Rais Samia aunda kamati kutathmini utendaji kazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda Kamati kwa ajili ya kutathmini utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kuiwezesha Wizara hiyo kutekeleza malengo ya Serikali katika kukuza diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa.

Ili kutekeleza azma hiyo amemteua Balozi Yahya Simba, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia kuwa Mwenyekiti wa Kamati.

Aidha, amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati:
1) Balozi Ramadhan Mwombe Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mstaafu;

2) Balozi Dkt. Mwanaidi Sinare Maajar, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza;

3) Balozi Peter Allan Kallaghe, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza;

4) Balozi Tovako Nathaniel Manongi, aliyekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa New York, Marekani.

Kamati hiyo itazinduliwa rasmi tarehe 31 Machi, 2023 Ikulu Dar es Salaam, saa 08:30 mchana.

FsVPnA1XwAAarO4.jpeg
 
View attachment 2569232
Kwani TISS hawawezi kufanya hiyo kazi?
 
Ni jambo jema

Nilidhani Taifa stars
Hapana.

Mi naomba kukuuliza kwa uzoefu wako, kwa sababu unao uzoefu wa muda kitambo; chimbua na huko kwenye historia ya nchi hii.
Je, uliwahi kusikia kuundwa kwa kamati kutathmini kazi za wizara yoyote hapa nchini?

Ukishafanya hivyo, tutajadili hili jipya, manufaa yake au kukosa manufaa. Lakini mimi naanza na kushauri Zanzibar wapewe wizara yao ya Mambo ya nje. Halafu tufunge kazi. Upuuzi umekuwa mwingi mno sasa.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda Kamati kwa ajili ya kutathmini utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kuiwezesha Wizara hiyo kutekeleza malengo ya Serikali katika kukuza diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa.

Ili kutekeleza azma hiyo amemteua Balozi Yahya Simba, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia kuwa Mwenyekiti wa Kamati.

Aidha, amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati:
1) Balozi Ramadhan Mwombe Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mstaafu;

2) Balozi Dkt. Mwanaidi Sinare Maajar, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza;

3) Balozi Peter Allan Kallaghe, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza;

4) Balozi Tovako Nathaniel Manongi, aliyekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa New York, Marekani.

Kamati hiyo itazinduliwa rasmi tarehe 31 Machi, 2023 Ikulu Dar es Salaam, saa 08:30 mchana.

View attachment 2569232
Sasa mama kashindwa kazi, wizara ina watu kibao, kwanini wasifanye tathmini na kuja na matokeo
 
Mambo ya hovyo na upuuzi kabisa! Ni mambo ya kutafutiana ulaji tu, what is diplomasia ya Afrika Mashariki kwa watanzania? Haikuundwa tume kuchunguza TANESCO na migao yao ya umeme sasa mnatuletea hizi takataka za ulaji?? Mambo ya HOVYO kabisa.Mungu atusaidie.
Niliposoma mara ya kwanza hii mada ilivyowekwa, akilini mwangu wizara ya kwanza ilikuwa ni hiyo hiyo inayohusu Tanesco.

Huyu anazo sababu zake. Wanaovuruga huko kwenye hii wizara ya Mambo ya Nje, ni hao hao watu wa aina yake muunda kamati, na anajua hivyo.
Tatizo linafahamika linakotokea, tume ni ya nini tena kama siyo kufuja pesa.
 
There is a Dis-connect kati ya Ik na Wizara, kila mmoja wao akitupa lawama kwa mwenzie.. Je upo uwezekano haya ni matokeo ya kuhamisha shughuli za kimataifa ikulu kama zilihamishwa? Je ni awamu gani?

Je, haya yamekuwa dhahiri zaidi baada ya mabadiliko ya haraka haraka katika miaka 3-4 iliyopita, je hakuna ajuaye anchofanya...yaani duties and responsibilities zimemegeka-megeka kati ya Ofisi ya mambo ya nje Ikulu...kama ipo? na Wizarani? au ni Ukinzani wa Sera inayoeleweka?

Je matarajio na matumaini ya SSH katika mchakato mzima wa ujio wa Kamara haukumpendeza...Je walisuasua na kushindwa kutoa msimamo baada ya kujua anayojua Makyembe?Nafikiri itakuwa sawa, nadhani, kuwa kabla ya ujio wa Kiongozi kama Kamara huwa ni shughuli pevu Wizara ya mambo ya nje na idara zingine za kiserekali...? au....ndio kwenye dis-connect?

Maswali mengi lakini naona SSH hajafurahishwa na majibu mepesi anayopewa.
Nasubiri matokeo kwa shauku kubwa
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda Kamati kwa ajili ya kutathmini utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kuiwezesha Wizara hiyo kutekeleza malengo ya Serikali katika kukuza diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa.

Ili kutekeleza azma hiyo amemteua Balozi Yahya Simba, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia kuwa Mwenyekiti wa Kamati.

Aidha, amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati:
1) Balozi Ramadhan Mwombe Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mstaafu;

2) Balozi Dkt. Mwanaidi Sinare Maajar, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza;

3) Balozi Peter Allan Kallaghe, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza;

4) Balozi Tovako Nathaniel Manongi, aliyekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa New York, Marekani.

Kamati hiyo itazinduliwa rasmi tarehe 31 Machi, 2023 Ikulu Dar es Salaam, saa 08:30 mchana.

View attachment 2569232
Serikalin kuna hela za kuchezea sana aisee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom