Rais Samia anapaswa kuchukua mazuri yote katika hotuba ya Mbowe ya Mwanza

Madai haya sio kweli kwa sehemu kubwa.

Piga hesabu ya vituo vya kura halafu unambie ni vituo vingapi mawakala waliondolewa.

Twende kisayansi.

Huku kwangu nilikokuwa, mawakala wa chadema hawakutokea kituo cha kura.

Kwa hiyo ni disinformation kudai mawakala wa chadema walifukuzwa vituo vyote vya kupigia kura.

Uwe systematic katika udadavuzi wako.
Nimekupa mfano wa Mara, huku Dsm nilipo vituo karibia vyote ikiwemo nilichopigia kura mawakala wa upinzani waliruhusiwa kuingia vituoni saa 6 mchana, ukitaka kubisha ok, but huo ndio ukweli.

Wengi wao walidanganywa watapewa barua za utambuzi siku ya kupiga kura mapema asubuhi kabla vituo havijafunguliwa, lakini ilipofika hiyo siku hapakuwepo na watendaji wa kutoa hizo barua, matokeo yake vituoni walikuwepo wasimamizi wa kura na wajumbe na wenyeviti wa serikali za mtaa ambao wote ni CCM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom