Rais Samia anajenga Tanzania ya viwanda kwa vitendo

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,907
Heko wadau..

Rais wa Tanzania mh.Samia Suluhu Hassan anajenga Tanzania ya viwanda kwa vitendo na bila makelele ..

Kwa mda mfupi Sana amevutia maelfu ya wawekezaji katika maeneo mbalimbali hususani viwanda .

Tulikuwa na Rais ambaye alikuwa anajigamba Sana Kuwa Rais wa viwanda lakini ndani ya miaka yote 6 hakuna viwanda vya maana ambavyo vilijengwa zaidi ya vyerehani .

Kwa Wakulima wanalia Lia Sana kwa bei za mbolea kuwa juu ila wasijari mwaka ujao bei zitashuka kwa vile viwanda viwili vikubwa vya mbolea vinajengwa Dodoma na Mtwara.

Sasa Tanzania ya viwanda inajengwa na Samia.Hongera Rais wangu kwa Kazi nzuri 👇

Screenshot_20211128-174543.png

Screenshot_20211128-174734.png

Screenshot_20211123-111536.png

Screenshot_20211123-111621.png

Screenshot_20211123-111217.png

Screenshot_20211117-134136.png
 
Hii nchi inavituko sana aisee, yaani vyerehani vitatu navyo vinageuka kua kiwanda , hadi watengeneza juice za miwa nao ni viwanda .
 
Mkuu umeleta mada tamu sana,

Mungu akubariki sana kwa hili,

Tuendelee kuipigania nchi yetu

Tuendelelee kumpigania Rais wetu

Kaziiendelee
 
Kwa hayo yanayoendelea, kuna hatua. Kwenye haya na mengine mengi, unaweza kumchukia Samia kwa sababu umeamua kumchukua.

Yupo sahihi sana kwenye sera za uchumi, japo anatakiwa kwenda hatua moja zaidi. Tunatakiwa kuwa na sheria ya uwekezaji, sheria ambayo inazuia kabisa uwezekano wa kiongozi yeyote kuvuruga uwekezaji kama ilivyotokea awamu ya 5.

Doa kubwa kwa Samia, ni hawa maharamia akina Kingai wanaobbikia kesi watu ovyo. Hawa akina Kingai, Mahita na akina Jumanne, wanatakiwa waende wakaungane na mwenzao Sabaya, waiache nchi inawili katika haki na maendeleo ya kiuchumi.

Mbowe amebambikiwa kesi, lakini tutambue kuwa si yeye pekee, wapo wengi. Ubambikiaji kesi kwa Mbowe inasikika zaidi kutokana na nafasi yake, na kauli mbaya aliyoitoa Samia.

Vinginevyo, Tanzania chini ya Samia ingekuwa na umoja wa ajabu, na katika umoja, maendeleo hayakosekani.

Wakati haya yakiendelea, ni muhimu kuwa na katiba mpya itakayohakikisha, huko mbeleni hatuji kuangukia kwenye primitive leadership kama ile ya awamu ya 5.
 
Heko wadau..

Rais wa Tanzania mh.Samia Suluhu Hassan anajenga Tanzania ya viwanda kwa vitendo na bila makelele ..

Kwa mda mfupi Sana amevutia maelfu ya wawekezaji katika maeneo mbalimbali hususani viwanda .

Tulikuwa na Rais ambaye alikuwa anajigamba Sana Kuwa Rais wa viwanda lakini ndani ya miaka yote 6 hakuna viwanda vya maana ambavyo vilijengwa zaidi ya vyerehani .

Kwa Wakulima wanalia Lia Sana kwa bei za mbolea kuwa juu ila wasijari mwaka ujao bei zitashuka kwa vile viwanda viwili vikubwa vya mbolea vinajengwa Dodoma na Mtwara.

Sasa Tanzania ya viwanda inajengwa na Samia.Hongera Rais wangu kwa Kazi nzuri 👇

View attachment 2026387

View attachment 2026388

View attachment 2026389

View attachment 2026390

View attachment 2026391

View attachment 2026392
nani wanamilki hivyo viwanda vyako kama si nagabacholi. anavijenga kwa matusi nonsense
 
Tunapigana na nyie wapuuzi wenye chuki na wapotoshaji.Tunampigania kwa mambo makubwa aliyofanya kama haya👇

View attachment 2026465

View attachment 2026466

View attachment 2026467

View attachment 2026468

View attachment 2026470

Kama mnampenda mama sana na mnamtakia mema; aachane na mapenzi na wakina January na Makonda kwani bila kuwa na umeme wa uhakika na usalama wa mali zao,hivyo viwanda vitafungwa kabla havijaanza kuzalisha !! Kwa wawekezaji wanajali faida na sio sura ya Rais wa nchi!!! Msijidanganye!
 
Back
Top Bottom