Rais Samia: Hatutazuia Maandamano na Mikutano ya Hadhara

Rais Samia: Hatutazuia Maandamano na Mikutano ya Hadhara

Ukweli maandamano yanayokuwa na impact kwangu naona ni yale yanayofanyika non stop, haya yanaendelea kwa muda kuilazimisha serikali itoe tamko, mpaka imafika baadhi ya shughuli zinakuwa hazifanyiki kama ilivyo kawaida.

Hapo serikali ikianza kupoteza mapato kutokana na shughuli za kiuchumi kusimama, au kuvurugwa kwa ratiba zake, ndio serikali itaanza kupata akili. Lakini sio kwa haya maandamano ya kila baada ya wiki mmoja, tena kwa jiji moja - No. Mwisho wake yanageuka ya kufurahia "nyomi" tu.

Kwangu ningependa haya maandamano yafanyike kama ni siku moja, kwa miji yote au majiji yote nchini, hapo Chadema wapeleke kiongozi wao mmoja kila mkoa kuongoza. Lakini sio kwa hivi sasa yanavyofanyika ni kama vile unawachoma sindano, kisha unawapa muda wapoze maumivu, ndio maana Samia anasema waache waandamane weee.. wanajua watapewa muda wapoe.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Viongozi wa CHADEMA wamesema Maandamano haya yataenda kwa Awamu yataanzia Miji mikubwa ili kujenga Confidence na kuwaondoa UOGA Watanzania waliokuwa Wametuwa UOGA na Serikali ya Magufuli.

Awamu ya pili itakuwa ni Nchi nzima na Migomo itafuatia.

360_F_580067370_E4BWDcJ2Da8UKPIc7I3iheF031KXoSu9.jpg

Ngoja yachemke tumuone Bibie Chura akisema Yarabi Nafa!...
 
Tunataka Raisi anaeheshimu Katiba na anaeona MAPUNGUFU ya hii Katiba ya sasa.

Tufanye mabadiliko madogo ya Katiba hii ili tupate TUME HURU YA UCHAGUZI halafu atupe TAREHE ya kuanza MCHAKATO WA KATIBA MPYA.

Hana haja ya KUWAOGOPA WAHAFIDHINA WA CCM.

Akifanya the righ thing tutamuunga mkono.
check hili huku limepewa lift siti ya mbele linataka kujipiga mihoni litakavyo 🐒
 
Rais Samia amesema serikali yake haitazuia Maandamano ya Vyama vya Siasa kwani Hiyo ndio demokrasia.

Vyama vya Upinzani vitaendelea kuruhusiwa kufanya Maandamano na Mikutano ya hadhara.

===


Kuhusu siasa Samia amesema, “Uhuru wa kujieleza na kumasisha siasa za ustarabu zenye kulenga kuleta maendeleo ya watu, tunasisitiza kustamiliana na kuzingatia sheria, siasa zetu kisiwe chanzo cha tafruku au machafuko”

"Vyama vya siasa vinafanya shuguli zao kwa uhuru kabisa, wanaotaka kuaadamana tunawambia ingia barabarani tutawalinda”

Ameeleza kuwa maandamano au kujieleza vyama vya siasa zinaendelea na shughuli zao na wanaendelea kuhamasisha uhuru wa watu kufanya siasa zao.

---
“Vyama vya siasa vinaendelea kufanya shughuli zao kwa uhuru kabisa, wanaotaka kuandamana tunawaambia ingieni barabarani tutawalinda, wanakwenda weee mpaka wakichoka wanakokwenda wanafika wanafanya yao haya tawanyikeni wanatawanyika, wanaotaka sijui kufanyaje tunawaruhusu, Mtu anatamani kusema tunamwambia kiwanja hiki hapa jukwaa hili, anasema weee akimaliza tunamwambia shuka Baba nenda zako anaenda zake”

“Kwahiyo tunaendelea kutoa uhuru kwa Watu kufanya siasa zao, kuna yale mazoea ya muda mrefu ya siasa za madaraka, kupakana matope na kuzushiana kama zilivyosemwa hapa bado zipo hatukatai bado zipo na nadhani mnazisikia Watu fulani wakisimama hivyo lakini tunaendelea ku-manage”

“Taifa sasa hivi lina Mama na Mama kazi yake kulea, kustahimili na kuhakikisha nyumba ina usalama, kwahiyo Mama yupo katika nafasi ya juu ya Taifa, tutegemee Taifa liendelee kutulia zaidi, jitihada zetu za kuimarisha misingi ya utawala na sheria zinaendelea kutambulika kote Ulimwenguni”
Katika hili, mama amepata sapoti yangu 100%
 
Viongozi wa CHADEMA wamesema Maandamano haya yataenda kwa Awamu yataanzia Miji mikubwa ili kujenga Confidence na kuwaondoa UOGA Watanzania waliokuwa Wametuwa UOGA na Serikali ya Magufuli.

Awamu ya pili itakuwa ni Nchi nzima na Migomo itafuatia.

View attachment 2920216
Ngoja yachemke tumuone Bibie Chura akisema Yarabi Nafa!...
Kwanini kumuogopa Magufuli aliyefariki mpaka leo?.

Mimi nachotaka kifanyike, hayo maandamano sasa yaanze kufanyika kwenye miji mingi kwa siku moja, ili tupime impact kwa ujumla wake kutoka maeneo tofauti kwa siku moja.

Lakini sio kwa mtindo huu wa sasa, yanaenda kugeuka kuwa kama "kili marathon" kwa wale wa mwendo mfupi wenye vitambi wanaotembea kwa miguu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Tunakushukuru mheshimiwa rais, kila mtu afanye kinachompa amani moyoni,
Tunaomba hata siku ya kupiga kura nayo iwe huru,nashauri safari hii
hata mabegi yapigwe marufuku kama ilivyo sare za vyama kwenye kituo cha kupiga kura.
 
Wakubwa wa ulaya na magaribi wamewabana gov officials....ni mwendo wa demokrasia tu hapa..........


Wrong thought , Hao ulaya na Magaribi wanafurahia serikali hizi za demokrasia ya kudanganyana na kutumia nguvu kwani wao hufaidika sana na watu kama hawa
 
Ukweli maandamano yanayokuwa na impact kwangu naona ni yale yanayofanyika non stop, haya yanaendelea kwa muda kuilazimisha serikali itoe tamko, mpaka inafikia wakati baadhi ya shughuli zinakuwa hazifanyiki kama ilivyo kawaida.

Hapo serikali ikianza kupoteza mapato kutokana na shughuli za kiuchumi kusimama, au kuvurugwa kwa ratiba zake, ndio serikali itaanza kupata akili. Lakini sio kwa haya maandamano ya kila baada ya wiki mmoja, tena kwa jiji moja - No. Mwisho wake yanageuka ya kufurahia "nyomi" tu.

Kwangu ningependa haya maandamano yafanyike kama ni siku moja, kwa miji yote au majiji yote nchini, hapo Chadema wapeleke kiongozi wao mmoja kila mkoa kuongoza.

Lakini sio kwa hivi sasa yanavyofanyika, naona ni kama vile unawachoma sindano, kisha unawapa muda wapoze maumivu, ndio maana Samia anasema waache waandamane weee.. wanajua watapewa muda wapoe.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kwahiyo mkivumiliwa na kupewa uhuru mnataka kuvuka mipaka?

Poleni sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom