Rais Samia azindua Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
Rais Samia anafungua hotel ya kisasa mkoani Arusha iitwayo Gran Melia na tukio liko mubashara ITV, TBC na Channel ten.

Karibuni sana.

=====

Rais Samia Suluhu amezindua rasmi hoteli ya kisasa ya nyota tano Gran Melia Arusha, huku akialika wawekezaji zaidi kwenye sekta ya Utalii nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo Novemba 22,2021 jijini Arusha, Rais Samia amesema Tanzania ni eneo bora la kuwekeza kutoka na kuwa vivutio vingi vya utalii huku ikitenga asilimia 32.5 ya ardhi katika uhifadhi na utalii.

Amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji na akawaalika taasisi ya Albwardy ambao ndio wamiliki wa hoteli kuwekeza zaidi hapa nchini.

Amesema Tanzania ni salama na hata kipindi hiki cha janga la uviko-19 imekuwa salama kutokana na kuzingatia tahadhari zote za kupambana na uviko-19.

Rais amesema miongoni mwa tahadhari hizo ni kuchanja ambapo yeye binafsi alizindua zoezi hilo mwezi Julai kwa kupata chanjo.

"Tanzani ni salama tunawakaribisha kuwekeza na kutembelea na mtaondoka salama"amesema

Amesema kutokana na Tanzania kuzingatia viwango vya kupambana ma uviko-19 imepewa tuzo kadhaa na mashirika ya kimataifa ya utalii na kutajwa kama kituo salama.cha kutalii.

Amesema pia hifadhi za Taifa ikiwapo Serengeti imeendelea kupata tuzo kama hifadhi bora zaidi Afrika 2020 na awali pamoja na hifadhi ya Ngorongoro na mlima Kilimanjaro zilipata tuzo ya hifadhi bora na miomgoni mwa maeneo ya maajabu ya asili barani Afrika .

Awali Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Damas Ndumbaro aliwapongeza Gran Melia kwa kiwekeza nchini hotel 6 za kitalii na kufanya Tanzania miongoni mwa nchi 40 ambazo kampuni hiyo imewekeza hoteli 350.

Hata hivyo ameomba kampuni hiyo kuwekeza hoteli nyingine tatu na kufanya ziwe tisa kama ilivyo katika nchi nyingine.

Mwenyekiti wa hoteli hizo, Ally Albwardy alishukuru serikali ya Tanzani kwa kusaidia iweze kuwekeza hapa nchini.

Amesema kwa sasa wafanyakazi 800 wameajiriwa katika hoteli za zao huku akiahidi kutoa huduma bora za hadhi ya nyota tano.

Chanzo: Mwananchi

======

1-20-1024x976.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifuta Kamba kuondoa kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha (Picha: Ikulu)

2-17-1024x626.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuashiria kuzinduzi rasmi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha leo tarehe 22 Novemba 2021. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Uwekezaji wa AlBwarddy Mhe. Ali AlBwardy, wa pili kulia Ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Damas Ndumbaro. (Picha: Ikulu)

7-8-1024x957.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mwenyekiti wa Uwekezaji wa AlBwarddy Mhe. Ali AlBwardy na baadhi ya Viongozi mbalimbali baada ya kuzinduzi rasmi Gran Melia Hotel Jijini Arusha. (Picha: Ikulu)
 
Tunahitaji watalii.

Tunazihitaji fedha zao.

Kazi ya serikali ni kuitia shime kiwasaa sekta binafsi.

#Siempre JMT
 
Back
Top Bottom