Fao la kujitoa haki itendeke

Justine Marack

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
567
1,551
Katika mambo yaliyoleta Ukakasi katika awamu iliyopita ni pamoja na hili LA FAO LA kujitoa. Hapo awali ilikua ni haki ya mtu kuamua muajiriwa au la.

Kwa Sababu yoyote mtu aliweza kuamua kutumia haki yake kupanga namna halali ya kupata riziki yake kihalali.
Na kwa waliokua watumishi wa umma au mashirika waliweza kacha kazi na kufanya kilimo au biashara. FAO la kujitoa lilitumika kama Mtaji katika kazi mpya ya ujasiriamali na kilimo. Sasa wakati ilipobadilishwa sheria, Fao hili likaondolewa na kifinyangwa kwa namna ambayo iliminya haki za watu kutumia pesa zao.

Serikali ilitoa hoja dhaifu sana, ikionesha kuwa inajali mustakabali wa watumishi, ikalazimisha mtu akiacha kazi spate pesa take mpaka afikapo miaka 50. Inajulikana kuna watu wengi ambao serikali haijasema inawajali vipi kwa kuwapa hiyo hifanya ya uzeeni. Watu wasio katika ajira rasmi hakuna namna serikali imeonesha kuwasaidia kwa huruma hiyo.

Sasa inakuwaje mtu nyimwe pesa yake? Ni wakati sasa Fao la kujitoa litolewe bila masharti. Hii itaongeza ajira kwani wano acha kazi wataacha nafasi wazi na huko wanako kwenda watatengeneza ajira na kuajiri wengine
 
Naunga mkono hoja watu walipwe ..Yule mungu mtu hakuwa binadam wa kawada...kufuata nyayo zake ni kumtukuza shetani
 
Back
Top Bottom