Rais Samia atategua kitendawili kilichotegwa na Hayati Magufuli mkoani Kagera?

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,730
KAGERA TUNAMPOKEA RAIS TUKIWA NA MATUMAINI NA FARAJA.

Miaka 6 imepita tangu tulipopatwa na janga kubwa na la kihistoria katika Mkoa wetu TETEMEKO LA ARDHI wengi mnakumbuka tulipopatwa na janga hilo RAIS alimtuma Waziri mkuu baada ya mwaka mmoja Rais alikuja Kagera akatwambia serkali yake haikuleta TETEMEKO binafsi maneno yale yananichoma moyo mpaka leo.

Baada ya miaka 6 amekuja Rais mwingine tunayemuona kama mfariji tunategemea mambo kadhaa kwake.

Tunaomba tupate punguzo la vifaa vya ujenzi kama alivyoomba aliyekuwa Mbunge wakati ule Mh.Lwakatare
Tunaomba tupate fidia kwa wahanga wa Tetemeko lile na kuvunja kwa utaratibu wa mfuko wa maafa kwani utaratibu uliotumika kuvunja mfuko wa maafa haukuwa sahihi.

Tunaomba utoe tamko la Stend kuu ya mabasi iliyotelekezwa Kyakairabwa.

Tunaomba utoe tamko la Ujenzi wa soko kuu la Bukoba ili kuondoa fedhea katikati ya mji kwani soko lililopo haliendani na sura ya mji na masoko ya Mikoa mingine.

Mwisho tunaomba utoe tamko kwa RPC na askari wake juu ya matumizi ya beria ya katoma inayoleta usumbufu kwa watumia barabara wakati wa usiku.

Nakutakia ziara njema yenye mafanikio.Karibu Bukoba "nyegera muno"

@katikabakama

Nieicopy ilivyo

View attachment 2253065View attachment 2253064View attachment 2253062View attachment 2253063View attachment 2253066View attachment 2253067

IMG_6795.jpg
View attachment 2253068
 
Back
Top Bottom