evangelical
JF-Expert Member
- Nov 21, 2011
- 5,970
- 9,901
Jana nimemsikia Samia akisema anasitisha shughuli za bunge tarehe 27 /6/2025 ila Bunge litavunjwa Tarehe 3/8/2025 nimesoma katiba yetu kwanza Ibara ya 65 ambayo inasema. Ninainukuu
" 65.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, maisha ya kila Bunge yatakuwa ni muda wa miaka mitano.
(2) Kwa madhumuni ya Katiba hii maneno "maisha ya Bunge" maana yake ni ule muda wote unaoanzia tarehe ambapo Bunge jipya limeitishwa kukutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge kwa ajili ya kuwezesha Uchaguzi Mkuu mwingine wa kawaida kufanyika. 50 "
Hapo sijaona sehemu yeyote inasema rais anatakiwa kusitisha shughuli za Bunge.
Nika pitia Ibara ya 90 nayo ninainukuu.
"90.-(1) Baada ya Uchaguzi Mkuu Rais ataitisha Mkutano wa Bunge Jipya ufanyike kabla ya kupita siku saba tangu kutangazwa matokeo ya huo Uchaguzi Mkuu katika majimbo ya uchaguzi yote isipokuwa katika majimbo yale ambako uchaguzi umefutwa na kufanywa upya. (2) Rais hatakuwa na uwezo wa kulivunja Bunge wakati wowote, isipokuwa tu-
(a) kama Bunge limemaliza muda wa uhai wake kwa mujibu wa ibara ya 65 ya Katiba hii; au wakati wowote katika miezi kumi na miwili ya mwisho ya uhai wa Bunge, isipokuwa tu kama Spika amepokea taarifa rasmi inayopendekeza kuundwa kwa Kamati Maalum ya Uchunguzi kwa madhumuni ya kumuondoa Rais madarakani kwa mujibu wa ibara ya 46A ya Katiba hii;
(b) kama Bunge limekataa kupitisha Bajeti iliyopendekezwa na Serikali;
(c) kama Bunge limekataa kupitisha Muswada wa sheria kwa mujibu wa idara ya 97(4) ya Katiba hii;
(d) kama Bunge limekataa kupitisha hoja ambayo ni ya msingi katika sera za Serikali, na Rais anaona kwamba njia ya kuendelea kutoka hapo si kumteua Waziri Mkuu mwingine bali ni kuitisha Uchaguzi Mkuu;
(e) endapo, kutokana na uwiano wa uwakilishi wa Vyama vya Siasa katika Bunge, Rais anaona kwamba hakuna uhalali kwa Serikali iliyopo kuendelea kuwapo, na wala haiwezekani kuunda Serikali mpya.
(3) Muda wa maisha ya Bunge ukimalizika Bunge litahesabiwa kuwa limevunjwa; isipokuwa kwamba muda huo ukisha wakati wowote ambapo Jamhuri ya Muungano iko katika vita Bunge laweza mara kwa mara kuongeza muda huo uliotajwa katika ibara ya 65 ya Katiba hii kwa muda usiozidi miezi kumi na miwili mara kwa mara lakini maisha ya Bunge hayawezi kuongezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo kwa muda unaozidi miaka mitano. "
Sasa hili suala la Rais kusema.nasitisha shughuli za Bunge amelitoa wapi?
Huu si uvunjaji wa katiba ulio wazi kwa Rais kuchomeka.maneno yake kwenye suala la Kikatiba .
Maneno ambayo hayapo kwenye katiba " kusitisha shughuli za bunge"