Rais Samia ashiriki Mkutano wa wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, leo Julai 26, 2033

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) tarehe 26 Julai, 2023 jijini Dar es Salaam.



===

Rais Samia anazungumza
Ninayo furaha kubwa kuwakaribisha Tanzania. Tunakutana leo kujadili ajenda mabyo ndio moyo wa mataifa yetu. Mkutano wetu wa leo utaamua ni aina gani ya uwekezaji tunafanya, hakuna muda mwingine wa kujadili haya isipokuwa sasa.

Ni jambo la kusikitisha kuwa baadhi ya nchi za Afrika ukuaji wa uchumi haujakua hasa kuchochea ajira mpya kwa vijana, pia bara la Afrika bado linakabiliwa na matatizo ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana, njaa n.k

Bara letu lina watoto na vijana wengi, tunapaswa kuwekeza kwenye rasilimali watu. Kwetu sisi tuliopo hata tujiulize, bara tulilotithi ndilo bara tunalotaka kuwaachia vijana wetu warithi?

Mwalimu JK Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema maendeleo ni watu, watu ndio walengwa na wanufaika wa chochote kinachoitwa maendeleo. Hatuwezi kuliomboa bara letu pasipo kuwekeza kwa rasilimali watu, tangu mtoto anapozaliwa kwa maana ya upatikanani wa lishe bora na chanjo ili kupunguza udumavu.

Pia elimu ili kuwaandaa watoto vizuri, mitaala ikidhi mahitaji ya sasa.
660c87f3-f903-487e-91c4-ff1281c4d75e.jpg

59bc6150-afa0-4171-83c2-5dad776abfc3.jpg

a59a422e-ed61-46ea-8b55-c99768eeb170.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.

Nelson Mandela alisema Elimu ndio silaha yenye nguvu zaidi inayoweza kutumika kuubadilisha ulimwengu. Kama Tanzania, tumetenga fedha nyingi kwa ajili ya afua mbalimbali za lishe na afya ya mama, kuanzisha vituo vya elimu ya awali, mapitio ya sera ya elimu, programu na mitaala ya elimu, uanzishaji wa mfuko wa kusaidia familia maskini, uanzishaji wa programu ya elimu bila malipo kuanzia shule za msinhgi hadi form 6.

Kuwezesha vijana kiuchumi kwa kutoa 4%, kwa wanawake 4% na watu wenye ulemavu 2%. Pia, kuruhusu waliopata ujauzito kurejea shuleni, pamoja na kuwekeza kwenye kilimo.

Idadi kubwa ya vijana tulionao Afrika ni fursa pekee ni fursa kubwa, vijana hawa wanapaswa kuendelezwa.

Vijana wafundishwe kuhusu uzazi wa mpango, tuhakikishe elimu tunayotoa inakuwa na tija kwa vijana.

8895e142-a72a-4e3c-9a17-6d64dec792b0.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Madagascar Mhe. Andry Nirina Rajoelina mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.

733a92b1-9e45-4d45-b137-c62c9a4b906b.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa São Tomé na Principe, Carlos Vila Nova mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.

1f451fac-3d12-42b5-8d75-5bedf5798980.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Kenya, William Ruto mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.

7c7830c1-6986-4fb5-a1cb-90a89194cc21.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Bio mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.

54895b88-df02-48e2-8f60-03b9226b08c4.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa kando ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.

b9842201-cf31-465d-b279-858489cc4bdf.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Victoria Kwakwa pamoja na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo kando ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2023.
 
mtoa mada wewe ni mtumwa wa kifikra. Wachina na Warusi hawaongeni kiingereza,je hiyo imewafanya kupungukiwa nini? Lugha ni lugha tu haina uhusiano na akili za mtu,elimu ya mtu wala uwezo wa mtu kuelewa mambo.
 
Alisikika mzanzibar mmoja wakati wa ufunguzi wa mkutano unaoendelea JNICC.

Kazi ipo jamani. Mnapenda kuzurura na kupiga deal lakini hampendi kutulia na ku-polish kizungu chenu.
Kingereza kimenyooka kabisa hicho ,acha upunguani wako
 
Huyo mdau fom foo necta aliscore kama Young lunya kwa mujibu wa maneno ya young killer
 
Alisikika mzanzibar mmoja wakati wa ufunguzi wa mkutano unaoendelea JNICC.

Kazi ipo jamani. Mnapenda kuzurura na kupiga deal lakini hampendi kutulia na ku-polish kizungu chenu.
Mleta mada what's wrong with you? Don't follow follow me without because. You cant me am another. I think the delegates have been tolded what exactly to do.

Nyau wewe!

Saint Anne
 
Alisikika mzanzibar mmoja wakati wa ufunguzi wa mkutano unaoendelea JNICC.

Kazi ipo jamani. Mnapenda kuzurura na kupiga deal lakini hampendi kutulia na ku-polish kizungu chenu.

Kwani umahiri wa lugha iliwa mojawapo ya agenda?
Nyie ndio wale wale mtu akiongea kingereza hata mambo ya hovyo hovyo mnapiga makofi na kuchekelea ILA mtu akishusha mapoint kwa kiswahili mnanyamaza...Shame!
 
Hoja yangu sio matumizi ya Kiswahili Bali ni grammatical mistake katika utangulizi wake
Hoja yangu sio matumizi ya Kiswahili Bali ni grammatical mistake katika utangulizi wake

Haijalishi grammatical au broken bado ni mtumwa wa kifikra na hujaenda na hutokuja kufika nje ya bongoland, mataifa kidume as German nk, au Guangzhou tu pale ukanunue 3rd handed products uje utuuzie kama utakutana na mchina anatapika kimalikia !.
 
Back
Top Bottom