Rais Samia ashauriwe vyema uchumi unakufa

Rais Samia ashauriwe vyema uchumi unakufa

konda msafi

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
1,752
Reaction score
8,950
Huwezi kupiga hatua ya kimaendeleo kwa kuongeza kodi (tozo). Unapoweka kodi kubwa unaua uchumi. Uchumi unapokufa huwezi kupata hiyo kodi. Shughuli za kiuchumi zinaposhuka kuna watu hawataweza kuajiriwa katika maisha yao yote. Watu watamaliza vyuo lakini hawatapata fursa ya kuajiriwa katika maisha yao yote.

Rais atafute washauri wazuri wa maswala ya uchumi ili kuliokoa taifa. Kuna watu wanasema tulipe tozo tujenge nchi. Tozo kubwa au kodi kubwa inaharibu uchumi.

Tozo ndogo au kodi ndogo inachochea uchumi, inaruhusu watu kuwa na kipato cha kufanya manunuzi au cha kufungua biashara mpya na kuongeza mzunguko wa fedha. Ukimkamua mtu kwa kodi kubwa au tozo kubwa unampunguzia uwezo wa kufanya manunuzi au unaua kabisa uwezo wake wa kufungua biashara mpya. Kodi kubwa haijawahi kuwa suluhisho la kuwa na uchumi mzuri.
 
Tatizo kubwa la Mama hadi sasa hajagundua yuko na washauri ambao sio sahihi. Wasaidizi wake wengi wana uchu wa kugombea urais 2025 hivyo wana mgombanisha na wananchi bila yeye kujua.

Huu ni mpango mahsusi ulio sukwa. Na kama mama hata shtuka avuruge safu yake ya uongozi kuanzia Pm hadi ma dc hamna rangi ata acha kuona.

Fikiria juzi kuna naibu katibu mkuu afya na hamasisha kujifukiza. Ni kwamba yuko wizara ya afya lakini ana pinga chanjo. Hiyo ni simple maths.
 
Tatizo kubwa la Mama hadi sasa hajagundua yuko na washauri ambao sio sahihi. Wasaidizi wake wengi wana uchu wa kugombea urais 2025 hivyo wana mgombanisha na wananchi bila yeye kujua...
Inasikitisha sana. Kuna mambo huhitaji kuwa mwanauchumi kuyaona hayako sawa.
 
Moja wapo ya athari zilizosababishwa na hizi kodi ni mfumuko wa bei Kila mfanyabiashara anangalia maslahi yake angalia bei ya gesi ,mbolea,mafuta,nyama,umeme....? Wenye wizara husika wala hawafatiliii aliongea kalemani gesi ishuke ndani ya siku 14 badala yake ikapanda zaidi
 
Tatizo kubwa la Mama hadi sasa hajagundua yuko na washauri ambao sio sahihi. Wasaidizi wake wengi wana uchu wa kugombea urais 2025 hivyo wana mgombanisha na wananchi bila yeye kujua...
Huyu si alishangiliwa alipoteua mpaka wasaidizi binafsi wa uchumi? Tulihoji hapa mawaziri wa fedha wanakazi gani tukajibiwa wale wanasiasa wanaweza mshauri vibaya ili waje wagombee huko mbele kwa maslah yao! Sawa ao washauri binafsi aliowateua wanakula tu mishahara ya bure.
 
Moja wapo ya athari zilizosababishwa na hizi kodi ni mfumuko wa bei Kila mfanyabiashara anangalia maslahi yake angalia bei ya gesi ,mbolea,mafuta,nyama,umeme....? Wenye wizara husika wala hawafatiliii aliongea kalemani gesi ishuke ndani ya siku 14 badala yake ikapanda zaidi
Dah! Mambo yapo wazi kabisa. Sijui kwa nini Rais halioni hili? Basi atafute washauri wa maswala ya uchumi wamshauri.
 
Huyu si alishangiliwa alipoteua mpaka wasaidizi binafsi wa uchumi? Tulihoji hapa mawaziri wa fedha wanakazi gani tukajibiwa wale wanasiasa wanaweza mshauri vibaya ili waje wagombee huko mbele kwa maslah yao! Sawa ao washauri binafsi aliowateua wanakula tu mishahara ya bure.
Wakina nani ni washuri wa rais wa uchumi? Kama wapo basi hawamshauri, wanakula mshahara wa bure kama ulivyosema.
 
Sidhani kama kuna ulazima wa kushauriwa katika hili hapa ni yeye mwenyewe akumbuke malalamiko ya wananchi kuhusu tozo hizi.

Hapa ni common sense tu itumike vinginevyo waacheni watuburuze kwa kodi dhalimu halafu tuwe kama Zimbabwe.
 
Tusisubiri tufike hadi Zimbabwe mkuu. Zimbabwe kulikuwa kunatisha, sijui kama bado kuko hivyo ila usiombe nchi ikafikia hali iliyokuwa nayo Zimbabwe. Kuna miaka nilipita Harare hali ilikuwa ya kusikitisha.
 
Back
Top Bottom