Rais Samia Ashusha Neema Miradi ya Trilioni 42.4/=

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,503
2,980
Tanzania inatarajia kupata miradi ya hifadhi ya mazingira, mabadiliko ya tabianchi ikiwemo nishati jadidifu yenye thamani ya sh. trilioni 42.4.

Miradi hiyo itasaidia kupunguza changamoto ya ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa kwa muiibu wa Mchango wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Nationally Determined Contribution-NDC). Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama ameeleza.

Dkt. Mkama alikuwa akifungua warsha ya kujadili matokeo ya Mkutano wa 27 na Maandalizi ya Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi.

Alisema fursa hiyo imekuja baada ya Rais Dkt. Samia kuwakutanisha Marais watano kutoka Zambia, Malawi, Zimbabwe, Botswana, Makamu wa Rais wa Angola.

Washiriki wengine wa kikao hicho ni Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo Afrika katika uzinduzi wa mtandao wa uzalishaji wa pamoja wa nishati jadidifu kwa nchi za Kusini mwa Afrika, kujad-ili fursa za uwekezaji kwenye sekta Anyo, miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Alisema miradi hiyo itafadhiliwa na Benki ya Dunia, Taasisi za Afrika 50, Shirika la Nishati la Afrika ambalo litashirikiana na Kampuni ya China Renewable Energies.​
 
Back
Top Bottom