Rais Samia anza kuandaa mlio utakaolia baada ya kuachia Ikulu

Rais Samia anza kuandaa mlio utakaolia baada ya kuachia Ikulu

Rais Samia na mwanao andaeni mlio

Rais Samia na mwanao Abdul andaeni mlio mtakaokuwa mkilia pale muda wa kukandwa kwenu utakapofika kwa madudu mnayoyafanya mkiwa Ikulu.

1. Kisiasa
Kisiasa Rais Samia hukubaliki ndani ya CCM na nje CCM mbaya zaidi haukubaliki pia ndani ya nchi na nje ya nchi.
Ndani ya ccm kuna kundi kubwa sana lina chuki sana na wewe hasa baada kupanga watu unaotaka wawe wabunge wenye mlengo wa kutetea ufisadi na kuwakata wale wanaopinga ufisadi na wenye ushawishi ndani ya ccm. Mfano Ummy Mwalimu, Luhaga Mpina, January Makamba, Flatei Maasai wewe ndiyo uliagiza wakatwe kibabe.
Kiburi chako kikakutuma umptishe mwanao Wanu na mme wake Mchengerwa kibabe kuwa wabunge.

Chuki kutoka nje ya ccm ni kubwa baada ya wewe Rais Samia kumzuia Luhaga Mpina kugombea urais kibabe na kihuni kabisa kinyume na katiba ya nchi, kana kwamba haitoshi ukaamua kumfunga Lisu kwa kesi ya uongo ya uhaini.

Chuki kutoka nje ya nchi pia ni kubwa sana, Tanzania imenyimwa misaada kutoka kila pembe ya dunia kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea tangu nchi ipate uhuru!. Rais Samia umeharibu legacy ya Tanzania kwamba ni nchi ya amani na utulivu kutokana na mauwaji ya raia wasio na hatia uliyoyafanya siku ya uchaguzi octoba 29/ 2025 na sasa hivi unawindwa na mahakama ya ICC .
Wakati unaingia madarakani ulijitapa kufungua nchi, je umeifungua mpaka wapi?

2. Kijamii
Kijamii hamna kiongozi aliyewahi kuchukiwa Tanzania kama wewe Rais Samia kwa sababu umeendesha utekaji na uuwaji wa waziwazi kabisa bila aibu. Watu waliotekwa chini ya utawala wako ni zaidi ya 100, Mdude na Humphrey Polepole wameacha michirizi ya damu hadi leo! Kwenye kichwa chako wewe Samia unadhani wana ccm wote wamefurahishwa na kitendo chako cha kumteka balozi, katibu wa itikadi na uenezi na mjumbe wa kamati kuu ya ccm? Nikutonye tu ya kuwa wanaccm wengi wamechukizwa mno na kitendo hicho na wanasubiri tu muda ufike wakugawane .
Kana kwamba haitoshi umefanya mauaji ya kutisha tarehe 29 Oktoba kwa kuuwa watoto, wazee ,vijana na kina mama wasiokuwa na hatia yoyote na badala ya kuwaomba radhi watanzania wewe ukajitokeza kushangilia huku ukiahidi kufanya mauaji mengine zaidi ya hayo pale itakapopidi!
Andaa mlio utakaokuwa unalia siku unaenda kuonyesha ulipowazika hao watu uliowaua ili tu wewe uendelee kukalia ikulu kwa mabavu.

3 Kiuchumi.
Rais Samia umeharibu uchumi wa nchi kwa kuuza mbuga, makaa ya mawe, bandari zote na hivi karibuni umeamua kuuza hifadhi ya taifa ya dhahabu! , sasa hivi kila kona wachimbaji wadogo na wafugaji wanafukuzwa bila fidia wala utaratibu wowote.
Tukuulize swali Rais Samia baada ya nchi kuikuta ipo uchumi wa kati mpaka sasa umeifikisha uchumi wa wapi?

Kwa madudu haya Rais Samia utatetewa na nani baada ya kutoka ikulu? Nakushauri tu uanze kuandaa mlio wa kulia maana chuki na kisasi cha watanzania juu yako na uzao wako ni kubwa sana.
Sawa Etwege. Samia ataondoka 2030, hamtaki mtoeni basi
 
Ina maana wale maelfu ya raia waliosusa kutoka kwenda kumpigia kura samuya ile oktoba 29 woote wale ni wakristo?!.
Kwann mnakosa akili kbs chawa, toka tupate uhuru hakujawahi kuwa na rais aliyekataliwa waziwazi na wananchi wengi kama huyu mama!
Waliojitokeza kuleta vurugu huwezi kuwalinganisha na wengi sana wanaokaa mbali na siasa lakini wanamuunga mkono SSH, usidanganywe na zile harakati za tarehe 29 October tazama mengi anayoyafanya nchi nzima.

Waingereza wanasema 'Silent Majority' yaani wengi walioamua kukaa ukimya.

Kule Tanga kumefanyika ukarabati mkubwa na meli kubwa zinaweza kushushwa na kupakiwa, mji ule muda sio mrefu utapewa hadhi ya kuwa jiji.

Mengi ya namna hiyo yanafanyika, wanaoyaona wanazichukulia kuwa ni ujinga hizo kelele za Samia Must Go.
 
Labda wewe mtoto mdogo huyaelewi masuala ya kisiasa, udini ukabila ukanda zote hizo huwa siasa chafu ambazo zinaanzishwa na watu wenye kutafuta uhalali mbele ya jamii (legitimacy).
Sawa mtu mzima. Udini mnautumia huko mbogamboga kwa anayeikosoa hii serikali yenu, kwani kila mkosoaji ni Mkristo? Wakosoaji Waislamu nao ni wadini?
 
Waliojitokeza kuleta vurugu huwezi kuwalinganisha na wengi sana wanaokaa mbali na siasa lakini wanamuunga mkono SSH, usidanganywe na zile harakati za tarehe 29 October tazama mengi anayoyafanya nchi nzima.

Waingereza wanasema 'Silent Majority' yaani wengi walioamua kukaa ukimya.

Kule Tanga kumefanyika ukarabati mkubwa na meli kubwa zinaweza kushushwa na kupakiwa, mji ule muda sio mrefu utapewa hadhi ya kuwa jiji.

Mengi ya namna hiyo yanafanyika, wanaoyaona wanazichukulia kuwa ni ujinga hizo kelele za Samia Must Go.
Tufanye ni sawa samuya kafanya/anafanya makubwa...ila swali ni kwamba ni kwann watz walio wengi hawamkubali??
Hata mikoa ambayo hakukuwa na vurugu kabisa mfano Pwani, watu wachache sana walijitokeza kwenda kumpigia kura!.
 
Hata wasipomkubali lakini ndiye Rais hadi 2030. Sasa hata kama unamkubali Tundu atakusaidia nini wakati yuko gerezani??
 
Amefeli wapi? Nani anq marking scheme ya kuongoza Tanzania?? Uchumi unapaa, miundombinu inajengwa, wafanyakazi wanapata mishahara, utalii unakuwa, mashule na hospitali zinajengwa.

Halafu mburukenge moja kutoka Kantalamba inasema Rais anafelishwa, amefeli wapi?
Kwa hyo kuishi kantalamba ni kosa kwamba wanaoishi kantalamba nanjilinji nakiu likawage njinjo migelegele hawana haki ya kutoa maoni?

Mawazo yako n ya 1961 ukikaa dsm ndio unaakili kubwa
 
Fua la kuku hili halimpati mwewe. Kulia utaendelea kulia mwenyewe, uRais siyo nafasi ya mchezo. Huyo siyo mwenzio. Ana security na mafao hadi mwisho wa maisha yake.
Mafao ni kodi yako na yangu atakayolipwa, sio hisani wala weledi wa utawala.

Urais ni wa damu sio sanduku la kura za 29/10/2025 AMBAZO hazikutimia mil 32 iliyobuniwa na tume hewa.

Kumaliza muda wake ni kwa sababu ya Katiba mbovu aliyoidharau na kuiita kijitabu tu.
 
Inasikitisha sana
Kinachosikitisha zaidi ni kuwaacha Watendaji/Wateule wake wajiamulie namna ya kuziendesha Taasisi/Wizara kwa utashi wao badala ya kwa mujibu wa Sheria za Nchi. Eti Waziri anakataa kulitumia gari la Serikali analitumia lake biafsi tena kwa plate number ya Serikali. Hilo halitoshi anajitengenezea msafara wake ambao haijulikani ni nani anaegharamia. Na kama ni yeye binafsi fedha kazitoa wapi? Hivi wanadhani kule wanakokwenda kutembeza mabakuli Balozi zao hapa Nchini hawaoni upuuzi wa uvujaji wa fedha za Umma?? Tena zilizopatikana kwa misaada??

Kama Nchi ingekuwa na maadili japo katone tu basi ingekuwa hivi:-
- Hutaki kutumia gari la serikali basi
na ofisi ya yake usisogelee.
Kila Waziri au wakuu wa taasisi wakiamua kufanya hivyo Nchi ingekuaje? Upuuzi wa kutisha.

Hapo wahangaika kumtafuta mchawi wakati matendo yao ya hovyo yako wazi.
 
Nyie vijana wa CCM ndo mumetufikisha hapa tulipo

Huwa mnawaza matumbo yenu tu mkiondolewa nje ya mfumo ndo akili zinawakaa sawa

Hili swala tulilipigia kelele sana jamani no reform no election nyie mkatuona sisi wajinga

Ona sasa nchi inauzwa wazi wazi na huyu mama wa kioman
Huu uzi ufungwe. Hii comment umemaliza. Nilikuwa najiuliza ni kweli au naota? Mtoa Mada alikuwa chawa pro leo kimemkuta nini?. Huyo mtu wenu hafai kwa kulumangia wala kwa mchuzi ananuka damu za watu kifupi aondoke tu.
 
Kwa hyo kuishi kantalamba ni kosa kwamba wanaoishi kantalamba nanjilinji nakiu likawage njinjo migelegele hawana haki ya kutoa maoni?

Mawazo yako n ya 1961 ukikaa dsm ndio unaakili kubwa
Kama una akili huwezi kukaa Nanjilinji au Migelegele. Huko ni kwenda unachungulia wazee then unatoka!!
 
Mafao ni kodi yako na yangu atakayolipwa, sio hisani wala weledi wa utawala.

Urais ni wa damu sio sanduku la kura za 29/10/2025 AMBAZO hazikutimia mil 32 iliyobuniwa na tume hewa.

Kumaliza muda wake ni kwa sababu ya Katiba mbovu aliyoidharau na kuiita kijitabu tu.
Nyinyi si mlisema mtakinukisha, mlitaka tufanye nini zaidi ya kuwawashia risasi wakati mnavuruga uchaguzi.

Hizo ndiyo hasira za mkizi, naamini mmejifunza hamtorudia tena
 
Back
Top Bottom