Rais Samia anajaribu kuzima moto wa petrol kwa maji

Unapokuwa na hadhi ya kibalozi ya nchi fulani,Wewe unakuwa ni mmoja kati ya waliopo katika hiyo serekalia,unapoipinga hiyo serekqli unajipinga wewe mwenyewe,kwa hiyo unajivua katika serekali bila wewe kuwa unajijua,ikiwa hujijui,inabakia kutanfazwa rasmi kuwa umevuliwa,kwa vile hujijui,wajibu wako.
Kwani wajibu wa balozi ni kutetea maovu ya serikali
 
Utake kuvuruga amani,halafu uchekewe.Hata Mwalimu Nyerere,hakuwachekea waliotaka kuvuruga amani.Hata aliogombania nao uhuru,walipotaka kuleta ujinga,aliwaonyesha cha moto.
Anayeuza bandari na anayetetea isiuzwe nani anayevunja amani.
 
Moto wa petroli una tabia kuu moja, unapoumwagia maji ili kuuzima unaibukia pembeni tena kwa nguvu zaidi ya ule wa mwanzo tena una tabia ya kulipuka.

Deusdedith Soka kijana aliyeandamana kupinga mkataba wa DPW jana kachomewa nyumba yake na watu wasiojulikana, Mdude, Mwambukusi na Dr. Slaa walifunguliwa mashitaka ya uhaini kwa kupinga mkataba wa DPW, jana Rais kamfutia dr. Slaa hadhi ya ubalozi kwa kupinga mkataba wa Bandari. Yote hii ni kujaribu kuwazima wote wanaohoji mkataba na DPW.

Nataka nimwambie Rais kuwa wanaomshauri afanye hivyo wanampotosha, unapojaribu kumdhibiti Soka anaibuka Mdude, unapomdhibiti Mdude anaibuka Mwambukusi, ukimdhibiti Mwambukusi anaibuka Slaa ukimdhibiti Slaa atakuja Tibaijuka ukiwadhibiti hao yatakuja madhehebu ya dini asifikiri atawamaliza.

Atambue nyuma ya hawa individuals kuna watu nyuma yao kuna taasisi nyuma yao kuna vyama nyuma yao. Siku hizo taasisi na watu wakiamua kuungana mlipuko wake utakuwa mkubwa sana sijui kama ataweza kuuzima.

Sabato njema watu wa Mungu.
Kumbe Slaa ni mbobevu wa Lugha nne hatari sana
 
Ukifuatilia maongezi ya nyumbu unaweza kuwehuka haki ya nani, wanaongea ujinga ujingaaaa!
 
Back
Top Bottom