Rais Samia ana bahati ya kuwa kipenzi cha wapinzani, haijawahi kutokea

Katika historia ya hii nchi haijawai tokea rais na mwenyekiti wa CCM akapendwa kiasi hiki na wafuasi wa vyama vya upinzani.

Naweza kusema taifa limepata bahati kubwa kuwa na kiongozi mwenye ushawishi wa kipekee.

Ni Rais ambaye hata ikitokea amekosea lawama zake atabebeshwa Kikwete au Magufuli inategemea na aina ya kosa. Itasemwa team msoga au sukuma gang. Na hii shughuli uwa inafanywa na wapinzani huku CCM wakila bata maana kazi ni nyepesi.

Ndio Rais ambaye akitokea yoyote wa kumnyooshea kidole basi wapinzani na CCM watasimama pamoja kumpambania.

Tuendelee kumuunga mkono Mama yetu Samia. Kwa kweli itatuchukua miaka hata elfu moja kumpata rais anaeweza kuunganisha makundi yote CCM na upinzani wakazungumza lugha moja.

Mama Samia anaupiga mwingi!
Mama Samia ana akili nyingi sana,kuna vidampa bado hawajamuelewa na hawatamuelewa.
 
Back
Top Bottom