Rais Samia: Hatutazuia Maandamano na Mikutano ya Hadhara

Rais Samia: Hatutazuia Maandamano na Mikutano ya Hadhara

Kwa wale tuliosomea Polical Science Rais Samia anaviua Vyama vya upinzani hususan Chadema. Ukiambiwa "andamaneni weeee na tutawalinda " ni kauli sawa na "we bwabwaja weeee mwisho utaenda kulala". Hii ni hatari. Ni kupuuzwa.
Duuu, kama ni hivyo kwenye nchi zote wanakoandamana kwa amani kusingekuwa na chama chochote Cha upinzani.
 
sio wadanganyika , ni mijoga , Kamanda Sirro akijamba wote wanaingia mivunguni kama kunguni 😛😛😛😛
Never say never.
Binadamu aliye hai si wa kumkatia tamaa.

Watanzania walioitwa "maiti" na "JK wa Kenya" miaka ile, sio hawa wa leo,japo wamebaki wachache walio chini ya chama cha mambuzi.
 
Kwa wale tuliosomea Polical Science Rais Samia anaviua Vyama vya upinzani hususan Chadema. Ukiambiwa "andamaneni weeee na tutawalinda " ni kauli sawa na "we bwabwaja weeee mwisho utaenda kulala". Hii ni hatari. Ni kupuuzwa.
Ninyi ndio Mathink Tank wa CCM? Taifa limekula Hasara.
 
Kwa wale tuliosomea Polical Science Rais Samia anaviua Vyama vya upinzani hususan Chadema. Ukiambiwa "andamaneni weeee na tutawalinda " ni kauli sawa na "we bwabwaja weeee mwisho utaenda kulala". Hii ni hatari. Ni kupuuzwa.
Hata nami nimehisi hili jambo, hiyo kauli ya "acha waandamane weee.." imenifikirisha.

Imenifikirisha kwasababu mpaka sasa bado sijaskia tamko la serikali kuhusu hatua wanazochukua kupambana na ugumu wa maisha kwa watanzania, licha ya kwamba hilo kuwa ndio lengo kuu la maandamano/ waandamanaji.

Huyu mama ni kama vile anachukulia vitu simple ilimradi aioneshe jumuia ya kimataifa kwamba Tanzania sasa inapiga hatua kwenye demokrasia ya kweli, wapate misaada, maisha yao yaende.

Lakini kwa upande wa ndani, sioni kama serikali ipo makini sana na kile kinachopiganiwa kwenye maandamano.

Hapa lazima waandamanaji kwa hiyo kauli sasa wajiongeze, wajue ni njia gani mbadala wataitumia kuwashtua hawa wanaoonesha hawana habari na maandamano yanayoendelea huku bara.

Kwa hiyo kauli yake Samia ni kama vile amesema; "waache waandamane hao mchana, usiku watalala". Inaendana na ile kauli ya JK; "kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala"!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Duuu, kama ni hivyo kwenye nchi zote wanakoandamana kwa amani kusingekuwa na chama chochote Cha upinzani.
Inategemea ni aina gani ya maandamano mkuu. Haya ya CHADEMA ni kama matembezi tu ya hisani. Maandamano yenye impact kiufupi ni yale yenye fujo kidogo,kias kwamba mtawala hatulii ofisini..inamlazimu atafute suluhu.
 
Rais Samia amesema serikali yake haitazuia Maandamano ya Vyama vya Siasa kwani Hiyo ndio demokrasia.

Vyama vya Upinzani vitaendelea kuruhusiwa kufanya Maandamano na Mikutano ya hadhara.

===


Kuhusu siasa Samia amesema, “Uhuru wa kujieleza na kumasisha siasa za ustarabu zenye kulenga kuleta maendeleo ya watu, tunasisitiza kustamiliana na kuzingatia sheria, siasa zetu kisiwe chanzo cha tafruku au machafuko”

"Vyama vya siasa vinafanya shuguli zao kwa uhuru kabisa, wanaotaka kuaadamana tunawambia ingia barabarani tutawalinda”

Ameeleza kuwa maandamano au kujieleza vyama vya siasa zinaendelea na shughuli zao na wanaendelea kuhamasisha uhuru wa watu kufanya siasa zao.

---
“Vyama vya siasa vinaendelea kufanya shughuli zao kwa uhuru kabisa, wanaotaka kuandamana tunawaambia ingieni barabarani tutawalinda, wanakwenda weee mpaka wakichoka wanakokwenda wanafika wanafanya yao haya tawanyikeni wanatawanyika, wanaotaka sijui kufanyaje tunawaruhusu, Mtu anatamani kusema tunamwambia kiwanja hiki hapa jukwaa hili, anasema weee akimaliza tunamwambia shuka Baba nenda zako anaenda zake”

“Kwahiyo tunaendelea kutoa uhuru kwa Watu kufanya siasa zao, kuna yale mazoea ya muda mrefu ya siasa za madaraka, kupakana matope na kuzushiana kama zilivyosemwa hapa bado zipo hatukatai bado zipo na nadhani mnazisikia Watu fulani wakisimama hivyo lakini tunaendelea ku-manage”

“Taifa sasa hivi lina Mama na Mama kazi yake kulea, kustahimili na kuhakikisha nyumba ina usalama, kwahiyo Mama yupo katika nafasi ya juu ya Taifa, tutegemee Taifa liendelee kutulia zaidi, jitihada zetu za kuimarisha misingi ya utawala na sheria zinaendelea kutambulika kote Ulimwenguni”
Wewe jamaa unaanza kuboa. Tunataka kujua aliyasema wapi na lini!
 
"acha waandamane weee.."
Hata Chura alisemaga "acha waongeze Gesi weee..."
e2a5be_08275c62602747aab331e59742649313.jpg
 
Kwa wale tuliosomea Polical Science Rais Samia anaviua Vyama vya upinzani hususan Chadema. Ukiambiwa "andamaneni weeee na tutawalinda " ni kauli sawa na "we bwabwaja weeee mwisho utaenda kulala". Hii ni hatari. Ni kupuuzwa.
wanachadome hawajui hiloo
 
Hii ni dharau kubwa sana kwa Chadema yani maandamano yameruhusiwa lakini yamejaa dharau kwamba andamaneni lakini hatubadilishi chochote yaleyale utaongea mchana we usiku utanyamanza na kulala😁😁😁😁

Chadema mmechambwa in a way...poleni sana
 
Kwa wale tuliosomea Polical Science Rais Samia anaviua Vyama vya upinzani hususan Chadema. Ukiambiwa "andamaneni weeee na tutawalinda " ni kauli sawa na "we bwabwaja weeee mwisho utaenda kulala". Hii ni hatari. Ni kupuuzwa.
Kwa Hamasa ile ya watu hapo political science Ina kudanganya. Sisi wengine tunasema success brings success. Mafanikio ya maandamano hayo ni chachu na hamasa kwa wananchi wengi kusikiliza hoja za chadema.
 
Kwa wale tuliosomea Polical Science Rais Samia anaviua Vyama vya upinzani hususan Chadema. Ukiambiwa "andamaneni weeee na tutawalinda " ni kauli sawa na "we bwabwaja weeee mwisho utaenda kulala". Hii ni hatari. Ni kupuuzwa.
Unapotosha kauli ya Rais. Je, unajua madhara yake?
 
HALI HII INAMKINZA SANA LISSU, MAANA ANGEPENDA YAZUIWE WATU WAPIGWE MABOMU ILI VIBALI VYAKE VIPATE VALIDITY YA UKIMBIZI, MH. SSH, UMAWAWEZA MNO WAHUNI HAWA!
---VURUGU NI FAIDA, VURUGU NI MTAJI - - -
Kwa hiyo magufuli alishindwa sio?
 
Sasa kwa nini alipoingia madarakani naye alisema hakuna mikutano ya kisiasa mpaka ashughulikie uchumi kwanza?

Anasahau maneno yake mwenyewe?
Swala la uchumi aliisha limaliza
Andamaneni atawalinda na baada ya uchaguzi muandamane kupinga matokeo atawalinda.
 
Hata Chura alisemaga "acha waongeze Gesi weee..."
View attachment 2920202
Ukweli maandamano yanayokuwa na impact kwangu naona ni yale yanayofanyika non stop, haya yanaendelea kwa muda kuilazimisha serikali itoe tamko, mpaka inafikia wakati baadhi ya shughuli zinakuwa hazifanyiki kama ilivyo kawaida.

Hapo serikali ikianza kupoteza mapato kutokana na shughuli za kiuchumi kusimama, au kuvurugwa kwa ratiba zake, ndio serikali itaanza kupata akili. Lakini sio kwa haya maandamano ya kila baada ya wiki mmoja, tena kwa jiji moja - No. Mwisho wake yanageuka ya kufurahia "nyomi" tu.

Kwangu ningependa haya maandamano yafanyike kama ni siku moja, kwa miji yote au majiji yote nchini, hapo Chadema wapeleke kiongozi wao mmoja kila mkoa kuongoza.

Lakini sio kwa hivi sasa yanavyofanyika, naona ni kama vile unawachoma sindano, kisha unawapa muda wapoze maumivu, ndio maana Samia anasema waache waandamane weee.. wanajua watapewa muda wapoe.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kwa wale tuliosomea Polical Science Rais Samia anaviua Vyama vya upinzani hususan Chadema. Ukiambiwa "andamaneni weeee na tutawalinda " ni kauli sawa na "we bwabwaja weeee mwisho utaenda kulala". Hii ni hatari. Ni kupuuzwa.
Kwa hiyo badala yake wafanyaje kusukuma ajenda zao. Be objective
 
Haki ya Kuongea vipi Kusikilizwa ? Siongelei vyama vya Siasa bali wananchi kitaa waliopigika....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom