kote.
Mifuko hyo ni kwa ajili ya kumlinda mfanyakazi na majanga baada ya kustaafu ndo maana wewe unachangia only 10% ili hali mwajiri nae anaweka 10%.
Kama unataka kujiajiri jiwekezee 10% kwenye kibubu tuone kama utaweza kuwekeza baada ya miaka kumi.

Fao la kujitoa liliwekwa mwaka 1998 wakati wa ushindani kwenye kusaka wanachama kwa kua kulikua na mifuko 5,
Mwaka 2012 liliondolewa kina ZZK wakatetea likabaki kiaina ila ni kinyume na maana ya kuanzishwa mifuko hyo.na mwaka 2018 IRENE ISAKA alilifuta rasmi lakini mwendazake ktk kutafuta sifa akamfukuza kazi nanyi mkachekelea kizuzu.

Hakuna fao la kujitoaaa

Over
Suala kustaafu ni suala binafsi na hiyari ya mtu.
Tunajua Duniani kote serikali zote ni za wizi mtupu.
Ila inasikitisha sana kama Kuna mwananchi mmoja anasupport wizi wa serikali
 
Waasalam!

Hili ni ombi muhimu sana kwa Rais wetu mpendwa, anairudisha nchi katika muelekeo sahihi basi na sie vijana tulio sekta binafsi ambao tunatamani kujiajiri tunatamani sana fao la kujitoa lirudi ili angalau tupate mtaji wa pa kuanzia.

Sio wote tunatamani kuajiriwa mpaka miaka 55 - 60+ huko, wengine tuna “entrepreneurial spirits” lakini mitaji ndio kikwazo na mifumo ya fedha ya nchi haiamini kuwekeza katika mawazo bunifu, ndio maana wengi tunakubali kuajiriwa kwa miaka 5 - 10 kwa ujira mdogo tuweze kuwekeza kwenye mafao yetu ili baada ya ajira tukaanzishe biashara zetu.

Lilipopitishwa suala la kuzuia fao la kujitoa “kibabe” pasipo kishirikisha wananchi, wengi tuliumia sana kwani mfumo huo unanyima vijana wenye mawazo ya kujiajiri nafasi ya kufanya hivyo na unawalizimisha kuajiriwa kwa maisha yao yote. Mfumo uliopo sasa hivi umetengeneza mwanya mkubwa sana wa rushwa ili mtu kupata hata hicho kiasi kidogo cha fao la kukosa ajira, kama hutoi rushwa utasugua sana soli NSSF na “maafisa” wanakuchora tu, mpaka unakata tamaa.

Tukilazimisha vijana wote kuajiriwa miaka 50+ pasipo kuwa na mbadala wa kufikiria kuanzisha biashara/kujiajiri ni kivipi tutaweza kuanzisha biashara mpya na kuongeza ajira zaidi nchini?

Ushauri wangu ni kurudisha uhuru wa fao la kujitoa ili kama kijana amechoka na ujira mdogo kibaruani, anaweza akajiajiri mwenyewe kwa kuwa tayari ana mtaji wa kuanzia.

Hoja ya kuwa vijana hawa wakizeeka watakua mzigo kwa serikali, inaweza kutazamwa upya kwa kuwndelea kuwawekea vijana hao waliojiri mazingira rafiki ya kuchangia mafao yao wakiwa kama wajasiriamali.

Shukrani.

Asante sana kwa hili jambo! Mama anajua ila anatenda kupitia waziri husika, tatizo ni huyo waziri sidhani hata IQ yake inaweza analytics za kujistify umuhimu wa fao hilo! She is more of praise and worship yule mwalimu ….Pale waziri hatuna !
 
Hili FAO lingetusaidia sana
Yaan ukichoka kufanya kazi za kuajiriwa unapisha wanakuja wengine wewe unaenda zako kulima mboga mboga
Mafao ya kujitoa ndiyo kiswahili sahihi hii ya fao siyo japo wanàsiasa wanashadidia sana
 
Ila babu hapana kwa kweli[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimecheka sana aisee[emoji119][emoji119]
Afu ulinipigia au ulibeep?
 
Hili FAO lingetusaidia sana
Yaan ukichoka kufanya kazi za kuajiriwa unapisha wanakuja wengine wewe unaenda zako kulima mboga mboga
Mafao ya kujitoa ndiyo kiswahili sahihi hii ya fao siyo japo wanàsiasa wanashadidia sana
Mkuu una uhakika wingi wa fao ni mafao?
Na kwa muktadha wa psssf hiyo ni kati ya product nyingi wanapotea kwa clients wao
 
Vipi pia wale sekta binafsi tuliokuwa LAPF tukahamishiwa NSSF. Kuna mwenye updates yoyote huko?.. Maana huwa hawaeleweki kama hela zitahamishiwa NSSF au la.

Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ndugu sikiliza, nimefanya kazi miaka 5 kwa mfano Kampuni B,baada ya hapo Kampuni imekufa,NSSF watakomaaje na Mafao yangu??wao wanipe nikapambane na mambo yangu mtaani,hata nikizi-mis-use wao haiwahusu!!na kimsingi sina Mkataba na Mungu kwamba nitafikisha miaka 60 ili nianze kupewa Pension,huo ndio uungwana
Shida watu wanapigia hesabu pesa ambazo sio zao. Ubinafsi unawapiga upofu hata wasione taabu za wanachama.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom