Rais Samia atoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Wafanyabiashara kufuatia kuungua kwa soko la Kariakoo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo kufuatia hasara kubwa waliyoipata kutokana na kuungua moto kwa soko hilo.

Kufuatia hasara kubwa iliyotokana na moto huo, Rais Samia ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina kujua chanzo cha moto huo.

Amesema Soko Kuu la Kariakoo ni soko kubwa jijini Dar es Salaam ambalo lina mkusanyiko mkubwa wa wafanyabiashara na kuteketea kwa soko hilo kutakuwa kumesababisha hasara kubwa kwa wapangaji na wamiliki wa soko hilo kongwe nchini.

Rais amesema soko hilo licha ya kuajiri wafanyabiashara wengi lakini ni kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki hivyo tukio hilo si hasara kwa wafanyabiashara tu bali hata kwa Serikali.




1625995952402.png

1625995987345.png


Pia soma: Soko la Kariakoo lateketea kwa moto
 
Mama mkono mtupu haulambwi, penye udhia penyeza rupia, wagawie hata lile fungu la sanamu.
Kweli.. inamaana hakuona mwenzie Lowasa ilibidi apenyeze lupia ili mwenyekiti ampitishe kugombea uraisi mwaka 2015. Huu usemi wa mkono mtupu haulambwi umeshamuadhibu dr Slaa tayari.
 
Back
Top Bottom