Rais Samia ashauriwe vyema uchumi unakufa

Rais Samia ashauriwe vyema uchumi unakufa

Ukiwa masikini au ukitoka familia masikini au wwe sio tajiri au mfanyabiashara sahau kuwa kiongozi kwa wenzetu maana wanayajua haya.
Kwao uraisi sio sandakalawe kitu cha kupewa pewa tu KILA mtu uraisi ni kubeba maisha ya nje.
Kiongozi wa nchi yafaa awe mfanyabiashara au mchumi.
Obama alitoka katika familia masikini, hakuwa tajiri wala mfanyabiashara!
 
Kiukweli hali ya nchi inako kwenda sio kuzur,Ijapokuwa tunaona kawaida me nafikiri turudi kumwomba Mungu kwa dini zetu mambo yatakaa sawa,makuhani wa nchi wamejiamini kupita kiasi hata vilio vya wananchi hawavisikii
 
Kwa Magufuli mlisema ameua uchumi, kwa Samia mnasema uchumi unakufa, kwani uchumi unakufa mara ngapi?
Uchumi unaweza kufa hata mara milioni.

Uchumi una tabia ya kufa mara nyingi na kufufuka mara nyingi pia ukifufuliwa.
 
Huwezi kupiga hatua ya kimaendeleo kwa kuongeza kodi (tozo). Unapoweka kodi kubwa unaua uchumi. Uchumi unapokufa huwezi kupata hiyo kodi. Shughuli za kiuchumi zinaposhuka kuna watu hawataweza kuajiriwa katika maisha yao yote. Watu watamaliza vyuo lakini hawatapata fursa ya kuajiriwa katika maisha yao yote.

Rais atafute washauri wazuri wa maswala ya uchumi ili kuliokoa taifa. Kuna watu wanasema tulipe tozo tujenge nchi. Tozo kubwa au kodi kubwa inaharibu uchumi.

Tozo ndogo au kodi ndogo inachochea uchumi, inaruhusu watu kuwa na kipato cha kufanya manunuzi au cha kufungua biashara mpya na kuongeza mzunguko wa fedha. Ukimkamua mtu kwa kodi kubwa au tozo kubwa unampunguzia uwezo wa kufanya manunuzi au unaua kabisa uwezo wake wa kufungua biashara mpya. Kodi kubwa haijawahi kuwa suluhisho la kuwa na uchumi mzuri.
Amerithi ubishi kwa kaka yake hashauriki.
 
Rais anatakiwa awe na washauri wazuri. Unajua serikali haina uwezo wa kuajiri labor force yote hivyo ana wajibu wa kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi. Sekta binafsi ndio mwajiri mkubwa kokote duniani.
Mkuu uko sahihi ila sioni kiongozi mwenye dhamira ya kuboresha sekta binafsi. Hawa viongozi ni wachoyo,wajivuni,waongo na wanyonyaji.Waache wafaidi tu.
 
Meanwhile wenzetu wanaondoa tozo katika miamala ya kifedha. Sisi ndio kwanza kuongeza kila leo

IMG-20210822-WA0027.jpg
 
Huwezi kupiga hatua ya kimaendeleo kwa kuongeza kodi (tozo). Unapoweka kodi kubwa unaua uchumi. Uchumi unapokufa huwezi kupata hiyo kodi. Shughuli za kiuchumi zinaposhuka kuna watu hawataweza kuajiriwa katika maisha yao yote. Watu watamaliza vyuo lakini hawatapata fursa ya kuajiriwa katika maisha yao yote.

Rais atafute washauri wazuri wa maswala ya uchumi ili kuliokoa taifa. Kuna watu wanasema tulipe tozo tujenge nchi. Tozo kubwa au kodi kubwa inaharibu uchumi.

Tozo ndogo au kodi ndogo inachochea uchumi, inaruhusu watu kuwa na kipato cha kufanya manunuzi au cha kufungua biashara mpya na kuongeza mzunguko wa fedha. Ukimkamua mtu kwa kodi kubwa au tozo kubwa unampunguzia uwezo wa kufanya manunuzi au unaua kabisa uwezo wake wa kufungua biashara mpya. Kodi kubwa haijawahi kuwa suluhisho la kuwa na uchumi mzuri.
Serikali inakusanya tozo, ili kuongeza vituo vya afya, madarasa na shule mpya. huko kuna kuongezeka kwa ajira za serikali. Kupitia mishahara kutaongeza purchasing power ya waajiriwa wapya, mzunguko wa fedha kwenye maeneo ya waajiriwa. Pia tukumbuke shughuli za ujenzi zitarudisha fedha kwa local contractors watakao jenga vituo vya afya na mashule, vibarua watapata ajira, wafanyabishara wata supply mahitaji ya ujenzi kwa wakandarasi.

Maeneo watakayo ajiriwa watu wapya yatachochea kuongezeka kwa watoa huduma za ziada, na biashara kama mawakala wa fedha, watoa huduma za usafiri, wafanyabiashara wa furniture, electronics watafanya biashara, mabenki yatakopesha wateja wapya watakao ajiriwa. Ni kwamba hautwezi kuona mchango wa tozo ndani ya mwezi mmoja au miwili. Tujifunge mkanda kwa mwaka mmoja tutafanya evaluation ya tozo. Maendeleo yanakuja na maumivu.
 
Kama unashauriwa na failures unaanzaje kuwa na akili na hao failures wewe ndio unaona vipaaanga, ndiomaana wakati mwingine udikteta unahitajika , ita wasomi ita wachumi wakushauri ikifika miezi miwili hakuna mabadiliko piga risasi wote watakaokuja tena watakua na mawazo yenye akili, China hawajaendelea kwa bahati mbaya wanafanya kazi na masihara ni msamiati kule hakuna unakula kitanzi tu, eti PHD nyoooo za Kwiyoo
 
Uchumi unaweza kufa hata mara milioni.

Uchumi una tabia ya kufa mara nyingi na kufufuka mara nyingi pia ukifufuliwa.
Kumbe! Magufuli aliua uchumi hadi March 17 alipofariki. Mama akrithi tarehe 17 hiyo hiyo hadi leo takribani miezi 6 tu, haijazidi hapo. Bila shaka huo uchumi uliokuwa umeuliwa na Magufuli ulifufuka kwa sekunde chache sana akaja kuuua Samia tena.
 
Nahisi Kuna kuharibiana!
Halafu anae haribiwa hajagundua
 
Sidhani kama kuna ulazima wa kushauriwa katika hili hapa ni yeye mwenyewe akumbuke malalamiko ya wananchi kuhusu tozo hizi.

Hapa ni common sense tu itumike vinginevyo waacheni watuburuze kwa kodi dhalimu halafu tuwe kama Zimbabwe.
Common sense is not common to all .. Remember that 😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom