Unko T
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 200
- 266
Waasalam!
Hili ni ombi muhimu sana kwa Rais wetu mpendwa, anairudisha nchi katika muelekeo sahihi basi na sie vijana tulio sekta binafsi ambao tunatamani kujiajiri tunatamani sana fao la kujitoa lirudi ili angalau tupate mtaji wa pa kuanzia.
Sio wote tunatamani kuajiriwa mpaka miaka 55 - 60+ huko, wengine tuna “entrepreneurial spirits” lakini mitaji ndio kikwazo na mifumo ya fedha ya nchi haiamini kuwekeza katika mawazo bunifu, ndio maana wengi tunakubali kuajiriwa kwa miaka 5 - 10 kwa ujira mdogo tuweze kuwekeza kwenye mafao yetu ili baada ya ajira tukaanzishe biashara zetu.
Lilipopitishwa suala la kuzuia fao la kujitoa “kibabe” pasipo kishirikisha wananchi, wengi tuliumia sana kwani mfumo huo unanyima vijana wenye mawazo ya kujiajiri nafasi ya kufanya hivyo na unawalizimisha kuajiriwa kwa maisha yao yote. Mfumo uliopo sasa hivi umetengeneza mwanya mkubwa sana wa rushwa ili mtu kupata hata hicho kiasi kidogo cha fao la kukosa ajira, kama hutoi rushwa utasugua sana soli NSSF na “maafisa” wanakuchora tu, mpaka unakata tamaa.
Tukilazimisha vijana wote kuajiriwa miaka 50+ pasipo kuwa na mbadala wa kufikiria kuanzisha biashara/kujiajiri ni kivipi tutaweza kuanzisha biashara mpya na kuongeza ajira zaidi nchini?
Ushauri wangu ni kurudisha uhuru wa fao la kujitoa ili kama kijana amechoka na ujira mdogo kibaruani, anaweza akajiajiri mwenyewe kwa kuwa tayari ana mtaji wa kuanzia.
Hoja ya kuwa vijana hawa wakizeeka watakua mzigo kwa serikali, inaweza kutazamwa upya kwa kuwndelea kuwawekea vijana hao waliojiri mazingira rafiki ya kuchangia mafao yao wakiwa kama wajasiriamali.
Shukrani.